Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 16.10.2019: Kante, Mandzukic, Giroud, Bale, Mourinho

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86 kwa Mcolombia James Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 anayecheza safu ya kati ili kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa N'Golo Kante. (El Desmarque, via Sport Witness.

Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, anasakwa na Manchester United lakini ameonywa kuwa atahitaji kushusha kiwango cha madai yake ya mshahara. (ESPN)

Unaweza pia kusoma:

Hata hivyo Manchester United wanahofu kuhusu ugumu wa kusaini mkataba mpya wowote na wachezaji wapya katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari . (Metro)

Image caption Real Madrid wanamsaka N'Golo Kante

Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake mweizi Januari wakati wa kipindi cha uhamisho wa wachezaji. (The Athletic, via Mirror)

Tottenham wameimarisha haja yao ya kumtaka Jose Mourinho huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu msimamo wa Manchester United wa kumtaka Mauricio Pochettino. (Daily Express)

Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud,mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwezi wa Januari ikiwa hatacheza tena. Inter Milan na timu ya Ligi kuu ya Canada Vancouver Whitecaps ni miongoni mwa timu zinazomtaka. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United wanamtaka Mario Mandzukic ashushe viwango vya mshahara ili wamuajiri

Mchezaji wa safu ya kati wa Croatia Luka Modric amemuomba mchezaji mwenzake katika kikosi cha Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 30, akimtaka abakie katika klabu baada ya mshambuliaji huyo wa kati wa Wales kukaribia kabisa kuhamia Bernabeu msimu uliopita. (Independent)

Kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, bado anaweza kurudi Liverpool - ikiwa Bayern Munich wataaamua kutosaini mkataba wa kudumu na yeye msimu ujao . Kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu hiyo ya Ujerumani kutoka Barcelona. (AS, via TeamTalk)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olivier Giroud anajiandaa kutoka Chelsea

Paul Ince, ambaye ni nahodha wa kwanza mweusi wa England, anasema angewaongoza wachezaji wenzake kuondoka nje ya uwanja kama angekuwa anacheza katika mchezo baina ya Bulgaria na England Jumatatu ambao ulitawaliwa na matusi ya ubaguzi wa rangi . (Times, subscription required)

Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa safu ya kati wa Inter Milan Gabriel Barbosa, mwenye umri wa miaka 23, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Flamengo nchini Brazil. (PassionInter, via TeamTalk)

Image caption Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kuwaacha kiungo wa kati Muingereza Angel Gomes, mwenye umri wa miaka 19, winga wa Uholanzi Tahith Chong, mwenye umri wa miaka 19, na kiungo wa kati Muingereza James Garner mwenye umri wa umri wa 18, waondoke kwa mkopo mwezi Januari. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 25, anadai kuwa hakujali mazungumzo ya uhamisho yanayomuhusisha na Barcelona katikia msimu waujao ,na mlinzi wakikosi cha Sweden . (goal.com)

Manchester United wanajiandaa kumuunga mkono meneja Ole Gunnar Solskjaer katika msimu wa uhamisho wa wachezaji ifikapo mwezi Januari lakini wanaonya kuwa hawatalipa malipo ya ziada kwa wachezaji eti tu kwasababu ya kunusuru msimu wao kimchezo . (ESPN)

Image caption Ole Gunnar Solskjaer

Kushindwa kwa Arsenal kufuzu kwa Championi Ligi katika michuano ya mwisho ya 2016-17 kuliwakosesha fursa ya kusani mkataba na mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, ambaye wakati huo alikuwa na Atletico Madrid. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28-alijiunga na Barcelona msimu huu. (Star

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii