Nani atamenyana na nani katika Kombe la Mataifa bingwa Afrika 2021?

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2021 kufanyika Cameroon Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2021 kufanyika Cameroon

Droo ya Kombe la taifa bingwa barani Afrika 2021 imefanyika Alhamisi mjini Cairo kabla ya michuano hiyo kufanyika nchini Cameroon.

Algeria, ambao walikutana na Senegal Ijumaa katika fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika la mwaka mjini Cairo, watalaimika kusafiri umbali wa bara zia kwa ajili ya mechi za waliofuzu la mwaka 2021

Katika draw hiyo mbwa mwitu wa jangwani (Desert Foxes) wamepangiwa kucheza katika kundi H pamoja na timu tatu za kusini mwa Afrika , Zambia, Zimbabwe na Botswana.

Mahasimu wa Algeria, Senegal, katika fainali ya Ijumaa , watakuwa katika kundi feature in I dhidi ya Congo Brazzaville, Guinea-Bissau na eSwatini.

Madagascar, ambao kufuzu kwao kwa robo fainali kuliwashangaza wengi katika kombe la AFCON 2019, wamewekwa katika kundi K pamoja na Ivory Coast, Niger na Ethiopia.

Nigeria, waliowapiga Tunisia 1-0 siku ya Jumatano wakiwa katika nafasi ya tatu , watakutana na wenzao wa Afrika magharibi Benin na Sierra Leone pamoja na Lesotho.

Ghana na Afrika Kusini wako kundi C na wote watatakiwa kiufuzu kutokana na kutoshiriki kwa Sudan na washindi wa wa awamu ya kwanza watakutana na Mauritius na Sao Tome e Principe.

Ingawa mwenyeji Cameroon ambaye anafuzu moja kwa moja kutokana na kwamba ndio inayopokea wageni, atalazimika kushiriki mechi ya ushindani na hivyo kuziacha Cape Verde, Msumbiji na Rwanda kushindana na kundi jingine la F.

Uganda, ambayo imekuwa ndio timu thabiti katika eneo la Afrika mashariki katika shindano la mwaka 2019 , wako pamoja na Burkina Faso, Malawi na Sudan kusini au Ushelisheli katika kundi B.

Michuano minne ya awali itachezwa mnamo mwezi wa Octoberna zile za makundi zitaanza mwezi utakaofuatia kwa raundi mbili.

Washindi na timu zitakazochukua nafasi ya pili kutoka kila kundi watafuzu isipokuwa Katika kundi F lenye Cameroon ambao wanafuzu moja kwa moja kama wenyeji .

Jinsi Droo kwa ukamilifu:

Raundi ya kwanza :

Liberia v Chad

South Sudan v Ushelisheli

Mauritius v Sao Tome e Principe

Djibouti v Gambia

Makundi:

A: Mali, Guinea, Namibia, Liberia/Chad

B: Burkina Faso, Uganda, Malawi, Sudan Kusini /Ushelisheli

C: Ghana, Afrika Kusini, Sudan, Mauritius/Sao Tome

D: Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Gabon, Angola, Djibouti/Gambia

E: Morocco, Mauritania, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Burundi

F: Cameroon (wenyeji), Cape Verde, Msumbiji, Rwanda

G: Misri, Kenya, Togo, Visiwa vya Komoro

H: Algeria, Zambia, Zimbabwe, Botswana

I: Senegal, Congo Brazzaville, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani ikiitwa Swaziland)

J: Tunisia, Libya, Tanzania, Equatorial Guinea

K: Ivory Coast, Niger, Madagascar, Ethiopia

L: Nigeria, Benin, Sierra Leone, Lesotho

Haikuingia: Eritrea, Somalia

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii