Mohamed Elneny: Mwili wapatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal nchini Misri

Mohamed Elneny (kushoto) amejiunga na Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la Afcon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mohamed Elneny (kushoto) amejiunga na Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la Afcon

Mwili wa mtu umepatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny nchini Misri.

Babake Elneny, Nasser aliupata mwili huo wakati alipotembelea nyumba hiyo mjini Mahalla al-Kubra , ambayo iko takriban kilomita 100 kaskazini mwa Cairo.

Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi, ambaye wanasema mtu huyo alikuwa akijaribu kuiba nyaya za umeme.

Inaaminika kwamba alichomwa na umeme wakati wa wizi huo. Nyumba hiyo ni mali mpya ambayo ilitolewa na familia ya Elneny kutumika kama ofisi.

Elneny ambaye amerudi Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la mataifa ya Afcon , aliambiwa kuhusu kisa hicho kupitia simu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii