CHAN 2020: Taifa Stars yaizuia Harambee Stars katika mechi ya kufuzu Tanzania

Walitoka sare ya 0-0 Haki miliki ya picha TFF

Harambee Stars ilitoka sare ya bila kwa bila dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania katika awamu ya kwanza ya michunao ya kufuzu kombe la CHAN 2020 iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam siku ya Jumpili jioni.

Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya iIikuwa Tanzania iliopata fursa chungu nzima , lakini Kenya nayo ilipata nafasi za wazi ambazo zingebadili matokeo iwapo washambuliaji wake wangejinoa makali.

Ikiwa mara ya kwanza kwa kocha Sebastien Migne kuongoza kikosi hicho bila wachezaji wanaocheza ughaibuni , Harambee Stars ililazimisha sare tasa dhidi ya timu ambayo asilimia 60 ya wachezaji wake wamekuwa wakiichezea kwa karibu muongo mmoja.

Tanzania ndio iliopata fursa ya kwanza katika dakika ya tatu , wakati mchezaji wa klabu ya Azam Hassan Dilunga alipopiga kichwa juu ya mwamba wa goli huku mlinda lango wa Kenya John Oyemba akiwa amepitwa- safu ya ulinzi ya Kenya ikionekana kubabaika.

Masikhara ya Clifton Miheso karibia yaipatie Tanzania kupitia mshambuliaji wake John Bosco bao lao la kwanza , lakini mchezaji Joash Onyango alifika kwa haraka na kumzuia mshambuliaji huyo kufunga goli hilo.

Hatahivyo nafasi ya kwanza ya wageni ilikuwepo kunako dakika ya 13 , wakati Musa Masika alipovamia lango la taifa Stars kupitia wingi ya kulia kabla ya kuzuiliwa na Gadiel Michael wakati alipotaka kufanya shambulio.

Haki miliki ya picha TFF

Na baada ya Tanzania kutawala mpira kwa kipindi kirefu wachezaji wa kocha Migne walianza kuonana katika kila pembe na kuanza kulivamia lango la taifa Stars na hivyobasi kupunguza idadi ya mashambulizi ya wenyeji hao katika safu ya ulinzi ya Kenya.

Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza winga wa Harambee Stars alikuwa amebadilisha wingi na kuelekea upande wa kushoto na baadaye katikati huku Kenya ikishindwa kufurukuta

Tanzania hatahivyo ilipata kona mbili mfululizo katika dakika tatu huku Kenya ikijibu kunako dakika ya 49.

Dilunga alidhania kwamba amefunga goli huku muda ukiendelea kuyoyoma lakini bao lake lilidaiwa kuwa la kuotea.

Kulikuwa na shinikizo kali katika safu ya Kenya lakini mlinda lango Oyemba alionyesha umahiri wake katika mechi yake ya kwanza.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii