Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 29.07.2019: Gareth Bale, Bruno Fernandes, Leroy Sane, Nicolas Pepe, Wilfried Zaha

Leroy Sane

Kocha wa Bayern Munich Niko Kovac "ana imani kubwa" mabingwa wa Ujerumani watakamilisha makubalianoya winga wa Manchester City Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 23. (ZDF Sport kupitia Manchester Evening News)

City imemlenga mchezaji wa kiungo cha mbele wa Real Sociedad mwenye umri wa miaka 22 Mikel Oyarzabal kama mchezaji atakayeichukua nafasi ya Sane na wapo tayari kulipa kitita cha Euro milioni 75 zinazohitajika kw a mujibu wa mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania ili kuachiliwa. (AS)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Wales Gareth Bale amekasirishwa na uamuzi wa rais wa Real Madrid Florentino Perez kukatiza uhamisho uliopendekezwa kwenda timu ya Uchina Jiangsu Suning. (Sun)

Perez, mwenye umri wa miaka 72, aliamua kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham mwenye miaka 30, ana thamani kubwa mno kuchukuliwa kwa urahisi huku Jiangsu Suning ikitarajiwa kumsajili katika uhamisho wa bure. (Daily Star)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, hatarajiwi kusafiri kwenda England kufayiwa ukaguzi wa kimatibabu na Manchester United. (Daily Express)

Winga wa Lille Nicolas Pepe, mwenye miaka 24, atakamilisha uhamisho wake wa thamani ya £72m kwenda Arsenal Jumanne au Jumatano -ili mradi mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain hawatojaribu kuteka makubaliano hayo. (La Voix Du Nord)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Blaise Matuidi, mwenye umri wa miaka 32, ana hamu ya kuelekea Manchester United. (Corriere di Torino kupitia Daily Express)

Everton imewasilisha ombi la £55m pesa taslimu kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika Premier League. (Sky Sports)

Palace inataka £60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa. (Daily Mirror)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Everton Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29, amepigwa picha akiwasili katika uwanja wa ndege Paris wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal akikaribia kuelekea kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. (RMC Sport kupitia Liverpool Echo)

Liverpool inapanga kumjumuisha winga mwenye miaka 16 Harvey Elliott katika kikosi cha kwanza msimu huu badala ya kumjumuisha na kikosi cha kinachopokea mafunzo kufuatia uhamisho wake kutoka Fulham. (Liverpool Echo)

Aston Villa imehimizwa katika kumtafuta kwao kwa kipa wa Cardiff City Neil Etheridge, mwenye umri wa miaka 29, baada ya bosi wa Bluebirds Neil Warnock kusema klabu hiyo ipoa tayari kusikiliza maombi. (Wales Online)

Hatahivyo, Villa iliokwea daraja haipo tayari kukutana na thamani ya Burnley ya £10m ya kipa wa England Tom Heaton, mwenye umri wa miaka 33. (Birmingham Mail)

Beki wa kushoto wa Paris St-Germain Stanley Nsoki, mwenye miaka 20, ana hamu ya kuhamia kwa timu iliyomfukuzia kwa muda mrefu Newcastle United, licha ya kwamba klabu hiyo bado ingali kufikia thamani iliyoitishwa na mabingwa hao wa Ufaransa ya £13.5m. (Newcastle Chronicle)

Watford ingali katika mazungumzo na klabu ya Ufaransa Rennes kuhusu kiungo cha mbele wa Senegal, Ismaila Sarr, mwenye miaka 21, licha ya kwamba makubaliano ya gharama yanadhaniwa kukaribia kukamilika.(Watford Observer)

Winga wa Liverpool Ryan Kent hatoondoka Anfield tena kwa mkopo, na kuipa pigo matumaini ya timu bingwa ya Uskotchi Rangers ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22 katika mgeuzi mengine ya muda mfupi. Hilo huenda likatoa fursa kwa Aston Villa au Leeds United kumpata Kent katika uhamisho wa £10m. (Daily Record)

Mabingwa Blackburn Rovers bado wana imani ya kumsajili beki wa kati wa Manchester City Tosin Adarabioyo, mwenye miaka 21, kwa mkopo wa msimu mzimu huku mchezaji wa Fortuna Dusseldorf Robin Bormuth, mwenye umri wa miaka 23, na wa Norwich Grant Hanley, wa miaka 27, huenda pia wakawasili. (Lancashire Telegraph)