Super Cup: Liverpool yailaza Chelsea na kuwa mabingwa

Adrian alikuwa shujaa alipozuia penalti ya Tammy Abraham Haki miliki ya picha Reuters

Liverpool ilishinda kombe la Super Cup kwa mara ya nne katika historia kwa kuilaza Chelsea 5-4 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2 mjini Istanbul.

Kipa Adrian alizuia penalti iliopigwa na mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham kuwapatia ushindi mabingwa hao wa kombe la mabingwa Ulaya.

Chelsea ilikua imechukua uongozi katika kipindi cha kwanza kupitia Olivier Giroud lakini Sadio Mane alifunga mara mbili kuipatia uongozi Liverpool.

Penalti ya Jorginho ilisababisha mikwaju ye penlati kupigwa ambapo Liverpool iliibuka washindi.

Ushindi huo unajiri miezi miwili tu baada ya Jurgen Klopp kushinda taji lake la kwanza kama mkufunzi wa Liverpool wakati alipoiongoza Reds kuishinda Tottenham katika fainali ya kombe la mabingwa.

Kwa nini kombe la Super Cup ni muhimu

Haki miliki ya picha Getty Images

Kombe la Uefa Super Cup litachezwa leo siku ya Jumatano ambapo mabingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya Liverpool itakabiliana na Chelsea nchini Ituruki.

Ni fursa kubwa kwa timu hizi mbili kushinda taji lao la kwanza msimu huu , lakini je kombe hili lina umuhimu gani?

Hizi hapa sababu tano

Ni mara ya kwanza kwa timu za Uingereza kukutana katika historia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Liverpool ilikuwa timu ya mwisho ya Uingereza kushinda kombe la Super Cup wakati walipoilaza CSKA Moscow Mwaka 2005. The Reds ilishinda 3-1 baada ya muda wa ziada

Kombe la Super Cup limebebwa sana na klabu za Uhispania hali ya kwamba limepata makaazi mapya nchini humo katika siku za hivi karibuni huku washindi watano wa kombe hilo wote wakitoka Uhispania.

Lakini kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 litaelekea Uingereza mwaka huu huku mechi hii ikiwa ya kwanza kupiganiwa kati ya timu mbili za ligi ya Premia.

Kwa jumla fainali saba za kombe la Super Cup zimekuwa kati ya wapinzani kutoka Uhispania ikiwemo timu nne tangu 2014 na timu mbili zote kutoka Itali.

Fainali za Super Cup kati ya wapinzani
1990 Milan v Sampdoria Milan ilishinda 3-1 kwa jumla
1993 Parma v Milan Parma ilishinda 2-1 kwa jumla
2006 Sevilla v Barcelona Sevilla ilishinda 3-0
2014 Real Madrid v Sevilla Real Madrid ilishinda 2-0
2015 Barcelona v Sevilla Barcelona won 5-4 baada ya muda wa ziada
2016 Real Madrid v Sevilla Real Madrid won 3-2 baada ya muda wa ziada
2018 Atletico Madrid v Real Madrid Atletico Madrid won 4-2 baada ya muda wa ziada

Historia itawekwa

Refa anayesimamia mechi hiyo ataangaziwa sana kwa sababu kwa mara ya kwanza katika historia ya fainali hiyo mwanamke atasimamia mechi kubwa barani Ulaya.

Raia wa Ufaransa Stephanie Frappart atasimamia na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema: Nafurahia sana ni fursa ilionishangaza. Sikutarajia kupewa kazi ya kusimamia kombe la Super Cup -

Ni heshima kubwa sana kwangu na marefa wanawake. Natumai itakuwa kama mfano kwa marefa wanawake na wasichana wadogo ambao wana ndoto za kuwa marefa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Liverpool ilishinda mechi yake ya ufunguzi ya ligi ya Premia huku Chelsea ikipoteza mechi yake

Kulikuwa na mvua ya magoli katika raundi ya kwanza ya mechi za ligi ya Premia na timu zote mbili Liverpool na Chelsea zilihusika katika mechi zenye magoli mengi.

Liverpool ilianza msimu wake kwa mguu mzuri baada ya kuilaza Norwich magoli 4-1 huku Chelsea nayo ikipoteza 4-0 dhidi ya Manchester united siku ya Jumapili.

Hii itakuwa mara 11 kwa Liverpool na Chelsea kukutana. Kihistoria hatahivyo , mechi zinazochezwa Ulaya kati ya timu hizo mbili zimekuwa ngumu.

Liverpool imeshinda mara mbili ikilinganishwa na Chelsea ambayo imeibuka mshindi mara tatu

Taji la kwanza kati ya masita yanayowaniwa na Liverpool?.

Liverpool ilianza msimu ikiwa na fursa ya kushinda mataji saba lakini walikosa kombe la kwanza kwa msimu wa 2019-20 wakati walipopoteza kwa Man City katika kombe la Community Shield.

Bado mataji sita hayajawahi kushindwa kwa msimu mmoja England. Timu ilioweza kushinda mataji mengi zaidi katika msimu mmoja ni Man City ilioshinda mataji manne - moja la Premier League, lile la League Cup, Community Shield na Club World Cup msimu 2008-09.

Mataji yanayowaniwa na Liverpool msimu huu
Champions League
Premier League
FA Cup
League Cup
Super Cup
Club World Cup
Community Shield*

Ni watu wachache wanafurahia mechi ya Super Cup zaidi ya mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp.

Hii ni kombe lake kubwa la Ulaya katika kipindi cha miaka mitatu na itakuwa mara ya kwanza kuwahi kuifunza timu katika kombe la Super Cup , baada ya kupoteza fainali ya kombe la Champions League na lile la Europa League.

Alisema: Kombe la Super Cup lenyewe sio kombe ambalo nimependelea kutazama katika siku za nyuma.

Lampard anaweza kushinda taji lake la kwanza kama mkufunzi wa Chelsea

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huu ni msimu wa pili wa Lampard kuwa mkufunzi baada ya kuifunza Derby County

Mkufunzi huyo wa mpya wa Chelsea alitazama huku kikosi chake kichanga kikishindwa magoli 4-0 na wapinzani wao Man United ijapokuwa matokeo hayo yalikuwa mabaya sana kwa The Blues ambao walitawala mpira kwa asilimia 55.

Walitawala katika kipindi cha kwanza na kugonga mwamba wa goli mara mbili lakini pengine walishindwa kutokana na washambuliaji wachanga walioshirikishwa kama vile Tammy Abraham na Mason Mount ambao walikuwa wakishiriki katika ligi ya Premia kwa mara ya kwanza.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii