Tetesi za soka Ulaya Jumanne 20.08.2019: Neymar, Eriksen, Varane, Vorm, Mustafi, Ibe, Bravo

Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsaini Neymar, 27, kwa mkopo kutoka Paris St-Germain wiki hii kukiwa na fursa ya kuyafanya makubaliano hayo kuwa ya kudumu.. (ESPN)

Juventus imeanza mazungumzo na PSG katika harakati za kutaka kumsaini mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ufaransa kwa dau la £200m mwaka 2017. (AS)

Barcelona haijajiandaa kuachilia ndoto yake ya kumrudisha Nou Camp mchezaji huyo wa Brazil . (Marca)

PSG iko tayari kuipatia Real Madrid mshambuliaji wake Neymar iwapo klabu hiyo itawapatia beki wake wa kati Raphael Varane, 26, na winga mwenye umri wa miaka 19 Vinicius Jr. (Telefoot, via Sun)

Christian Ericsen

Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, ana hamu ya kujiunga na klabu kubwa Ulaya ikiwemo , Barcelona, Real Madrid au Juventus. (ESPN)

Liverpool huenda ikamsaini kipa wa Tottenham Michel Vorm, 35, ambaye amesalia bila klabu baada ya kuachiliwa msimu uliopita. (Caught Offside)

Arsenal imejiandaa kumwachilia beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, kuelekea Roma kwa mkopo wa msimu huu kwa lengo la kumsajili kwa mkataba wa kudumu wa dau la £23m . (Forza Roma, via Sun)

Mustafi Haki miliki ya picha Getty Images

Celtic imejiandaa kumchukua mchezaji wa Bournemouth's Jordan Ibe, 23, kabla ya dirisha la uhamisho la Uskochi kufungwa tarehe 2 September. (Express)

Manchester City, Arsenal na Tottenham wote walituma maskauti kumchunguza kinda wa klabu ya Rennes Eduardo Camavinga katika mechi ya ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Paris St-Germain. (mail)

Kipa wa Chile Claudio Bravo, 36, anatarajiwa kuondoka Manchester City mwisho wa msimu huu katika uhamisho wa bila malipo.. (Sun)

Claudio Bravo

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente, 34, anakaribia kujiunga na Lazio kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kuachiliwa na Spurs msimu huu. (Corriere dello Sport)

Monaco inamlenga kiungo wa kati asiyetakikana Chelsea Tiemoue Bakayoko, 25, kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho Ulaya . (L'Equipe, via Talksport)

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kwamba kiungo wa kati wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, hataondoka Manchester United msimu huu . (Sky Sports)

Pogba

Juventus inaandaa dau la £9m kumnunua beki wa kushoto wa Barcelona Juan Miranda, 19. (Mundo Deportivo)

Beki wa Lazio raia wa Brazil Wallace, 24, ambaye alikua amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Wolves wakati wa dirisha la uhamisho sasa anatarajiwa kuelekea Valencia au Monaco.(Birmingham Mail)

West Ham wanamtaka Manuel Lanzini kutia saini kandarasi ya muda mrefu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Argentina akiwa amesalia na miezi 12 katika kandarasi yake . (Sky Sports)

Manuel lanzini

Beki wa Manchester United raia wa Argentina Marcos Rojo, 29, alinyimwa uhamisho wa Everton wakati wa siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kwa kuwa wamiliki wa Man United the Glazers wanaowaona the Toffees kama wapinzani wao wa moja kwa moja . (Express)

TETESI ZA JUMATATU

Paulo Dubala

Mabingwa wa Ufaransa PSG wamefanya mazungumzo na Juventus kuhusu uhamisho wa dau la £73m kumsajili mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 Paulo Dybala. (Mail)

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho amewasili nchini Ujerumani ili kukamilisha mkopo wake wa msimu huu kwa mabingwa wa ujerumani Bayern Munich. (Sun)

Paris St-Germain wamemtaka beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 26, pamoja na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 19, katika mpango wa kubadilishana wachezaji iwapo wanamuitaji mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Neymar. (Telefoot - in French)

Haki miliki ya picha Getty Images

Barcelona inatumai kumrudisha Neymar Nou Camp , lakini kukiwa na kifungu cha kumnunua.. (Sport - in Spanish)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 34, anakaribia kujiunga na klabu ya Itali Lazio. Inter Milan, Fiorentina na Napoli pia zina hamu ya kumsaini raia huyo wa Uhispania , ambaye kwa sasa hana klabu. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Inter Milan wanataka kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Chile Alexis Sanchez, 30, na pia wana hamu na mshambuliaji Llorente na kiungo wa kati wa Barcelona na raia wa Chile Arturo Vidal, 32. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images

Ajenti wa Sanchez yuko nchini Uingereza kuzungumzia mkopo wake kuelekea Inter Milan. (Sky Italy, via Sky Sports)

Sanchez alikua akifanya mazoezi na United siku ya Jumapili alfajiri.. (The Sun)

Inter Milan inajaribu kuafikia makubaliano ya kumnunua Sanchez lakini United imelazimika kumtoa kwa mkopo ili kutolipa mshahara wake wa £500,000 kwa wiki. (Mirror)

Manchester United wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi beki Eric Bailey mchezaji mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ivory Coast . (Sun)

Paris St-Germain na Bayern Munich huenda zikawasilisha ombi kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can, 25, baada ya kuambiwa na mkufunzi wake Maurizio Sarri anahitajiki Juventus. (Tuttosport, via Mail)

Paris St-Germain na Monaco zinafikiria kumpatia ofa kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 25, kwa kuwa muda wake Chelsea unaonekana kwamba umekwisha.. (Daily Express)

Celtic imeipatia ofa Bordeaux kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Olivier Ntcham . (20 Minutes via Daily Record)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce yuko tayari kumrudisha uwanjani mshambuliaji wa England Dwight Gayle, 28, haraka iwezekanavyo. (Newcastle Chronicle)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii