Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 14.10.2019: Fernandes, Mandzukic, Rakitic, Mbappe, Eriksen, Rice

Barcelona wangependa kumchukua mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa ya Paris St-Germain Kylian Mbappe
Image caption Barcelona wangependa kumchukua mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa ya Paris St-Germain Kylian Mbappe

Tottenham wameanza upya kuelezea haja yao ya kumtaka mchezaji wa kimataifa wa safu ya kati wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 25, wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa tena mwezi Januari (A Bola , via Mail)

Manchester United watatakiwa kutumia pauni milioni £10m ikiwa wanataka kusaini mkataba na Mcroatia anayecheza safu ya mashambulizi Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, kutoka Juventus katika kipindi cha uhamisho mwezi Januari, lakini mchezaji huyo amefikia makubaliano ya mdomo na Red Devils. (Express)

Image caption Mario Mandzukic

Barcelona huenda wakawa na haja ya kumuuza kiungo wa kati Ivan Rakitic mwenye umri wa miaka 31 mwezi Januari, huku Manchester United wakiaminiwa kuanzisha mazungumzo kuhusu hatua ya kumnunua Mcroasia huyo . (Sport)

Barcelona wangependa kumchukua mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, ambaye sasa ana umri wa miaka 20, na mshambuliaji wa kati Tottenham Harry Kane,mwenye umri wa miaka 26, kuliko kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mbrazili Roberto Firmino. (Mundo Deportivo, via Liverpool Echo)

Mpango wa Real Madrid wa kumnunua kiungo wa kimataifa wa Tottenham Mdenmark Christian Eriksen,mwenye umri wa miaka 27, huenda ukategemea mafanikio ya timu hiyo na kama kuna majeruhi wa muda mrefu. (AS)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eriksen angependelea kujiunga na Real Madrid katika msimu ujao

Eriksen angependelea kujiunga na Real Madrid katika msimu ujao badala ya Januari kwasababu wakati huo anaweza kuomba kusaini mkataba wa marupurupu ya juu zaidi. (Express)

Kiungo wa safu ya kati wa timu ya kimataifa ya England Declan Rice, mwenye umri wa miaka 19,anasisitiza kuwa anafurahia kuwa katika kikosi cha West Ham, akizielezea ripoti zilizomuhusisha na kuhamia Manchester United kama "porojo tu hadi kitakapotokea kitu - na kwamba hakuna kilichotokea ". (mirror)

Image caption Meneja wa Ex-Rangers na Birmingham Alex McLeish

Bristol City wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah kwa mkopo ,mwenye umri wa miaka ambaye walijaribu kusaini nae mkataba msimu uliopita kabla ya mchexzaji huyo kuamua kujiunga na Leeds. (Sun)

Leeds wanaamini kuwa Nketia hataruhusiwa kuendelea kubaki katika klabu ,licha ya kipengele cha Januari cha kumrejesha kujumuishwa katika mkataba wake wa mkopo . (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bristol City wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah kwa mkopo

Meneja wa Ex-Rangers na Birmingham Alex McLeish atachukua muda kuchukua hatua nyingine ya kiuongozi baada ya kukataa ofa kutoka England na nje ya nchi tangu alipoacha wadhihfa wake kama meneja wa Scotland mapema mwaka huu. (The Scottish Herald)

Meneja wa zamani wa Manchester City Stuart Pearce anaamini kabisa kwamba winga wa kimataifa wa England Phil Foden, mwenye umri wa miaka 19, anapaswa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa mkopo mwezi Januari . (Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa zamani wa Manchester City Stuart Pearce anaamini kwamba winga wa kimataifa wa England Phil Foden, anapaswa kuondoka kwenye klabu hiyo

Arsenal wako makini kumuajiri mchezaji mwenye umri mdogo kabisa wa kwanza wa Scunthorpe Joey Dawson, mwenye umri wa miaka 16- nanayecheza safu ya kati ambaye ni mpwa wa Michael Dawson. (Sun)

Meneja wa Tottenham Harry Redknapp anaamini kuwa Mauricio Pochettino hatafukuzwa , akidai kuwa Muargentina huyo ana kikosi kizuri kama kile cha claiming the Argentine has Liverpool au Manchester City. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa kimataifa wa Kenya anayecheza katika safu ya kati ya timu ya Tottenham Victor Wanyama anahusishwa na taarifa za kureje katika Celtic

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya anayecheza katika safu ya kati ya timu ya Tottenham Victor Wanyama, mwenye umri wa miaka 28, anahusishwa na taarifa za kureje katika Celtic, anatumaini kuwa itakuwa ni timu yake ya kwanza kurejea baada ya nia yake ya kuhamia Bruges msimu uliopita kushindwa kutekelezwa. (Football.London)

Mshambuliaji wa zamani wa Nottingham Forest Pierre van Hooijdonk, mwenye umri wa miaka 49, anasema kuwa alimuita meneja Ron Atkinson "meneja wa baa "wakati wa tamko lake fupi katika City Ground. (Guardian)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii