Gareth Bale: Real Madrid yasitisha uhamisho wa bale kuelekea China

Gareth Bale Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Uhamisho wa winga wa Real Madrid kuelekea China umefutiliwa mbali na sasa winga huyo wa Wales anatarajiwa kusalia Real Madrid

Bale, 30, alitarajiwa kujiunga na klabu ya China Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kulipwa £1m kwa wiki .

Wiki iliopita mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane alisema kuwa Bale alikuwa anakaribia kuondoka Madrid baada ya kiwango chake cha mchezo kuzorota.

Zidane aliongezea kwamba kuondoka kwake kutakuwa vyema kwa kila mtu. Bale alijiunga na miamba hiyo ya Uhispania kwa dau lililovunja rekodi la £85m kutoka Tottenham 2013.

Amesalia na kandarasi ya miaka mitatu katika uwanja wa Bernabeu ambapo ameshinda mataji manne ya ligi ya mabingwa Ulaya , taji moja la la Liga, mataji matatu ya Uefa na mataji matatu ya klabu bora duniani.

Alifunga magoli matatu , pamoja na penalti katika fainali nne za ligi ya mabingwa baada ya kushinda kombe hilo 2014, 2016, 2017 and 2018.

Hatahivyo majeraha yamemkwaza kuanzishwa mara 79 katika misimu yote minne akiichezea R Madrid.

Aliichezea Real mechi 42 msimu uliopita lakini alizomelewa na mashabiki wa nyumbani katika mechi kadhaa .

Kurudi kwa Zidane katika timu hiyo kulidaiwa kuwa habari mbaya na ajenti wa mshambuliaji huyo Jonathan Barnett, kwa kuwa raia huyo wa Ufaransa hakutaka kufanya kazi na Bale na wawili hao walitofautiana kuhusu mfumo wa kucheza.

Bale alimaliza msimu uliopita kama mchezaji wa ziada wakati Real Madrid ilIpoandikisha matokeo mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 20 wakishindwa mara 12 na kupata pointi 68 na kuwa katika nafasi ya tatu - pointi 19 nyuma ya mabingwa Barcelona.

Mada zinazohusiana