Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 12.10.2019: Eriksen, Haland, Aurier, Dier, Parkinson, Lacazette

Kungo wa kati wa Tottenham Christian Ericksen

Real Madrid itataka kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwezi Januari.(Marca)

Real Madrid pia wanaisaka saini ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, 19 raia wa Norway Erling Haaland, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United. (AS)

Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 26, amefichua kwamba alitaka kuondoka mjini London mwisho wa msimu uliopita na amekiri kwamba hajui hatma yake iko vipi katika klabu hiyo. (Football.London)

Aston Villa imehusishwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)

Kazi ya Unai Emery kama mkufunzi Arsenal huenda ipo hatarani iwapo kikosi chake kitashindwa kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu . (Times - subscription required)

Mchezaji wa zamani wa Uingereza na nahodha David Beckham anamlenga mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kama mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya kama ajenti . (Mail)

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Man United Mark Robins amesema kwamba ilikuwa rahisi kwake kukataa kuwa mkufunzi wa Sunderland na kuamua kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Coventry. (talksport)

Ajenti mmoja raia wa Urusi anadai kwamba aliiomba klabu ya Zenit St - Petersburg kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexander Lacazette ambaye alikuwa anagharimu £61m . (mirror)

Kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba ,26, anakaribia kupona jeraha tayari kucheza mechi dhidi ya Liverpool mnamo tarehe 20 mwezi Oktoba licha ya ripoti ya kuvunjika kidole. (sun)

Man United inaweza kutarajia ufadhili wa shati utaokagharimu £450m huku wakisaka kandarasi mpya.(ESPN)

Kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Matty Longstaff , aliyefunga bao la ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Man United mwezi huu , kwa sasa analipwa £850 kwa wiki na klabu hiyo. (sun)

Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Jaoa Moutinho 33 anatarajiwa kukubali kuweka kandarasi mpya katika uwanja wa Molineux. (Birmingham Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images

Wolves ina mpango wa kuimarika katikati ya safu ya ulinzi pamoja na safu ya katikati wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari (The Athletic, via Inside Futbol)

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amemwambia Aliyekuwa mshambuliaji wa Sunderland Kevin Phillips kwamba heri anemsajili yeye badala ya Francis Jeffers. (Mirror)

Kiungo wa zamani wa Man United Marouane Fellaini, 31 raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya China ya Shandong Luneng, anasema kwamba Jose Mourinho hakupewa muda wa kutosha katika uwanja wa Old Trafford. (Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii