Kwanini mlindalango wa Liverpool Adrian ''atakosa'' mechi dhidi ya Southampton?

Shabiki alimuumiza Adrian wakati wachezaji wa Liverpool walipokusanyika pamoja kusherehekea ushindi wao Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shabiki alimuumiza Adrian wakati wachezaji wa Liverpool walipokusanyika pamoja kusherehekea ushindi wao

Mlindalango wa Liverpool Adrian huenda akakosa mechi ya Premia Ligi dhidi ya Southampton Jumamosi baada ya kugongana na mtu aliyevamia uwanja

Meneja Jurgen Klopp anasema Muhispania huyo aliumia wakati wa sherehe za baada ya mechi kufuatia ushindi wa Liverpool dhidi ya Chelsea katika mchezo wa kuwania Super Cup siku ya Jumatano.

" Shabiki aliruka juu ya kitu fulani , akateleza halafu akamgonga kwenye fundo la mguu . Kimevimba lakini lazima tuangalie ,"amesema Klopp baada ya Adrian kuinusuru timu hiyo na mkwaju wa penati wa Tammy Abraham ulioinusuru timu. Tukio hilo lilitokea wakati wachezaji wa Liverpool walipokusanyika pamoja kusherehekea ushindi wao.

Shabiki wao , aliyetaka kujiunga kikosi, alikimbia walipokuwa, akateleza ndipo aliposhikwa na steward, na kugongana wachezaji kadhaa.

Klopp amesema : "Inashangaza. Tunawapenda mashabiki wetu, bila shaka, lakini tungeacha kufanya hivyo. tulicheza dhdi ya City na mtu akakimbilia uwanjani.

Image caption Adrian akibebwa juu juu baada ya ushindi wa Liverpool

"Tuilipokuwa Norwich, kulikuwa tena na shabiki mwingine aliyefanya hivyo pia.

"Haifurahisi kabisa. Kama msichana aliyekimbilia uwanjani wakati wa Ligi ya Championi alitengeneza pesa. Tutafanya nini ?"

Klopp anasema chaguo la tatu la mlindalango wa Liverpool Andy Lonergan, mwenye umri wa miaka 35, ambaye hakutumiwa kama mchezaji wa ziada katika mechi na Istanbul iliyoisha kwa 2-2 baada ya muda wa ziada ,yuko "tayari" kukaimu ikiwa Adrian mwenye umri wa miaka 32-atashindwa kuingia uwanjani.

Chaguo la kwanza la Liverpool -Alisson ana jeraha la mguu.

Image caption Meneja wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp

"Andy Lonergan anafanya mazoezi na (Caoimhin) Kelleherna tunao ikiwa tutataka kufanya uamuzi ," amesema Klopp kuhusu wachezaji hao mbadala.

"Ilikuwa ni wiki moja kabla ya Adrian kufanya mazoezi nasi , Lonergan amefany amazoezi na sisi . Tutaona. Kelleher anauwezekano mkubwa wa kucheza nasi lakini si kwa 100% bado."

Wakati huo huo , Liverpool wamesitisha mazungumzo ya uhamisho na upande wa Ligi ya Serie A - Roma kuhusiana na mlinzi wa timu hiyo Dejan Lovren.

Hii inakuja baada ya Romakuonyesha utashi wa kutengeneza mkataba wa euro milioni 20 kwa ajili ya Mcroasia anayecheza safu ya kati-nyuma lakini wakashindwa tu kutoa ombi rasmi.

Badala yake, inafahamika kuwa Roma wanametuma ujumbe kujaribu kumchukua Lovren kwa mkobo wa gharama ndogo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii