Maldini, Zidane, Kluivert, Hagi, Weah - Wana wa wachezaji waliotia fora

Haki miliki ya picha Getty Images

Wanao wachezaji waliotia fora wameanza kuingia katika soka ya kulipwa, wafuatao ni baadhi ya majina maarufu

Daniel Maldini - 17, AC Milan

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daniel Maldini alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuchezeshwa na AC Milan katika kombe la kimataifa

Paolo Maldini ni gwiji wa klabu ya AC Milan na klabu hiyo ilijulikana kama 'klabu ya mtu mmoja'.

Beki huyo alicheza mechi 902 ikiwemo mechi 647 katika ligi ya Seria A - na kushinda mataji matano ya Ulaya na mataji saba ya ligi ya mabingwa akicheza kwa karibia miaka 25

Kwa kuichezea Rossoneri Daniel pia anafuata nyayo za babu yake, Cesare ambaye aliichezea Milan mara 300 katika miaka ya hamsini na sitini kabla ya kuifunza klabu hiyo.

Kipindi cha mchezo cha Daniel kufikia sasa: Alianza kuichezea rasmi AC Milan wiki hii katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich.

Cha kushangaza: Jezi nambari tatu iliofanywa maarufu na Paolo ilistaafishwa wakati Maldini alipostaafu lakini ameiruhusu klabu hiyo kuitumia tena iwapo mwanae ataichezea klabu hiyo.

Justin Kluivert - 20, Roma

Patrick Kluivert aliichezea miamba ya Ajax, AC Milan na Barcelona wakati wa kipindi chake cha mchezo ambapo alifunga magoli 205.

Katika mechi 79 akiichezea Uholanzi alifunga magoli 40 na kuwasaidia katika nusu fainali ya kombe la dunia 1998.

Alishinda mataji machache, ikiwemo lile la Eredivise mara mbili, La Liga na lile la klabu ya mabingwa ambapo alifunga goli la ushindi wakati alipokuwa na umri wa miaka 18.

Kipindi cha mchezo wa Justina kufikia sasa: Yeye pia alianza kuichezea Ajax na kufunga goli lake la kwanza miaka kumi na siku moja tangu babake kufunga goli lake la mwisho.

Pia alishinda medali ya nafasi ya pili ya Ulaya katika kipindi cha mwaka 2016/17. Kama babake, alielekea Itali baada ya kusainiwa na klabu ya Roma mwaka 2018.

Ijapokuwa anajaribu kuingia katika kikosi cha kwanza cha timu alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Roma kufunga goli katika ligi ya mabingwa msimu uliopita baada ya kufunga dhidi ya Viktoria Plzen, likiwa bao lake la kwanza la klabu hiyo.

Cha Kushangaza: Anavalia jezi nambari 34 kumkumbuka mchezaji mwenza wa babake Abdelhak Nouri ambaye alipatwa na mshutuko wa moyo 2017 na hivyobasi kustaafu katika soka.

Timothy Weah - 19, Lille

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Timothy Weah alitia saini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Lille mwezi Juni baada ya kukosa kujumuishwsa katika kikosi cha kwanza PSG

Babake alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda taji la Ballon d'Or. Kwa sasa ndiye rais wa taifa la Liberia.

Goerge Weah alijitengenezea jina lake nchini Ufaransa wakati aliposajiliwa na Arsene Wenger kutoka Monaco kwa dau la £12,000.

Alikuwa mchezaji maarufu duniani nchini Italy na kuisadia AC Milan kushinda mataji mawili ya ligi , Ballon D'Or na kufunga goli maarufu ambapo alitamba na mpira kutoka upande mmoja wa kiwanja na kuwachenga karibia wacheza wote wa klabu ya Hellas Verona kabla ya kufunga.

Licha ya kumili magoli 200 aliyofunga , Weah alistaafu na kuingia siasa ambazo zimefanya kuwa rais wa Liberia 2018 na baadaye kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria baadaye mwaka huo akiwa na umri wa miaka 51.

Kipindi cha mchezo wa Timothy kufikia sasa: Akianza kusakata soka katika klabu ya New York red Bull , mchezaji huyo wa Marekani alifuata nyanyo za babake akitia saini kandarasi yake ya kwanza na klabu ya PSG.

Ni wazi kwamba ingekuwa vigumu kubeba jina lake huku timu hiyo ikiwa na wachezaji maarufu kama vile Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani.

Hivyobasi baada ya kuhudumu kwa mkopo katika klabu ya Celtic haishangazi kwamba aliamua kuelekea katika klabu ya Lille nchini Ufaransa.

Cha kushangaza: Gianluigi Buffon alianza kuichezea Parma mwaka 1995, akicheza bila kufungwa na klabu ya George weah ya AC Milan.

Na miaka 23 baadaye , Buffon alicheza kama mchezaji mwenza wa mwanawe akiwa PSG.

Ianis Hagi - 20, Genk

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ian hagi alifunga magoli mawili dhidi ya Romania na kufika nusu fainali ya kombe la mabingwa ulaya mwezi JUlai akichezea timu ya wachezai wasiozidi umri wa miaka 21

Akiwa maradona wa Carpathians' {mlima mmoja nchini Romania ) Gheorghe Hagi - ni mchezaji nyota aliyeichezea Real Madrid, Barcelona na Galatasaray - alitajwa kuwa mojawapo ya wachezaji wazuri zaidi duniani katika miaka 80 na 90.

Kiungo huyo mshambuliaji alicheza mara 125 na ametajwa kuwa mchezaji bora nchini Romania.

Mchezo wa Ian kufikia sasa: Akichaguliwa mara mbili kama mshindi wa tuzo ya Golden Boy, talanta yake imeonekana.

Alianza kucheza soka katika taasisi ilioanzishwa na babake na baadaye ikafunzwa na Gheorghe huko Viitorul Constanta.

Ijapokuwa uhamisho wake kutoka Romania hadi Fiorentina haukufanya kazi, Ian alijipatia matumaini katika klabu ya Viitorul kabla ya kuelekea klabu ya Genk nchini Ubelgiji - klabu ambayo ilizindua mchezo wa Kevin De Bryune, Divock Origi na Thibaut Courtois.

Cha kushangaza: Babake alimfanya nahodha wa klabu ya Viitorul Constanta akiwa na umri wa miaka 20.

Luca Zidane - 21, Racing Club Santander ( kwa mkopo)

Luca Zidane - 21, Racing Club Santander (on loan)

Kuwa Zinedine Zidane - mmoja ya wachezaji bora zaidi duniani , alieshinda kila kitu ambacho mchezaji na mkufunzi alitaka kushinda.

Mchezo wa Lucas kufikia sasa: Amepanda ngazi katika klabu ya Real Madrid , akifuzu kuchezea timu ya wachezaji wa ziada na hadi katika kikosi cha kwanza cha timu huku babake akiwa mkufunzi.

Akilinganishwa na wachezaji wengine wa magwiji wa soka waliopita , hajafuata nyayo za babake akicheza kama mlinda lango badala ya safu ya kati.

Cha kushangaza: Ni mchezaji wa pili kati ya wanne ambao wametoka katika taasisi ya Real Madrid.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii