Majanga yanayomkabili Ole Gunnar Solskjaer - Je atamaliza msimu ujao akiwa Manchester United

Solskjaer (kushoto) alijasiliwa kwa mkataba wa kudumu mnamo mwezi Machi na kumrithi Mournho kama kaimu mkufunzi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Solskjaer (kushoto) alijasiliwa kwa mkataba wa kudumu mnamo mwezi Machi na kumrithi Mournho kama kaimu mkufunzi

Manchester United wamesafiri umbali wa maili 9000 nchini Australia ili kuanza maandilizi yao msimu ujao kupitia mechi sita , lakini iwapo kocha Ole Gunnar anadhani kwamba umbali huo utamsaidia katika kuyakwepa baadhi ya matatizo ambayo yamekuwa yakiongezeka amekosa.

Ni chini ya miezi miwili tangu United ilipomaliza msimu wake kwa kujipatia pointi moja kutoka mechi za ligi ya Uingereza dhidi ya Huddersfield na Cardiff na katika maandalizi ya msimu ujao mechi yao dhidi ya Perth Glory katika uwanja wa Optus siku ya Jumamosi ilionyesha kwamba matatizo yao bado yapo.

Picha ya kiungo wa kati Paul Pogba aliyenunuliwa kwa dau la £89m ilikuwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la eneo hilo siku ya Jumatano , ikisisitiza umuhimu mkubwa unaozunguka uhusiano mbaya uliopo kati ya United na mchezaji nyota huyo.

Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya mshambuliaji wao Romelu Lukaku aliyenunuliwa kwa dau la £75m akiwa ndiye mchezaji ghali zaidi wa pili katika historia ya United mbali na mlinda lango David De Gea ambaye anatarajiwa kukamilisha mwaka mmoja uliosalia wa kandarasi yake.

Ni wachezaji wawili pekee walioongezwa katika kikosi hicho kilichomaliza katika nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza , na huku Man United ikitumia £60m kumsajili beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka ,21 na Danile James kutoka Swansea, ni wazi kwamba miezi 18 iliopita mchezaji huyo hakucheza hata mechi moja kama mchezaji wa kulipwa.

Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliangazia maswala ambayo kocha Ole Gunnar Solskjaer anafaa kuyatatua kabla United kuanza kampeni yao ya ligi ya Premier dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Old Trafford mnamo tarehe 11 mwezi Agosti.

Tatizo la Pogba

Huwezi kusikiliza tena
Transfer Gossip Extra: Pogba, Neymar & Bale

Haiwezi kusahaulika kwamba hatma ya Pogba itatawala ziara hiyo ya maandalizi na bila shaka swala hilo litajadiliwa hadi kufungwa kwa dirisha la uhamisho siku ya Alhamisi na kuna uwezekano kwamba zaidi klabu za Uhispania zinaweza kusajili wachezaji hadi Septemba 2.

Pogba na mshauri wake Mino raiola , mara mbili wamesema kwamba mshindi huyo wa kombe la dunia angependa kuondoka Man United.

Real Madrid naklabu ya zamani ya Pogba Juventus wana hamu ya kumsajili. Lakini kati yazo hakuna hata moja ambayo imewasilisha ombi, mbali na kusema kuwa zinaweza kuafikia dau linaloitishwa na United la £150m.

Kwa sasa kuna hali ya switofahamu na Pogba ndio kivutia kikuu.

Kanda ya video ya Pogba akikosana na Jesse Lingard walipokuwa wakitembea karibu na hoteli ya timu hiyo baada ya kuwasili Australia siku ya Jumatatu ilionekana kama ushahidi wa kuwepo kwa tatizo katika kambi hiyo.

Kanda nyengine ya video ilionyeshwa wawili hao wakicheka.

Huku hilo likiwa miongoni mwa vitu vinavyovutia hatma ya mchezaji huyo , Solskjaer alihitaji kutatua swala hilo wakati wa mkutano wake na wanahabari alipowasili katika uwanja wa Waca siku ya Jumatano.

Uvumi kuhusu hatma ya nyota huyo ndio iliowavutia waandishi wa habari kumuhoji mkufunzi huyo ambaye alisema kwamba United haina haja ya kumuuza ,mchezaji wake ghali.

Hatahivyo haikusema hawatamuuza .Hawezi . Katika kiwango hiki hakuna anayeweza.

Tatizo la kikosi litatau shida yote iliopo

Iwapo Pogba ndiye tatizo la pekee ambalo linaathiri kikosi chote , lingekuwa swala ambalo lingeweza kutatuliwa. Ukweli ni kwamba sio tatizo hilo pekee.

Lukaku pia yupo katika hali kama hiyo .

Tayari Inter Milan ambaye kocha wake Antonio Conte alidhani kwamba atamsajili mcjhezaji huyo kujiunga na Chelsea 2017 kabla ya kugundua kwamba tayari United na Mourinho walikuwa wamefanya makubaliano na mchezaji huyo anamuhitaji.

Katika kisa cha Lukaku , Solskjaer yuko wazi kukabiliana nacho husuasna wakati huu ambao mchezaji huyo hakuwa akianzishwa mara kwa mara na kiwango chochote cha fedha kitakachowasili kinaweza kuimarisha safu nyengine.

Lakini kama Pogba, hakuna ombi lililowasilihswa hatua inayowaacha wachezaji wote wawili katika hali ya mshikemshike huku ikizidi kuonekana kwamba huenda mshambuliaji huyo wa Ubelgiji akasalia.

Kumekuwa na mazungumzo kwa kipindi kirefu kati ya United na washauri wa kipa huyo.

Msimamo wao uko wazi- Kipa huyo wa Uhispania yuko tayari kusalia Old Trafford.

Lakini ili kufanya hivyo anataka kulipwa mshahara ambao utamuorodhesha miongoni mwa walinda lango wazuri , mbali na kuwa mchezaji bora wa mwaka mara nne katika klabu ya United kati ya misimu minne hadi 2018.

Hilo inamaanisha kwamba anataka kulipwa takriban £400,000 kwa wiki ambazo United inamlipa Sanchez ambaye amekatisha tamaa mashabiki wa timu hiyo.

Muda unayoyoma .

Mnamo mwezi Januari De Gea ataweza kutia saini masharti ya kandarasi yake na klabu yoyote nje ya ligi ya Uingereza.

Hakuna suluhu ya haraka, ndio jibu alilotoa Solskjaer siku ya Jumatano alipoulizwa kwamba alisema mwezi Aprili kwamba United italazimika kutokuwa na huruma katika kukifanyia mabadiliko kikosi hicho.

Badala yake wachezaji wa pekee walioondoka old Trafford ni kiungo wa kati Ander Herrera ambaye kandarasi yake ilikamilika.

Inamaanisha kwamba uamuzi hauwezi kutolewa kuhusu hatma ya kinda wa Aston Villa Axel Tuanzebe ambaye alionyesha umahiri wake akiichezea Aston Villa msimu uliopita na ametia saini kandarasi mpya na United hadi 2022, kwa kuwa Solskjaer hajui la kuchagua.

Mashabiki wameanza kuchoka

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uwanja ambao Man United wanafanyia mazoezi nchini Australia

Sio vigumu kukosolewa na baadhi ya mashabiki wa United kutokana na shaka iliotiliwa busara ya kumsajili Ole Gunnar kuwa kocha wa United.

Usimamizi wake ulionekana kuwa mzuri katika misimu miwili na klabu ya Norway Club Molde lakini ukawa mbaya katika kipindi cha miezi tisa kabla ya kufutwa kazi kama kocha wa Cardiff.

Kazi yake kama kaimu kocha wa mMn United ilikuwa nzuri.

Alishinda mechi nane mfululizo mwanzo wa ukufunzi wake huku akishindwa mara moja katika mechi 17 alizosimamia ikikumbukwa mechi ya marudio ya kombe la mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ufaransa PSG ambapo United ilitoka nyuma 2-0 na kuilza miamba hiyo ya Ufaransa nyumbani ili kutinga robo fainali.

Baadaye United ilishinda mara mbili katika mechi 10 baada ya Solskjaer kupata mkataba wa kudumu.

Walipata pointi mbili katika mechi tano za mwisho katika ligi ya EPL ambapo pointi sita zaidi zingewawezesha kutinga ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

Haki miliki ya picha Getty Images

Hadhi ya Solsjaer kama lajendari wa klabu hiyo inamaanisha kwamba bado anaungwa mkono na mashabiki lakini wengi wanahoji iwapo United ilikosa kwa kumuajiri mchezaji huyo wa zamani badala ya mkufunzi mwenye uzoefu mkubwa ili kumrithi Mourinho.

Na iwapo wengi wanamuunga mkono mkufunzi huyo uhusiano uliopo kati ya naibu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward na mmiliki wa klabu hiyo familia ya Glazer unazidi kuwa mbaya.

Woodward analaumiwa kuwa mtu aliyesababisha United kuwa katika hali ilionayo sasa.

Kutokuwepo kwa mkurugenzi wa kiufundi , kitu ambacho klabu hiyo ilisema ni muhimu baada ya kupigwa klamu kwa Mourinho inaonekana na wengine kama ushahidi kwamba Woodward hataki kuwachilia uwezo wa kutaka kushiriki katika uhamisho wa wachezaji.

Mada zinazohusiana