Tetesi za soka Ulaya Jumapili 28.07.2019: Maguire, Lukaku, Gueye, Kean, Alves, Bale, Pogba

Pogba

Real Madrid iko tayari kutoa dau la £150m ili kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, baada ya kumuuza Bale. (Sun)

Mkufunzi wa Leicester Brendan Rodgers anasema kuwa klabu hiyo bado haijapokea ofa nzuri ya kumuuza beki wake Harry Maguire licha ya hamu kutoka kwa klabu ya Man United na Manchester City ikiongezea kuwa klabu hiyo inatazama hali hiyo.(Leicester Mercury)

Leicester inataka Man United kulipa dau la juu la £80m kwa kuwa haina uhakika watapokea marupurupu ya nyongeza iwapo Maguire ataisaidia klabu yake kufuzu ligi ya mabingwa. (Mail)

Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, kwa dau la Yuro 70m euros. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, anataka kusalia Juventus na kupigania nafasi yake chini ya usimamizi wa kocha Maurizio Sarri. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku huenda ametoa ishara kwamba huenda akaondoka Man United katika siku chache zijazo baada ya kuchapisha picha katika mtandao wake wa twitter akiwa na ajenti wake.

Haki miliki ya picha AFP

Mchezaji huyo wa Ubelgiji anaashiria kwamba wawili hao huenda wakafanya kazi pamoja.

Mkufunzi wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson anataka klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati wa Uskochi John McGinn - ambaye babu yake ni rafiki wake wa karibu. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales na Real Madrid Gareth Bale, 30, atalipwa mshahara wa £1.1m kwa wiki na atajiunga na Lionel Messi kama wachezaji wanaolipwa mshahara wa juu zaidi duniani baada ya kukubali mktaba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya ligi ya China Jiangsu Suning. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid italazimika kupata hasara ya £86m kutoka kwa Bale iwapo uhamisho wake wa klabu ya Jiangsu Suning utakamilika kabla ya dirisha la uhamisho la China kufungwa siku ya Jumatano.

Klabu hiyo imekataa kutoa dau la uhamisho wake juu ya mshahara mkubwa watakaomlipa winga huyo wa Wales. (Mail)

Newcastle United haitaki kufikisha dau la £20m ambalo Hull City inataka kumnunua mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 Jarrod Bowen. (Newcastle Chronicle)

The Magpies pia wana mpango wa kutoa dau la £5m kumnunua kiungo wa kati wa Everton James McCarthy, 28, ambaye hapendwi tena katika klabu ya Goodison Park. (Sun)

Haki miliki ya picha AFP

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasisitiza kuwa makubaliano hayajaafikiwa na mabingwa wa Ufaransa PSG kuhusu kiungo wa kati Idrissa Gueye, huku mkufunzi huyo wa Ureno akitumai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atasalia katika uwanja wa Goodison Park. (Liverpool Echo)

Hatahivyo, Gueye anatarajiwa kuelekea nchini Ufaransa kufanyiwa ukaguzi wa kimataibabu baada ya kukataa ofa Man United. (Express)

The Toffees wameanzisha mazunguumzo na Juventus kuhusu kumsajili mshambuliaji kinda Moise Kean. Mabingwa hao wa ligi ya Serie A wanataka dau la £36m kwa mchezaji huyo wa Itali na wanasisitiza kuhusu kumnunua tena iwapo timu hiyo itamuhitaji. (Sky Sports)

Wolves wameafikia makubaliano na mabinga wa Itali AC Milan kumnunua mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21 Patrick Cutrone. Klabu hiyo ya ligi ya Premia kwa sasa inajaribu kumrai mchezaji huyo wa Itali kujiunga na klabu ya Molineux. (Express and Star)

Mkufunzi wa klabu ya Crystal Palace Roy Hodgson ana hamu ya kumsajili mchezaji wa West Ham mwenye umri wa miaka 29 Michail Antonio. (Mirror)

Mkufunzi mpya wa Chelsea Frank Lampard ameambia wachezaji Tiemoue Bakayoko na Danny Drinkwater - ambao waligharimu £80m - kwamba wanaweza kuondoka Stamford Bridge. (Mirror)

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Paris St-Germain beki wa kulia Dani Alves, 36, bado anatafuta klabu mpya na kwamba ameandika katika mtandao wake wa instagram akitafuta kazi mpya". (AS)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa Ujerumani Andre Schurrle, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Fulham, anatarajiwa kuondoka Borussia Dortmund ili kujiunga na klabu ya Urusi ya Spartak Moscow. (Bild)

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke Saido Berahino anatarajiwa kuichezea klabu ya Ufaransa Nimes katika mechi ya kirafiki dhidi Toulouse huku klabu hiyo ya daraja la kwanza Uingereza ikijaribu kufutilia mbali kandarasi yake. (Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii