Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 20.10.2019: Sterling, Eriksen, Solskjaer, Koulibaly, Ceballos, McGinn, Matic

Raheem Sterling Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling

Manchester City inajiandaa kumlipa Raheem Sterling kitita cha £450,000-kwa wiki ili kukatiza azma ya Real Madrid ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza wa miaka 24. (Star)

Paris St-Germain itamenyana na Real Madrid kujaribu kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mail on Sunday)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anatafakari hatma yake ya baadae katika klabu hiyo ikihisi kuwa uwepo wake utaathiri hali ya mambo katika uwanja wa Old Trafford. (Metro)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alionekana akizungumza na Solskjaer katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wakatibwa mazoezi kuelekea mechi yao dhidi yao na Liverpool leo Jumapili. (Manchester Evening News)

Mwenyekiti wa Napoli Aurelio De Laurentiis amekiri kuwa "wakati utawadia" ambapo klabu hiyo italazimika kumuuza mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa klabu hiyo Kalidou Koulibaly,28, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United. (Sky Sports Italia, via Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Koulibaly(wa kati) ameiwakilisha Napoli mara 149 tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2014

Tottenham inamlenga beki wa West Brom Nathan Ferguson, huku Crystal Palace pia ikimnyatia mchezaji huyo wa miaka 19. (Sun on Sunday)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, amefanya mazungumzo na rais wa Real Madrid Florentino Perez kuhusu uwezekano wa kubadilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Arsenal kuwa uhamisho wa kudumu. (El Desmarque, via Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos

Meneja wa Aston Villa Dean Smith amesema klabu hiyo haina mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa John McGinn, 25. (Sunday Express)

Vilabu vya Manchester City na Barcelona vinapania kumnunua mchezaji wa safu ya kati waklabu ya Anderlecht Albert Sambi Lokonga, 19, ambaye amehusishwa na uhamisho kwenda Sevilla. (Marca)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kwa kuhofia kumpoteza mchezaji huyo wa miaka 31, ambaye analengwa na Inter Milan, kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Corriere dello Sport, via Sunday Express)

Tetesi Bora Jumamosi

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, anasema kwamba baadhi ya watu katika klabu hiyo hawamtaki mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kurudi. (Metro 95.1 via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi anadai baadhi ya watu katika klabu hiyo hawamtaka

Manchester United wanafikiria kumsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Ujerumani alijiunga na Juventus 2018. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anaamini amefanywa kisingizio katika klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 anasema kwamba atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa kandarasi yake 2021. (Times via The Athletic - subscription required)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil

United pia wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 22, mbali na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (ESPN)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii