Harry Maguire: Man Utd yamfanya beki wa Leicester kuwa ghali zaidi duniani

Harry Maguire na mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Maguire (kulia) scored alifunga magoli matano katika mechi 76 alizochezea Leicester

Manchester United imemsaini beki wa kati a Uingereza Harry Maguire kutoka kwa wapinzani wao Leicester kwa dau la £80m - ikiwa ndio dau lililovunja rekodi ya beki ghali zaidi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kuweka kandarasi ya miaka 6 katika uwanja wa Old Trafford, huku akiwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja.

Dau hilo la Maguire limepiku lile la £75m la Liverpool wakati walipomsaini beki Virgil van Dijk kutoka Southampton Januari 2018.

''Wakati Man United inapoanza kukulizia , ni fursa nzuri'', alisema Maguire.

Maguire ndiye mchezaji wa pili ghali zaidi kusainiwa katika ligi ya Uingereza baada ya Paul Pogba aliyejiunga na Man United kwa dau la (£89m), na anakuwa mchezaji wa pili ghali wa Uingereza aliye ghali baada ya winga wa Wales Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka Tottenham kwa dau la £85m mwaka 2013.

Ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer, baada ya Aaron wan Bisaka kuwasili kutoka Crystal Palace kwa dau la £50m huku naye winga Daniel James akijiunga na miamba hiyo kutoka Swansea kwa dau la £15m.

Maguire aliongezea: kufuatia mazungumzo yetu na mkufunzi, ninafurahia kuhusu maono na mipango aliyonayo kwa timu. Ni wazi kwamba Ole anajenga timu itakayoshinda mataji.

Kwa sasa nataraji kukutana na wachezaji wenzangu kabla ya msimu kuanza.

Solskjaer: Harry ni miongoni mwa wachezaji bora katika mchezo huu leo. Anajua kusoma mchezo na uwepo wake katika uwanja unaonekana huku akiwa na uwezo wa kutulia kunapotokea shinikizo.

Takwimu za mabeki wa kati tangu msimu wa 2016-17 season
Maguire Van Dijk Laporte Ramos Koulibaly Hummels Umtiti Kompany Pique De Ligt
Dakika walizocheza 8,326 7,492 8,439 7,253 8,672 6,170 5,512 3,442 7,975 6,447
Makabiliano 148 102 144 122 169 145 86 50 116 82
makabiliano angani(%) 71% 74% 67% 65% 57% 66% 65% 72% 71% 62%
Kuharibu mipira 148 141 140 141 146 144 102 48 104 107
Kuondoa hatarai 469 499 341 268 362 172 166 167 376 317
makosa yaliosababisha magoli 1 1 0 1 4 2 1 0 3 4

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii