David Luiz wa Arsenal azuru Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Beki wa Arsenal azuru Rwanda

Mchezaji nyota wa Arsenal David Luiz amefanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda iliyomwezezesha kutembelea maeneo maarufu ya kitalii nchini humo na kujione utamaduni wa watu wa taifa hilo.

Beki huyo wa Kimataifa wa Brazil pia alitaka kujifahamisha mawili matatu kuhusu nchi hiyo na jinsi inavyojipambanua kuwa mstari wa mbele katika masuala ya kuleta mabadiliko barani Afrika.