Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 19.10.2019: Sterling, Neymar, Can, Cook, Cavani, Cahill, Nketiah

Manchester City inataka kumpatia mshambuliaji wa England Raheem Sterling mkataba mpya - chini ya miezi 12 baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutia saini mkataba mpya . (Metro)

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, anasema kwamba baadhi ya watu katika klabu hiyo hawamtaki mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kurudi. (Metro 95.1 via Sun)

Manchester United wanafikiria kumsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Ujerumani alijiunga na Juventus 2018. (Sky Sports)

Mchezaji bora duniani Lionel Messi

United pia wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 22, mbali na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (ESPN)

Liverpool na Chelsea zinamtaka kiungo wa kati wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 22 Lewis Cook. (Mail)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya David Beckham ya Inter Miami . (L'Equipe via Calciomercato - in Italian)

James Madisson wa Liecester

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anaamini amefanywa kisingizio katika klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 anasema kwamba atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa kandarasi yake 2021.. (Times via The Athletic - subscription required)

Newcastle imeanza mazungumzo na ndugu wawili Sean Longstaff, 21, na nduguye Matty, 19, katika harakati za kukubaliana mkataba ili kuwaweka wawili hao katika klabu hiyo licha ya hamu kutoka kwa Man United . (Express)

Beki wa Crystal Palace na England Gary Cahill, 33, amesema kwamba kustaafu sio lengo lake baada ya kutochezeshwa akiwa katika klabu ya Chelsea msimu uliopita. (Times - subscription required)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil

Mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Jurgen Klinsmann anatarajiwa kurudi katika ukufunzi wakati huu akiwa kocha wa timu ya taifa ya Ecuador. (Sun)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis anasema kwamba klabu hiyo huenda ikalazimika kumuuza kiungo wa kati Kalidou Koulibaly. Manchester United ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 28. (Talksport)

Manchester United iliwasilisha ombi la kumsajili beki wa Uturuki na Juventus mwenye umri wa miaka 21 Merih Demiral kabla ya kumsaini beki wa kati mwenye umri wa miaka 26 Harry Maguire. (Sky Italia via Sporx - in Turkish)

Khalidou Koulibaly Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa Leicester City na Nigeria Kelechi Iheanacho, 23, huenda analengwa na klabu ya Besiktas. (Calciomercato - in Italian)

Mshambuliaji wa klabu ya Al-Sadd na Algeria Baghdad Bounedjah, 27, anachunguzwa na klabu ya Leeds , Lille na Marseille. (Le Buteur - in French)

Mkufunzi wa Leeds Marcelo Bielsa anasema kwamba angependa sana mshambuliaji wa Arsenal aliyepo kwa mkopo katika klabu hiyo Eddie Nketiah, 20, kufanikiwa katika klabu hiyo ya Elland .. (Yorkshire Evening Post)

Eddie Nketia

Beki wa Everton Lewis Gibson anataka kujiunga tena na Newcastle. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa shule ya mafunzo ya soka katika klabu hiyo ya Magpies. (Football Insider)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, AC Milan, Inter Milan, Juventus na Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic, 38, ametoa ishara kwamba atstaafu kuichezea klabu ya LA Galaxy baada ya mechi yake wikendi hii (Sun)

TETESI ZA SOKA IJUMAA

Nemanja Matic anatafutwa na Inter Mila
Image caption Nemanja Matic anatafutwa na Inter Mila

Kiungo wa kati Manchester United na Serbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, anatafutwa na Inter Milan. (Sun)

Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, ameacha azma yake ya kuhamia Manchester United mwezi Januari kwasababu Wacroasia hawataki ahamie Manchester. (Mail)

Unaweza pia kusoma:

Image caption Ivan Rakitic,

La Liga imependekeza kwa shirikisho la soka la Uhispania kwamba shindano la El Clasico lililiyopangwa tarehe 26 Oktoba Barcelona lifanyike badala yake tarehe 7 Disemba . Tayari shirikisho hilo la mpira wa miguu limeomba kubadilisha gemu hiyo ifanyike Madrid kutokana na hofu ya ghasia za kiraia.(AS)

Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland analengwa na Manchester City. Kijana huyo Mnorway mwenye umri wa miaka 19 ni mtoto wa kiungo wa kati wa Manchester City Alf-Inge Haaland. (Sun)

Image caption Erling Haaland analengwa na Manchester City

Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya klabu ya Lyon Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England , huku akiripotiwa kusakwa na Everton na Manchester United. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23- aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Ufaransa ya walio chini ya umri wa miaka -21 awali alichezea klabu ya Fulham. (Football Insider)

Image caption Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England

Manchester United walimtaka na kumfuatilia mchezaji wa Juventus raia wa poland na mlindalango wa zamani wa Arsenal goalkeeper Wojciech Szczesny,mwenye umri wa miaka 29, wakati wa msimu ujao wa soka kabla David de Gea kusaini mkataba mpya katika Old Trafford mwezi uliopita. (Goal)

Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 22 kutoka AC Milan mwezi Januari . (La Gazzetta dello Sport via Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie

Tottenham na Manchester United ni miongoni mwa klabu kadhaa zilizowasiliana na Borussia Monchengladbach kuhusiana na namna wanavyoweza kumpata Mswiss anayecheza safu ya kati Denis Zakaria ambaye sasa ana umri wa miaka 22. (Bild - in German)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, "si mzuri vya kutosha " kwa Bayern Munich, anasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Lothar Matthaus. (Sport 1, via Standard)

Tottenham watalenga kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Madrid Muhispania Isco,mwenye umri wa miaka 27, kama wataamua kumuuza Eriksen ifikapo mwezi Januari (El Desmarque - in Spanish)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Lallana

Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, mwishoni mwa msimu ikiwa atbakia kuwa mchezaji wa ziada. (Football Insider)

Mlindalango wa Liverpool Mhispania Adrian, mwenye umri wa miaka 32, anasema the Reds walimkanyaga mara mbili na kumuumiza mlindalango wa Brazil Alisson Becker,mwenye umri wa miaka 27. (Telegraph)

Watfordwamekataa ombi kutoka kwa Fluminense la kuendelea kubaki na Joao Pedro nchini Brazil hadi Juni -2020. Hornets wamekubali kusiani mkataba na kijana huyo mchanga mwenye umri wa miaka 18 tu anayecheza safu ya mashambulizi Januari 1 . (Watford Observer)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wilfried Zaha

Winga wa Crystal Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, hutoa 10% ya mshahara wake kama msaada katika nchini Ivory Coast ambako ndio asili yake , ikiwa ni ni pamoja na kusaidia kituo cha yatima kinachoendeshwa na dada yake. (Mirror)

Liverpool ina matumaini ya kuipiku Chelsea kwa kusiani mkataba na mchezaji wa kimataifa wa vijana wadogo ya England kutoka Exeter anayecheza safu ya kati Ben Chrisene ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii