Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 21.10.2019: Sancho, Haaland, Werner, Meunier, Koeman

Jadon Sancho Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho

Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. (El Desmarque, via Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Express)

Manchester United inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. (Sun)

Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. (Chronicle)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Victor Osimhen

Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. (Telegraph)

Chelsea imemuongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Chelsea Frank Lampard

Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 28, anasema angelijiunga na Everton msimu huu lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hakuridhishwa na ofa aliotolewa na klabu hiyo. (Het Laatste Nieuws, via Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. (mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette

Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman angependelea kuwa msimamizi wa klabu ya Barcelona siku moja na anasema kuwa mkataba wake una kifungu cha sheria kinachomruhusu kuajiriwa na baada ya mashindano ya Ulaya mwaka 2020, amesema mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la kandanda la Uhuolanzi, Nico-Jan Hoogma.(Fox Sports, via Marca)

Tetesi Bora Jumapili

Manchester City inajiandaa kumlipa Raheem Sterling kitita cha £450,000-kwa wiki ili kukatiza azma ya Real Madrid ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza wa miaka 24. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raheem Sterling

Paris St-Germain itamenyana na Real Madrid kujaribu kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii