Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 16.08.2019: Pogba, Maguire, Eriksen, Sanchez, Dybala, Neymar, Balotelli

POgba Haki miliki ya picha Getty Images

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, bado ana hamu kubwa ya kutaka kuondoka Manchester United kuelekea Real Madrid msimu huu wa joto. (Marca)

Beki wa kati wa England Harry Maguire, mwenye miaka 26, amekataa pendekezo la thamani ya £278,000 kwa wiki kutoka Manchester City badala ya kujiunga na timu hasimu United. (Star)

Meneja wa United, Ole Gunnar Solskjaer amefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham, Christian Eriksen kuhusu uwezekano wa uhamisho kuelekea Old Trafford, hatahivyo mchezaji huyo wa miaka 27alikuwa anataka kusubiria uhamisho kuelekea Uhispania. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa United na timu ya taifa ya Chile, Alexis Sanchez, aliye na umri wa miaka 30, yupo tayari kwa uhamisho kuelekea Italia , wakati Juventus, Napoli, AC Milan na Inter Milan zote zikiwania kumsajili. (Mirror)

Sanchez atashinikiza uhamisho kuondoka Old Trafford kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya Septemba 2. (Times)

Kwa upande mwingine, United imeshindwa kupata mnunuzi wa Sanchez- anayepokea malipo ya £560,000 kwa wiki. (Mirror)

Juventus bado inatumai kumuondoa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Argentina, Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya - licha ya kwamba mabingwa hao wa Italia bado hawajapokea maombi thabiti kwa mchezaji huyo. (Independent)

Huwezi kusikiliza tena
Watch as Colombian U21 player Anderson Diaz scores a Maradona-like Wonder goal

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain, Leonardo anasema mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil, Neymar "amefanya makosa" lakini amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 27 yupo Paris "kwa miaka mitatu". (RMC)

Kipa wa Stoke City na timu ya taifa ya England Jack Butland, aliye na miaka 26, ataomba uhamisho kujilazimisha kuwa katika mipango ya meneja wa England, Gareth Southgate kwa ajili ya mashindano ya Euro 2020. (Mail)

Timu ya Brazil Flamengo ilmejitoa katika uhamisho wa mshambuliaji Mario Balotelli baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuitisha mkataba wa thamani ya £4m. (Mail)

Haki miliki ya picha Reuters

Napoli imekubali kumsaini winga wa Mexico mwenye miaka 23 Hirving Lozano kutoka timu ya Uholanzi PSV Eindhoven. (Voetbal International)

Napoli imekataa ombi la thamani ya £82m kutoka kwa Manchester United kwa mchezaji wa miaka 28 raia wa Senegal Kalidou Koulibaly kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho England. (Corriere dello Sport, kupitia Calciomercato)

Winga wa Bournemouth Jordon Ibe anasakwa na mabingwa wa Uskotchi, Celtic. Timu ya Napoli Italia, tayari imemuulizia mchezaji huyo wa miaka 23. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United imewapiga marufuku wachezaji kusaini kumbukumbu au autograph kwa mashabiki katika kiingilio cha uwanja wa mazoezi kutokana na masuala ya usalama.(Telegraph)

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anasema alitaka kipa wa Liverpool Adrian, mwenye miaka 32, asalie katika klabu hiyo. (Mail)

Bora za siku ya Alhamisi:

Neymar alikuwa mazoezini mwenyewe siku ya Jumatano, ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapouzwa.(Esporte Interactivo, via Mundo Deportivo - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, anaweza bado kujiunga na PSG ikiwa hatakuwa sehemu ya ofa ya Neymar. (Goal)

Beki wa kati wa Manchester United Victor Lindelof, 25, anajiandaa kusaini mkataba mpya kwa ongezeko la mshahara mbali na pauni 75,000 alizokuwa akipata kwa wiki. (Aftonbladet - in Swedish)

Bayern Munich huenda wakafufua nia yao ya kumnasa winga wa Manchester City, Leroy Sane, ingawa mchezaji huyo, 23, ana jeraha la mguu, litakalo mfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba. (Bild - in German)

Mshambuliaji wa Marseille na Italia Mario Balotelli,29, anajiandaa kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Brescia baada ya kukataa ofa ya Flamengo ya Brazil. (Guardian)

Flamengo bado wana matumaini ya kubadili msimamo wa Balotelli, baada ya kukubali ombi lake la kumsajili kaka yake Enock kucheza katika moja kati ya timu zao nyingine (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya picha Reuters

Winga wa klabu ya Everton Alex Iwobi, 23, amesema aliondoka Arsenal katika siku ya mwisho ya usajili kuthibitisha kuwa yeye si mchezaji anayechipukia tena. (Mirror)

Tottenham itazungumza na Christian Eriksen, 27,tena kuhusu mkataba mpya kabla kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, tarehe 2 mwezi Septemba, baada ya Real Madrid na Juventus kuonesha nia ya kumnasa kiungo huyo.(Independent)

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, anaonekana kujiandaa kujiunga na timu ya Trabzonspor ya Uturuki kwa dili la pauni milioni 2.8 kwa kila msimu.(Goal)

Monaco imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwasajili wachezaji kiungo Blaise Matuidi,32, na beki wa kati Daniele Rugani,25, kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii