Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 05.09.2019: Moura, Can, Mandzukic, Willian, Bailly

Lucas Moura Haki miliki ya picha Getty Images

Barcelona ingelimsaini mshambuliaji wa Tottenham Lucas Moura, 27, msimu huu lakini ilishindwa kufikia bei yake ya £45m. (Mundo Deportivo)

Juventus itawauza mshambuliaji Mario Mandzukic, 33, na kiungo wa kati Emre Can, 25, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal)

Atletico Madrid bado inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, na wako tayari kuweka dau kubwa mwezi Januari. (AS - Spanish)

Juventus pia inawfuatilia wachezaji watatu wa Manchester United miongoni mwao kipa David de Gea, 28, Eric Bailly, 25, na Nemanja Matic, 31, kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufunguliwa msimu ujao. (Daily Mirror via Gazzetta Dello Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eric Bailly

Beki wa Liverpool Dejan Lovren, 30, amesema anatathmini uwezekano wa kuhamia AC Milan na Roma msimu huu wa joto. (Sportske Novosti via Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, alilia machozi alipoambiwa kuwa hawezi kujiunga tena na klabu yake ya zamani Barcelona. (El Chiringuito radio via Esporte - Portuguese)

Mshambulizi wa Barcelona Luis Suarez, 32, amesema Neymar alikua amefanya kila awezalo kuondoka Paris St-Germain. (Fox Sports Radio via Barca Blaugranes)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambulizi wa Barcelona, Luis Suarez

Callum Hudson-Odoi, 18, amabye ni mshambuliaji wa Chelsea yuko tayari kujitolea kwa mustakabali wake wa muda mrefu na klabu hiyo. (Football.london)

Winga wa zamani wa Liverpool Ryan Kent, 22, anasema wachezaji wawili wa zamani wa klabu hiyo Steven Gerrard na Michael Beale, ambaye sasa ni msimamizi wa Rangers, walikua kiungo muhimu katika mchakato wa wake kuhamia klabu ya Glasgow. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mchezaji wa kiungo cha kati anayelengwa na Manchester United Bruno Fernandes, 24, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Sporting Lisbon. (Record via Manchester Evening News)

Nottingham Forest walimtaka kiungo wa zamani wa Tottenham Marcus Edwards, 20, msimu huu. (The Athletic)

Aston Villa imewasilisha dau la £9m la kumnunua mshambulizi wa Celta Vigo Pione Sisto, 24, msimu wa joto. (Faro de Vigo - Spain)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption United Paul Pogba (Kushoto)

Ndugu yake kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amesisitiza kuwa mchezaji huyo wa miaka 26 atatumia muda wake mwingi Old Trafford kujiimarisha bada ya jaribio lake la kuhama klabu hiyo msimu huu kugonga mwamba. (El Chiringuito via Metro)

Mshambuliziwa Borussia Dortmund Marco Reus, 30,anasema yuko tayari kufanya kila awezalo katika uwezo wake kuhakikisha kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 20, anaungana nae katika klabu hiyo. (Sport1 via Lancashire Live)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa Chelsea, Cesar Azpilicueta

Vilabu vya Real Sociedad na Athletic Bilbao nchini Uhispani vinajiandaa kumnyakua beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 30, ikiwa mchezaji huyo atapatikana. (Express)

Tetesi Bora Jumatano

Manchester United ina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, mwezi Januari mwakani kwa bei iliopunguzwa kandarasi yake ikiingia mwaka wa mwisho katika klabu hiyo .(Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Eriksen

United itamenyana na Inter Milan kupata saini ya Eriksen. (Express)

Jaribio la Bayern Munich kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu wa juto limetibuka baada ya kushindwa kufikia masharti ya mshahara wa mchezaji huyo. (Manchester Evening News)

Mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling, ambaye awali alijiunga na Roma kwa mkopo huenda akasalia katika klabu hiyo ya Italia zidi ya msimu huu. (Manchester Evening News)

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa akidai kuwa amekataa ofa ya vilabu kadhaa vilivyotaka kumsajili. (mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling

Liverpool na Chelsea wanapania kumsajili mshambuliaji wa Wigan Athletic wa miaka 17- Muingereza Joe Gelhardt, ambaye ameshirikishwa mara tatu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Mirror)

Winga wa Chelsear Willian, 31, ananyatiwa na kocha wake wa zamani Maurizio Sarri ambaye sasa ni mkufunzi wa Juventus, wakati kandarasi ya nyota huyo Stamford Bridge ikiingia mwaka wa mwisho. (Express)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii