Tetesi za soka Ulaya Jumapili 11.08.2019: Pogba, Neymar, Moyes, Dybala, Khedira, Bolasie, Mourinho

Haki miliki ya picha Getty Images

Juventus haijapoteza hamu ya kumsaini kiungo wakati wa Man United Paul Pogba, 26. (Express)

Pogba anasisitiza kuwa hataleta mgawanyiko miongoni mwa wachezaji licha ya madai kwamba alitaka kuondoka Trafford. (Mirror)

Paris St-Germain ina hamu ya kuafikia mkataba utakayoifanya Real Madrid kumnunua mshambuliaji wake raia wa Brazil Neymar, 27, kutoka kwao kwa dau la £149m mbali na klabu hiyo kuikabidhi kiungo wake wa kati raia wa Croatia Luka Modric, 33. (Times - subscription required)

Real Madrid iilikuwa imeipatia PSG ofa ya £85m pamoja na mshambuliaji wake Gareth Bale, 30, ili kumnunua Neymar. (Mundo Deportivo, via Express)

Neymar

Bayern Munich inakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Croatia Ivan Perisic, 30, kutoka Inter Milan. Timu hizo mbili zinakamilisha makubaliano ambayo yatamfanya mchezaji huyo kuhamia kwa mkopo pia kukiwa na fursa ya kumnunua mchezaji huyo kwa dau la £23.5m. (Sky Italia via Sky Sports)

Beki wa Tottenham Serge Aurier anataka kuondoka katika klabu hiyo huku AC Milan na klabu yake ya zamani PSG zikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Coast . (Mail)

Manchester United hawana hakika iwapo mlinda lango David de Gea atatia saini kandarasi mpya . Kandarsi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 inakamilika msimu ujao na raia huyo wa Uhbispania yuko hurru kuanza mazungumzo na klabu za kigeni mwezi Januari(Mirror)

David de Gea

Ombi la Manchester United kumsaini kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb kwa dau la £24m Dani Olmo limekatalia kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la England siku ya Alhamisi .(Sportske Novosti via Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Everton na Manchester United David Moyes amerodheshwa miongoni ma wakufunzi wanaotarajiwa kuifunza klabu ya David Bechkam ya Inter Miami. (Mirror)

Mshambuliaji wa Juventus na raia wa Argentine Paulo Dybala, 25,alidafiri na timu yake kw amechi ya mwisho ya maandalizi ya msimu dhidi ya Atletico Madrid mjini Stockholm licha ya hamu kutoka kwa klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa. (Mail)

Paulo Dybala Haki miliki ya picha Getty Images

Juventus imevunjwa tamaa na kiungo wa kati wa Ujerumani Sami Khedira baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kukataa ofaa kadhaa za uhamisho ikiwemo moja kutoka klabu ya Wolves akijaribu kushikilia ofa kutoka Arsenal ambayo haikufua dafu. (Calciomercato via Sun)

Celtic, Besiktas na Rennes wote wanatafuta saini ya mchezaji wa klabu ya Everton na DR Congo Yannick Bolasie, 30, ambaye amekataa ofa moja ya kuhamia katika klabu ya Urusi ya CSKA Moscow. (Goal)

Jose Mourinho amechukua kazi kama mchanganuzi na chombo cha habari cha Sky Sports na jukumu lake la kanza litakuwa mechi ya Jumapili kati ya timu zake za zamani Manchester United na Chelsea. (Sky Sports)

TETESI ZA JUMAMOSI

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha Alex Morton

Roma wamefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 30. (Telegraph)

Wachezaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, ambao wanadaiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wanajadiliana kuhusu kurefushwa kwa mikataba yao. (Sun)

Paris St-Germain wanataka kumsaini mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala baada ya uhamisho wa nyota huyo wa miaka 25 kwenda kutibuka. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paulo Dybala

Juventus itaendelea kupokea ofa ya kumuuza Dybala na wako tayari kumkabidhi kiungo huyo kwa klabu yoyote isipokuwa Inter Milan. (Calciomercato)

Kipa wa Manchester United David de Gea bado hajatia saini mkataba mpya baada ya kukubali mkataba mpya wa miaka sita na United mwezi uliopita.(Sun)

Arsenal wako tayari kupokea ofa ya kumuuza beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, na kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny, 27, kutoka kwa vilabu vya Ulaya. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David de Gea, Kipa wa Manchester United

Roma wanashauriana na Liverpool kuhusu mkataba wa thamani ya euro milioni 20 (£18.6m) kumhusi beki wa Croatia Dejan Lovren, 30. (Football Italia)

Real Madrid na Barcelona huenda wakamng'ang'ania mshambuliaji wa PSG na nyota wa Brazil Neymar, 27. (AS)

Chelsea wanajiandaa kutumia £200m kuwasajiklili wachezaji wapya mwaka huu wanaposubiri kukamilika kwa marufuku ya uhamisho wa wachezaji waliowekewa na shirikisho la soka Duniani FIFA. (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Chelsea watampatia mkataba mpya mlinzi wa chini wa chini ya miaka 21 Fikayo Tomori, 21, baada ya kupinga uhamisho wake kwenda Everton. (Goal)

Bekiwa Argentina Marcos Rojo, 29, alikuwa tayari kujiunga na Everton kwa mkopo kutoka Manchester United, lakini United wanataka kumuuza. (Liverpool Echo)

Manchester United walikuwa wanatafajkari uwezrkano wa kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao wa miaka 25 Mhispania Inaki Williams kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (El Chiringuito, via Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marcos Rojo (kulia)

Winga wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, atasalia Crystal Palace hadi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parrish kusema hatapinga uhamisho wake katika klabu ya Ulaya . (Express)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 20, amesema mwaka huu anayetazamia kukabiliana na mchezaji mpya wa Tottenham Mfaransa Tanguy Ndombele, 22 . (Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa West Ham, Declan Rice

Mshambuluaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, amekabidhiwa jezi nambari saba ya Real Madrid- iliyovaliwa na Cristiano Ronaldo alipokuwa akichezea klabu hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic alitumia maneno makali kuukosoa mfumo mpya wa michuano ya soka ya ligi ya Major . (ESPN)

Mshambuliaji wa zamani wa Stoke City Saido Berahino, 26, amejiunga na klabu ya Ubelgiji ya Zulte Waregem kwa uhamisho wa bila malipo. (Mail)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mshambuluaji wa Ubelgiji, Eden Hazard

Nahodha wa Crystal Palace, Luka Milivojevic ametia saini mkataba mpya wa miaka minne. (Talksport)


Tetesi Bora Ijumaa

Kiungo wa kati wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, amepata pigo baada ya uhamisho wake kwenda Everton kutibuka lakini amesisitiza anataka kuondoka Selhurst Park. (Telegraph)

Zaha anahofia amepoteza nafasi ya kuhama kwa kitita kikubwa imepotea baada ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa siku ya Alhamisi. (Mail)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wilfried Zaha

Meneja wa Palace Roy Hodgson alimzuia Zaha kufanya mazoezi siku ya Alhamisi kwa sababu mchezaji huyo ''hakuwa na utulivu wa kiakili'' baada ya kuwasilisha barua ya kuomba uhamisho. (Mirror)

Real Madrid wanaamini wamemkosa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, baada ya United kutoimarisha safu yake ya kati siku ya mwisho wa uhamisho wa wachezaji.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Uhispania maarufu La Liga, badala yake imeelekeza darubini yake kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27. (Marca)

Hofu ya kikosi cha kwanza kitakacho cheza chini ya meneja mpya wa Chelsea Frank Lampard imemfanya beki wa Brazil David Luiz, 32, kushinikiza uhamisho kwenda Arsenal. (Standard)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Neymar

Tottenham walipata pigo baada ya Sporting Lisbon kukataa kupunguza bei ya kiungo wao wa kati Mreno Bruno Fernandes, 24. (Mirror)

United ilipuuza nafasi ya kumsajili mshambuliaji Moise Kean kutoka Juventus, kabla ya kiungo huyo wa miaka 19 kujiunga na mahasimu wao Everton. (90min)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii