Tetesi za soka Ulaya Jumanne 08.10.2019: Solskjaer, Countinho, Dembele, Pulisic, Martinelli

Ole Gunnar Solskjaer

Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anahofia kwamba hatma ya kazi yake itakuwa haijulikani iwapo timu yake itashindwa kwa mabao mengi ugenini Liverpool.(Mail)

Baadhi ya wachezaji wamepoteza matumaini na raia huyo wa Norway anaamini baadhi yao wamekataa kumsikiliza. (Sun)

Solskjaer anahitaji kitita cha £300m kutumia katika dirisha lijalo la uhamisho na kumnunua mshambuliaji kama vile mshambuliaji wa Tottenhama na England Harry Kane,26, kulingana na winga wa zamani Lee Sharpe. (Talksport)

Kane anafaa kuondoka Tottenham na badala yake kuhamia Manchester City, kulingana na beki wa zamani wa England Glen Johnson. (Betdaq, via Independent)

Liverpool huenda ikapokea kitita cha £4.5m kati ya kile cha £84m wanazodaiwa na Barcelona baada ya kumnunua kiungo Philippe Coutinho, 27, ambaye alihamia Nou Camp mwaka 2018. (Mirror)

Everton inafikiria kumnunua mchezaji anayelengwa na Manchester United Moussa Dembele katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa , mwenye umri wa miaka 23 anaweza kugharimu £40m kutoka Lyon. (Star)

Chelsea na mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 21, amekiri kukasirishwa kwake kwa kukosa muda wa kucheza zaidi tangu uhamisho wake wa £58m kutoka Borussia Dortmund. (Guardian)

Mshambulaji wa Arsenal Gabriel Martinelli, 18, anakabiliwa na chaguo katika hatma yake ya kimataifa kwa kuwa anahitajika na Itali pamoja na Brazil. Alizaliwa nchini Brazil lakini lakini babake ni raia wa Itali hivyobasi anaweza kuwakilisha timu zote mbili.. (Mirror)

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 30, amekiri kwamba angependelea kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Newcastle lakini akasema kwamba hakupatiwa fursa kubadili uhamisho wake wa mkopo wa msimu uliopita kuwa kandarasi ya kudumu na hivyobasi akaelekea katika klabu ya China ya Dalian Yifang. (Newcastle Chronicle)

Mkufunzi Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace italazimika kumsaini mshambuliaji mpya mwezi januari iwapo wanataka kumaliza katika orodha ya timu sita za kwanza katika jedwali na pia analenga kuwasajili mabeki wawili wapya wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Standard)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii