Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 25.07.2019: Coutinho,Dybala, Gueye, Zaha, Pepe, Eriksen

Philippe Coutinho Haki miliki ya picha Reuters

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, ambaye aliondoka Anfield kwa kima cha £142m mwaka 2018. (ESPN)

Paris St-Germain imekubali kulipa £28m kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, 29, kutoka Everton. (Mail)

Toffees wanaendelea kushauriana na Crystal Palace kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, kwa pauni £80m. (Sky Sports)

Tottenham imewasiliana na Juventus kuhusu usajili wa nyota wa kimataifa wa Argentina international mshambuliaji Paulo Dybala, 25, ambaye bei yake anayekadiriwa kuwa £80m. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paolo Dybala

Manchester United wameomba kufahamishwa kuhusu hatma ya mchezaji Christian Eriksen, 27, wa Tottenham. Kandarasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Denmark amesalia na mwaka mmoja kukamilika na huenda akauzwa kwa pauni milioni 70. (Mail)

United pia inamlenga mshambuliaji wa Lille na nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £70m, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku endapo atajiunga na Inter Milan. (Times)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Romelu Lukaku aliifungia United mabao 15 msimu uliopita

Kiungo wa kati wa Kimataifa wa Serbia na Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 24, amewaambia wachezaji wenzake kuwa ataondoka klabu hiyo msimu huu licha ya tetesi huendaakajiunga na Manchester United. (Il Tempo via Express)

Chelsea na West Ham wanapania kumsajili kwa mkopo winga wa Portsmouth Leon Maloney, 18 ambaye ameifungia Pompey academy mabao 26 msimu uliopita. (Sun)

Wolfsburg na RB Leipzig wanataka kumsajili kwa mkopo winga wa Arsenal wa miaka 18 Muingereza Emile Smith Rowe. (Independent)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Emile Smith-Rowe

Crystal Palace na Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland anayecheza safu ya mashambulizi Jonathan Afolabi ambaye aliondoka Southampton mwisho wa msimu uliopita. (Football.London)

Sheffield United ambao wamepandishwa daraja kushiriki ligi kuu ya Premia wanatafakari uwezekano wa kumnunua kipa wa zamani wa kimataifa wa England Joe Hart, 32, kutoka Burnley. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa wa Burnely Joe Hart

Villa wanashauriana na kipa wa Juventus, Mtaliano Mattia Perin baada ya uhamisho wake £13m kwenda Benfica kugonga mwamba baada ya kukosa uchunguzi wa kiafya. (Football Italia)

Barcelona wameweka dau la £24m kumnunua mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo. (Sport - in Spanish)

Tetesi Bora Jumatano

Paris St-Germain wameishinda Juventus katika kinyang'anyiro cha kumsaini mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, na wanaamini watafikia mkataba wa pauni milioni 20 kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England . (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Naibu mwenyekiti mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yuko mbioni kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wapya, zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kukamilia. (ESPN)

Woodward ana matumaini ya kukamilisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City, Harry Maguire, 26, na mchezaji wa safu ya kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Mlinzi wa Leicester City, Harry Maguire

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado anapania kumnunua mchezaji mwingine mmoja msimu huu. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa safu ya kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24, amesema kuwa ataendelea kucheza katika ligi kuu ya Ureno licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bruno Fernandes

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana wiki mbili kuamua ikiwa atamuachilia winga wa England wa chini ya miaka-21 Reiss Nelson, 19, kujiunga na Hertha Berlin kwa mkopo msimu ujao. (Sun

Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis Muargentina Giovani lo Celso, 23, kwa kima cha pauni milioni 45. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii