Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 31.07.2019: Umtiti, Neymar, Tierney, Icardi, Chalov, Sane, Mourinho

Manchester United wana nia kusaini mkataba na kiungo wa kati- nyuma wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti
Image caption Manchester United wana nia kusaini mkataba na kiungo wa kati- nyuma wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti

Manchester United wana nia kusaini mkataba na kiungo wa kati- nyuma wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 25. (Le10 Sport )

Paris St-Germain wameweka turufu yao ya uhamisho wa mshambuliaji wao Neymar mwenye umri wa miaka 27 kwa Barcelona. (Marca)

Arsenal wanakamilisha mkataba kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kushoto-nyumba wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Paris St-Germain wameweka turufu yao ya uhamisho wa mshambuliaji wao Neymar kwa Barcelona

Kiungo wa safu ya mashambulizi wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuwa anaelekea Napoli kwa mkataba wa euro milioni 80 (£73m) . (Corriere dello Sport - in Italian)

Crystal Palace wameweka dau la takriban pauni milioni 14 kwa ajili ya mshambuliaji wa timu za CSKA Moscow na Urusi -Fedor Chalov mwenye umri wa miaka 21 . (Sky Sports)

Mkurugenzi mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema hakuelewa ni kwanini meneja Niko Kovac alisema kuwa klabu hiyo inaamini itasaini mkataba na winga Mjerumani Leroy Sane ambaye anaichezea sasa Manchester City akiwa na umri wa miaka 23. (Bild - in German)

Image caption Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuwa anaelekea Napoli

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hafahamu ikiwa kiungo wa kati wa mashambulizi wa timu ya Colombia -James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao. (Marca)

West Brom hawajapokea ofa yoyote kutoka kwa Aston Villa kwa ajili ya winga wa uskochi Matt Phillips, mwenye umri wa miaka 28. (Birmingham Mail)

Mlindalango wa Newcastle na England wa kikosi cha walio chini ya umri wa miaka -21 Freddie Woodman,ambaye ana umri wa miaka 22, analengwa na Celtic na Arsenal, pamoja na klabu ambazo hazijatajwa za Championi. (Chronicle)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hafahamu ikiwa James Rodriguez atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao

Newcastle wamekataliwa dau la pauni milioni 4.5 kwa jili ya kiungo wa kulia nyuma wa Amiens na Sweden Emil Krafth mwenye umri wa miaka 24 . (Sun)

Mchezaji wa klabu ya Partizan ya Serbia anayecheza safu ya kati-nyuma Strahinja Pavlovic, mwenye umri wa miaka 18, "ameshangazwa " na tetesi zinazomuhusisha na kuhamia Celtic. (Daily Record)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Freddie Woodman , analengwa na Celtic na Arsenal

Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho atarejea katika utawala wakati fursa itakapojitokeza. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Teddy Sheringham anasema Ole Gunnar Solskjaer anapaswa kumuuza kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26. (Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho atarejea katika utawala fursa itakapojitokeza

Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Koke anasema kuwa anaamini mshambuliaji wa Ureno Joao Felix mwenye umri wa miaka 19-atakuwa "mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani . (ESPN)

Preston North End wamekatalia mbali dau la deni kutoka kwa Wigan Athletic kwa ajili ya kiungo wa kati Daniel Johnson mwenye umri wa miaka 26-mzaliwa wa Jamaica. (Lancashire Evening Post)

Bora za kutoka Jumanne

Mchezaji mwenza wa Neymar katika kikosi cha Paris St-Germain Marco Verratti anakiri kuwa klabu hiyo lazima imuuze mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- raia wa Brazil ikiwa hana raha katika Parc des Princes, licha ya kocha Thomas Tuchel wa kutaka mchezaji huyo abaki kikosini. (Express)

Juventus amethibitisha kuwa kumekuwa na ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa Manchester United na Tottenham ya kumnunua . (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki Bernabeu

Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 28, kwamba atakuwa katika Bernabeu. (AS - in Spanish)

Crystal Palace wamepanga kuwasilisha dau la pauni milioni 5 la kutaka kumnunua mchezaji wa Newcastle na Jamuhuri ya Ireland anayecheza safu ya kati nyuma Ciaran Clark, mwenye umri wa miaka 29. (sun)

Everton wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, mwenye umri wa miaka 25, pamoja na mchezaji wa Chelsea na England kutoka kikosi cha vijana wenye umri wa chini ya miaka -21 Fikayo Tomori, mwenye 21 anayecheza katika safu ya ulinzi . (Sky Sports)

Meneja wa Newcastle Steve Bruce haamini kuwa mashabiki wa klabu hiyo watasusia mechi ya kwanzaya msimu dhidi ya Arsenal. (Talksport)

Swansea City wanaangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Mskochi Oli McBurnie mwenye umri wa miaka 23 kutoka Sheffield United. (Wales Online)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Everton wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina

Real Madrid wamepokea ofa kutoka kwa Roma na Monaco kwa ajili ya mshambuliaji wa Dominican Mariano, mwenye umri wa miaka 25. (AS - in Spanish)

Lille wanaangalia uwezekano wa kuwaajiri washambuliaji wawili au watatu kwa Euro milioni 115 (£104m) wanazotarajia kuzipata kutokana na mauzo ya wachezaji Nicolas Pepe na Rafael Leao. (RMC Sport - in French)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Ujerumani Jurgen Klinsmann, mwenye umri wa miaka 55 Jumanne anafanya mazungumzo na VfB Stuttgart ili kuwa mkurugenzi wao mkuu wa kwanza kabisa. (Bild - in German)

Mlindalango wa Real Madrid Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, hana uhakika kuhusu mwango wa La Liga baada ya kuumia kiwiko . (Evening Standard)

kiungo wa kati wa Ireland midfielder Sam Foley,mwenye umri wa miaka 32,ambaye ni wakala huru ,anakamilisha taratibu za kuhamia St Mirren. (Record)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Newcastle Steve Bruce haamini kuwa mashabiki wa klabu hiyo watasusia mechi ya kwanzaya msimu dhidi ya Arsenal

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, hatarajiwi kusafiri kwenda England kufayiwa ukaguzi wa kimatibabu na Manchester United. (Daily Express)

Winga wa Lille Nicolas Pepe, mwenye miaka 24, atakamilisha uhamisho wake wa thamani ya £72m kwenda Arsenal Jumanne au Jumatano -ili mradi mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain hawatojaribu kuteka makubaliano hayo. (La Voix Du Nord)

Haki miliki ya picha AFP

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Blaise Matuidi, mwenye umri wa miaka 32, ana hamu ya kuelekea Manchester United. (Corriere di Torino kupitia Daily Express)

Everton imewasilisha ombi la £55m pesa taslimu kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika Premier League. (Sky Sports)

Palace inataka £60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa. (Daily Mirror)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii