Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 04.10.2019: Ozil, Emery, Mandzukic, Wilson, Willian, Eriksen

Serge Gnabry
Image caption Serge Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski ametoa kauli ya kebehi kwa wapinzani wake wa zamani Tottenham kwa kusema kuwa Serge Gnabry inabidi awe mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal. Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii.

Kocha wa zamani wa England Fabio Capello amefichua kuwa alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa mkopo kipindi akiinoa timu ya Juventus. (Sky Sports Italia via Mail)

Mchezaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33, na Callum Wilson, 27, wa Bournemouth wapo katika rada za usajili wa klabu ya Manchester United ambao wanatafuta kwa nguvu zote mshambuliaji wa kusajili katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Sky Sports)

Kiungo nyota wa Norway Martin Odegaard, 20, anapanga kurejea Real Madrid japo klabu za Manchester United na Liverpool. Kiungo huyo kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Real Sociedad. (Goal)

Kiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen bado anaamini mipango yake ya kuhamia Real Madrid inaweza kufanikiwa, na wakala wake mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kwenda Uhispania kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madrid. (Star)

Image caption Christian Eriksen

Real Madrid walifikiria kumteaua Antonio Conte kuwa kocha wao mwaka jana, kabla ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea kurudi dimbani na klabu ya Inter Milan. (Fichajes.net, via Calciomercato)

Klabu ya soka ya LA Galaxy ya Marekani inaripotiwa kumnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Rangers ya Uskochi na raia wa Colombia Alfredo Morelos, 23. (Star)

Image caption Mesut Ozil

Kocha wa Arsenal Unai Emery amegoma kukanusha uwezekano wa kiungo Mesut Ozil kuihama klabu hiyo mwezi Januari. (Sun)

Kocha wa zamani wa Brighton Chris Hughton amekataa ofa ya kuinoa klabu inayosuasua ya daraja la kwanza, Stoke City. (Mirror)

Image caption Willian

Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anatumaini kuwa ataungana tenza na winga Willian katika klabu ya Juventus. Hata hivyo kocha wa Chelsea Frank Lampard amefichua kuwa mchezaji huyo raia wa Brazil yupo katika "mazungumzo" ya kuongeza mkataba. (Calciomercato, via Sun)

Tetesi bora za Alhamisi

Image caption N'Golo Kante

Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri ana matumaini ya kuungana tena na kiungo mkabaji N'Golo Kante, 28. Sarri ambaye kwa sasa anainoa Juventus yupo tayari kumnunua kiungo huyo raia wa Ufaransa kwa kitita cha takribani pauni milioni 70. (Mail)

Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kama sehemu ya kufufua kikosi cha Manchester United. (Manchester Evening News)

Image caption Ousmane Dembele

Manchester United pia wanaendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 22, ambapo wanaweza kumsajili kwa pauni milioni 80. (Mail)

Mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 24, anaamini wakati wa klabu yake kushinda michuano ya Champions League umekaribia, japo amewaasa wachezaji wenzake kusalia na subira.(Mirror)

Image caption Mauricio Pochettino

Wachezaji wa Tottenham wanahofu juu ya mustakabali wa wa kocha wao Mauricio Pochettino, na wanaamini raia huyo wa Argentina anatafuta njia ya kuondoka klabuni hapo. (Mail)

Mshambuliaji fundi wa zamani wa Spurs na Manchester United Dimitar Berbatov anaamini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy atafanya mazungumzo na Pochettino "wiki hii" ili "kupata majibu sahihi na njia muafaka ya kusonga mbele." (Star)

Mada zinazohusiana