Manny Pacquiao ampiga Keith Thurman kwa pointi ili kushinda taji la uzani wa Welterweight duniani

Manny Pacquiao Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa Marekani Keith Thurman aliangushwa katika raundi ya kwanza na Manny Pacquiao

Manny Pacquiao amesema kuwa alifurahia pigano lake dhidi ya bingwa wa taji la WBA Keith Thurman ambapo alimshinda kwa pointi na kuwa bingwa mpya wa uzani wa Welterweight duniani akiwa na umri wa miaka 40.

Thurman ambaye alikuwa hajashindwa alikuwa ameahidi kumstaafisha bingwa huyo wa Ufilipino lakini aliangushwa katika raundi ya kwanza kabla ya pigano hilo lililochangamsha kuendelea hadi raundi ya 12.

''Nilijua kwamba mtu yeyote angeibuka mshindi'' , alisema Thurman .

''Aliniangusha katika raundi ya kwanza akapata motisha mkubwa . Lilikuwa pigano zuri sana''.

Thurman mwenye umri wa miaka alitaraji kupata ushindi wake wa 30.

Majaji wawili walisema kwamba Pacquiao alijipatia 115-112 dhidi ya Thurman huku jaji mmoja akimpatia Thurman ushindi wa 114-113 dhidi ya Pacquiao.

Pacquiao ambaye amekuwa bingwa wa dunia katika mizani minane alikuwa akipigana kwa mara ya 71 katika kipindi ambacho ameshindwa mara saba.

Baadaye Pacquiao alisema kwamba alihisi amebarikiwa na kwamba atarudi Ufilipino ili kuendelea na kazi yake ya Useneta kabla ya kuamua kuhusu hatua atakayochukua.

''Nitapigana mwaka ujao''.

Thurman alikuwa na urefu wa kumfikia rahisi Pacquiao na umri mdogo lakini alikuwa nyuma kutoka mwanzo kabla ya kuanza kutokwa na damu puani baada ya raundi ya tano.

Alijikusanya katikati ya pigano lakini Pacquiao alirudi na kumkabilii katika rundi za mwisho za pigano.

Raia huyo wa Ufilipino sasa huenda akapigana dhidi ya Amir Khan wa Uingereza , licha ya kwamba wiki iliopita alikana madai kwamba makubaliano yameafikiwa kwa wawili hao kuzipiga Saudia mnamo mwezi Novemba.

Khan amedai kwamba pigano hilo litafanyika tarehe 8 Novemba.

''Natamani ningeweza kuimarisha mchezo wangu'' , Thurman aliambia vyombo vya habafri nchini marekani.

''Nilihisi kwamba alikuwa amechoka, lakini uzoefu wake ndio uliomuokoa ndani ya ukumbi. Ningependa mechi ya marudiano''.

''Nataka kuwashukuru mashabiki . Nataka kumshukuru kila mtu kwa kuhudhuria pigano hili. Manny Pacquiao ni bondia bora. Na bingwa wa Ukweli''.

Mada zinazohusiana