Romelu Lukaku: Matamshi ya tumbili ni 'heshima' na sio 'ubaguzi' wasema mashabiki wa Inter Milan

Romelu Lukaku Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lukaku alikuwa akishiriki katika mechi ya pili ya Inter Milan baada ya kujiunga kutoka Manchester United katika dirisha la uhamisho

Kundi moja la mashabiki wa klabu ya Inter Milan limedai kwamba mashabiki wa klabu ya Cagliari walikuwa wakimpatia heshima Romelu Lukaku wakati walipoimba nyimbo za ubaguzi dhidi yake siku ya Jumapili.

Lukaku ambaye alihamia Inter Milan kutoka Manchester United msimu huu , alikumbwa na matamshi ya kibaguzi alipofunga goli la ushindi wa 2-1 dhidi ya klabu hiyo.

Taarifa kutoka kundi la mashabiki wa Inter Milan ilisema kwamba mashambiki wa Itali sio wabaguzi na kwamba udhalilishaji huo ni miongoni mwa urafiki wa mchezo huo.

Iliongezea: Tunaomba msamaha kwamba kile kilichotokea Cagliari kilikuwa ubaguzi.

Barua hiyo ya wazi kwa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji iliochapishwa katika ukurasa wa facebook ilisema: lazima uelewe kwamba Itali sio kama mataifa ya kaskazini mwa Ulaya ambapo Ubaguzi ni tatizo kuu.

Tunaelewa kwamba ulidhania ni ubaguzi kwako lakini sio hivyo.

''Nchini Itali tunatumia njia ili kuzisaidia timu zetu na kuwafanya wapinzani wetu kuwa na wasiwasi sio kwa ubaguzi lakini kuwaharibia''.

''Tafadhali chukulia tabia hii ya mashabiki wa Itali kama heshima kwa kuwa wanaogopa idadi ya magoli utakayowafunga na sio kwamba ni wabaguzi''.

Lukaku ambaye alisema kandanda inarudi nyuma kutokana na matamshi hayo ya kibaguzi, alisimama na kuwatazama mashabiki nyuma ya goli ambapo matamshi hayo ya kibaguzi yalikuwa yakitolewa baada ya kufunga goli la ushindi.

Beki wa Inter Milan Skriniar ambaye alionekana akiweka kidole chake katika mdomo akimuunga mkono mchezaji mwenza alishutumu vitendo vya mashabiki katika mahojiano ya baada ya mechi hiyo.

Ubaguzi huo dhidi ya Lukaku ulikuwa kisa cha hivi karibuni ambapo mchezaji mweusi alibaguliwa uwanjani na mashabiki wa Cagliar.

Katika taarifa , Cagliari ilisema kwamba inawatafuta mashabiki waliotekeleza kitendo hicho kwa lengo ka kuwapiga marufuku.

Haki miliki ya picha Alamy

Msimu uliopita mshambuliaji wa Everton Moise Kean alikabiliwa na matamshi kama hayo ya kibaguzi alipocheza dhidi ya Cagliari akiichezea Juventus

Ligi ya Seria A iliamua kwamba haitawachukulia hatua ,mashabiki wa Cagliari licha ya kwamba matamshi waliotoa yalikuwa ya kibaguzi.

Mwaka uliopita mashabiki wa Cagliari walishutumiwa baada ya kumtupia maneno ya kiubaguzi mchezaji wa Juventus Blaise Matuidi - Lakini wakuu wa ligi ya Itali hawakuwachukulia hatua yoyote mashabiki hao.

Mwaka 2017 kiungo wa kati wa klabu ya Pascara Sulley Muntari aliondoka uwanjani baada ya kubaguliwa na mashabiki wa klabu ya Cagliari hatua iliomfanya kupigwa marufuku kwa kitendo chake hicho.

Inafuatia kisa ambacho Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba na Marcus Rashfrod pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham walidhalilishwa katika mitando ya kijamii.

Waliokuwa wachezaji wenza wa Lukaku, Pogba na Rashford wote walilengwa katika mitandao ya kijamii baada ya kukosa penalti msimu huu.

Beki wa Chelsea Kurt Zuma pia alidhalilishwa kirangi baada ya kujifunga dhidi ya Sheffield United huku wachezaji wenza Abraham na mchezaji wa Reading Yakou Meite wote wakipokea ujumbe wa kibaguzi mitandaoni baada ya kukosa penalti mwezi uliopita.

Taarifa ya Cagliari

Klabu ya Cagliari Calcio ilisema katika taarifa yake kwamba imepinga kile kilichotokea siku ya Jumapili usiku katika uwanja wa Sardegna katika mechi dhidi ya Intermilan.

Klabu hiyo imesema kwamba itawatafuta na kuwapiga marufuku mashabiki wake waliohusika katika kitendo hicho kila siku.

Ba awataka wachezaji weusi kuondoka Serie A

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Newcastle Demba Ba, akitoa maoni yake kuhusu taarifa hiyo ya mashabiki wa Inter , akisema kwamba wachezaji weusi wanafaa kuondoka katika ligi hiyo ya Itali.

'Na hii ndio sababu {Taarifa kutoka kwa mashabiki hao} niliamua nisiende kucheza katika ligi hiyo''.

''Najua kwamba kuondoka kwa wachezaji weusi hakutawazuia kuendelea na ujinga wao na chuki lakini ni bora kwamba hakutadhuru rangi nyengine''.

Mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster , aliyedai alinyanyaswa kibaguzi wakati wa wa kombe la Uefa 2017 alituma ujumbe wa twitter siku ya Jumanne akisema: kila siku kunatokea kisa kipya, inakera kuona chengine cha mtu akibaguliwa

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii