Premier League: Je Arsenal, Chelsea, Spurs na Man Utd zinakabiliwa na matatizo gani?

Marcus Rashford, Christian Eriksen, Sokratis na Kepa Arrizabalaga wote wana malalamishi kutokana na sababu tofauti Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcus Rashford, Christian Eriksen, Sokratis na Kepa Arrizabalaga wote wana malalamishi kutokana na sababu tofauti

Klabu nne kati ya sita kubwa katika ligi ya Premia - Arsenal , Chelsea , Manchester United na Tottenham - zimeonyesha ishara za kudorora kufikia sasa msimu huu.

Huku klabu hizo nne zikichukua jumla ya pointi 49 katika mechi zake nane za kwanza - ikiwa ni pointi chache zaidi tangu kampeni ya kwanza ya ligi ya premia 1992 na chache zaidi katika misimu ya hivi karibuni tunaangazia matatizo wanayokumbana nayo.

Manchester United

Baada ya kujishindia pointi nane kutoka mechi zake nane za kwanza - ikiwa ndio idadi ndogo zaidi katika kipindi kama hiki tangu 1989 - Man United ni mwathiriwa mkuu aliyepoteza alama nyingi.

Akiwa na magoli tisa pekee kutoka katika mechi zake nane , ni wazi kuna tatizo.

Huku wakiwa na kikosi cha wachezaji wenye umri mdogo zaidi katika msimu wa ligi ya Uingereza, klabu hiyo ndio iliokuwa na mshambulio machache zaidi ikiwa katika nafasi ya tano , lakini ni ubora wa mshambulio yake ambao unaleta wasiwasi.

Kulingana na magoli yaliotarajiwa, ni klabu ya Newcastle pekee ambayo imekuwa na mahsambulizi mabaya kwa wastani ikilinganishwa na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer, kando na penalti.

Cha kufurahisha miongoni mwa mashabiki wa Man United ni kwamba huku washambuliaji wakishindwa kutengeza fursa za kufunga magoli , safu ya ulinzi imewakabili washambuliaji wa timu pinzani na hivyobasi kuwa mojawapo ya safu bora za ulinzi kufkia kipindi hiki cha msimu.

Baada ya kutumia £130m kuwanunua mabeki Harry Maguire na Aaorn Wan-Bissaka na kumuuza mshambuliaji Romelu Lukaku msimu uliopita hilo halionekani kuwa swala la kushangaza.

Tottenham: Hali yao ni ngumu

Kufikia siku kuu ya wapendwa nao au Valentine's Day, Tottenham ilikuwa katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza na pointi tano pekee nyuma ya viongozi Liverpool.

Lakini pointi 22 kutoka mechi 20 tangu wakati huo zimeweka doa katika uhusiano kati ya Mkufunzi , wachezaji na klabu hiyo huku kukiwa na mazungumzo kuhusu hatma ya wachezaji wa timu hiyo nao wengine wakitafuta kujiunga na klabu nyengine.

Tatizo kuu la Tottenham ni kwamba sio eneo moja la timu hiyo ambalo lina tatizo.

Mbali na wachezaji kushindwa kuvamia lango la wapinzani wao kama ilivyokuwa hapo awali , jedwali hapo chini linaonyesha kwamba safu ya ulinzi na ile ya mashambulizi kufikia sasa ziko katika hali mbaya zaidi katika misimu sita ambayo klabu hiyo imekuwa chini ya uongozi wa Mauricio Pochettino.

Msimu huu Nafasi ilioshika chini ya mkufunzi Pochettino (misimu sita)
Magoli yaliofungwa 4th= 5th
Magoli yaliotarajiwa kufungwa 16th 6th
Mashambulizi 9th 6th
Magoli yalioingia 12th= 6th
Idadi ya magoli yaliotarajiwa 15th 6th
Mashambulizi yaliofanywa 16th 6th

Huku ikiwa sio rahisi kubaini, hii huenda inatokana na ukweli kwamba mkufunzi na wachezaji wamekuwa pamoja kwa muda mrefu.

Wachezaji wanane bado wapo katika klabu hiyo tangu msimu wa kwanza wa Pochettino wa 2014-15 ikilinganishwa na misimu mitatu pekee katika klabu ya Manchester City, na miwili katika klabu ya liverpool - huku kati ya wakufunzi 32 katika ligi ya mabingwa msimu huu , ikiwa ni mkufunzi wa Atletico Madrid pekee Diego Simione ambaye ameifunza klabu hiyo kwa kipindi kirefu zaidi ya raia mwenzake wa Argentina.

Arsenal: Gunners imedhoofika

Huku klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi , itaonekana swala lisilo la kawaida tukisema kwamba klabu hiyo imekuwa katika matatizo msimu huu.

Lakini tofauti ya magoli ya +2 inaonyesha kwamba yote sio tambarare kama yanayoonekana, huku kukiwa hakuna timu iliopo katika hali yake iliopo juu ya jedwali ikiwa na takwimu za kiwango cha chini tangu klabu ya Phil Brown Hull City ilipokuwa na tofauti ya magoli sufuri 2008.

Baada ya kuruhusu mashambulio 10-12 kwa kila mechi katika kila msimu wa misimu 13 ya klabu hiyo chini ya ukufunzi wa Arsene Wenger, waliruhusu mashambulizi 13 katika kampeni yao ya kwanza chini ya mkufunzi Unai Emery msimu uliopita.

Msimu huu , hatahivyo Arsenal imeruhusu mashambulizi 17 kwa mechi huku ikiwa ni klabu iliopandishwa daraja ya Aston Villa na Norwich ambazo zimeshambuliwa zaidi ikilinganishwa na Arsenal msimu huu.

Cha kufurahisha pekee kwa Arsenal ni kwamba huku timu hiyo ikiwa chini ya shinikizo kali msimu huu, wameweza kuzuia upinzani kupata kutekeleza mashambulizi makali ugenini huku ikiwa ni klabu ya Burnley pekee ambayo imeruhusu fursa chache zisizo na ubora zaidi ya kikosi cha Mkufunzi Unai Emery kwa wastani.

Hatahivyo katika misimu mitano iliopita kabla ya msimu huu, ni klabu tatu pekee ambazo zimeruhusu mashambulio 17 ama zaidi kwa mechi- klabu ya Sean Dyche mara mbili na ile ya David Moyes ilioshushwa daraja msimu wa 2016-2017.

Chelsea: Kepa anaweza kujiimarisha?

Licha ya kuwa na kikosi kichanga zaidi katika ligi ya Premia msimu huu, kimepongezwa na wengi, pia kimeruhusu magoli yasio ya kawaida 14 katika mechi zake nane kufikia sasa, huku Norwich pekee Watford na Southampton zikiruhusu magoli zaidi ya klabu hiyo.

Ni mara ya pili katika uongozi wa Roman Abrahamovich ambapo klabu hiyo imeruhusu magoli mengi katika kipindi hiki cha msimu , baada ya klabu hiyo chini ya uongozi wa Jose Mourinho ambapo walifungwa magoli 17 katika mechi zake nane 2015.

Huku akiokoa asilimia 48 ya mashambulizo yote ya upinzani msimu huu, Kipa Kepa Arrizabalaga ana takwimu mbaya zaidi za uokoaji katika ligi ya Premia kufikia sasa na analaumiwa kuhusiana na matatizo ya safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Kati ya walinda lango 25 walioshiriki katika ligi ya Uingereza msimu huu , ni kipa wa Southampton pekee Angus Gunn ambaye ameruhusu magoli mengi zaidi ya kipa wa Chelsea.

Kipa Idadi ya magoli aliyofungwa Magoli aliyofungwa Magoli aliyozuia
21 Tim Krul 10.43 13 -2.57
22 Tom Heaton 9.37 12 -2.63
23 Ben Foster 15.35 18 -2.65
24 Kepa Arrizabalaga 8.9 12 -3.1
25 Angus Gunn 10.63 15 -4.37

Lawama hiyo hatahivyo haifai kuwekwa mbele yake pekee.

Licha ya Manchester City kuwa timu pekee inayokabiliwa na mashambulio machache kufikia sasa msimu huu, ni timu nne pekee ambazo zimeruhusu upinzani kutengeza fursa rahisi zaidi za kufunga magoli zaidi ya Chelsea , hivyobasi Frank Lampard atatumai kikosi chake kichanga kitaifanya kazi ya Arrizabalaga kuwa rahisi zaidi katika siku za usoni.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii