Morocco kutumia All Africa Games kutafuta nafasi ya kuandaa mashindano makubwa duniani

Sherehe ya ufunguzi wa michezo ya All Africa Gamaes

Mashindano ya All Africa Games yanaaendelea nchini Morocco katika kile kinachotazamwa na wengi kama mazoezi kwa azma ya nchi hiyo kuandaa michezo ya Olimpiki barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Zaidi ya wanamichezo 6000 kutoka mataifa yote 54 wamekusanyika kushindana kwa aina 30 ya michezo itakayojumuisha fani 17 zitakazotumika kama mashindano ya kufuzu Olimpiki.

Fainali ya voliboli ya ufukweni yataandaliwa baadae leo amabopo washindi watajikatia tiketi ya kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayoandaliwa mjini Tokyo Japan.

Nawal El Moutawakel alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria sherhe ya ufunguzi .

Alikuwa mwanariadha wa kwanza mwanamke na Muislamu kutoka Afrika kushinda medani ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za mita 400 kuruka fuhunzi katika mashsindano ya Olimpiki ya mwaka 1984

Nawal ambaye sasa ni afisa wa ngazi ya juu katika kamati ya Kimataifa ya Olimpiki aliisimulia BBC safari yake kutoka uwanjani hadi kufikia ufanisi wa kupanga michezo katika ngazi ya Kimataifa.

''Kama raia wa Morocco najivunia sana kumwakilisha rais wangu Thomas Barke katika ufunguzi wa michezo hii. Watu watarajia mashindano mazuri kwa sababu fani zote zariadha zimezingatiwa'' alisema akizungumzia sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo.

Image caption Nawal El Moutawakel

Kuhusu hatua ya Morocco kuandaa mashindano hayo Nawal alisema ni heshima kubwa kwa taifa hilo kuandaa makala ya 12 ya michezo ya Afrika ambayo inaleta pamoja jumla ya mataifa 54 na wadau wa kitamaifa wa michezo na mabalozi waliokusanyika pamoja kusherehekea michezo,vijana na talanta ya hali juu. Hii ni fursa nzuri kwa Morroco kuonesha imerejea tena ulingoni katika michezo,'' alisema.

Kuhusu uwezo wa Morocco kuandaa mashindano ya ya Olimpiki Bi Nawal ana sema Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki inatumia mashindano ya All Africa Games kutathmini uwezo wa taifa hilo.

''Morocco imetumia juhudi kubwa kujiweka katika ramani ya kimataifa na iliwahi hata kutoa ombi la kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia Mwaka 2016. Japo haikufuzu imekuwa ikijiandaa kwa na ishara zote ziko wazi kuwa ina uwezo wa kuandaa mashindano makubwa siku zijazo'' aliangeza Bi Nawal.

Pia anasema ametumia zaidi ya miaka 25 ya maika yake kujiimarisha katika nyanja zingine baada ya kushtaafu michezo kwasababu hakutaka kujulikana kwa ufanisi wake wa sekunde 54 uwanjani aliposhinda mbio za mita 400 kuruka vionzi mwaka 1984.

''Ushindi huo ulinifungulia milango ya uongozi katika fani mbali mbali ya maendeleo'' aliiambia BBC.

Bi Nawal aliongeza kuwa kilichompatia uwezo wa kufikia ufanisi aliopata hata baada ya ushindi wake wa Olimpiki miaka 25 iliyopita ni azma ya kujifunza kutoka watangulizi wake.

Mwanariadha wa zamani wa Kenya Tegla Loroupe, amabye ni gwiji wa mbio za masafa marefu, na sasa ni afisa katika kamati ya Olimpiki ya bara Afrika amesema mashindano ya All Africa games ni kigezo cha wanariadha kujipima uwezo wao wa kushiriki mashindano ya Olimpiki.

Image caption Kikosi cha wanariadha wa Ethiopia

Kenya yafuzu kwa fainali ya voliboli ya ufukweni

Kenya imejihakikishia medali yake ya kwanza kwa kufuzu kwa fainali ya mashindano ya voliboli ya ufukweni kwenye michezo ya mataifa ya Afrika nchini Morocco.

Kenya, ikiwakilishwa na Naomi Too na Gaudencia Makokha, imeshinda bingwa mtetezi Msumbiji seti 2-0 na sasa itakutana na Misri mechi ya fainali leo hii.

Kenya ilishinda seti ya kwanza 21-18 na ya pili 21-15. Katika mechi ya robo fainali, Kenya iliifunga Nigeria seti 2-1 na Msumbiji ikaiondoa Morocco seti 2-1 pia.

Misri ilishinda Mauritius seti 2-0 katika mechi ya nusu fainali. Kenya tayari imezoa medali yake ya kwanza kwani hata wakishindwa na Misri watapata medali ya fedha.

Ni taifa la kwanza la Afrika Mashariki kupata medali kwenye michezo ya mataifa ya Afrika.

Morocco haijashiriki katika mashindano ya mataifa yote ya Afrika kwa karibu miaka 30 kutokana na msimamo wa Muungano wa Afrika kuhusu eneo la Sahara Magharibi. Mara ya mwisho Morocco michezo hiyo ilikuwa mwaka 1978 mjini Algiers.

Hata hivyo hatua ya nchi hiyo kujiunga tena na AU mwaka 2017 iliifanya Morocco kuwa sehemu kubwa ya shirika hilo la Kiafrika na kukuchukua nyadhifa kadhaa muhimu katika muungano huo ikiwa ni pamoja na Baraza la usalama.

Mashindano ya All Africa Games huandaliwa kila baada ya miaka minne.

Mashindano ya mwaka 2015 yalifanyika Congo Brazzaville.

Image caption Nigeria ina kikosi kikubwa cha wanamichezo(427) wanaoshiriki mashindano hayo

Kando na kuandaa mashindano ya Olimpiki, Morocco pia inapania kuanadaa mashindano ya kimataifa ya soka ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia.

Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika imesema itawasilisha rasmi ombi la kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2030 wakati FIFA itakapo tangaza mchakato wa zabuni.

Pia kuna uwezekano wa Morocco kuwasilisha zabuni kwa ushirikiano na mataifa mengine ya kiarabiu kama vile, Algeria na Tunisia, huku FIFA ikivutiwa zaidi na ombi la kuandaa pamoja mashindano hayo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii