Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 24.10.2019: Fabinho, Upamecano, Fabian, Everton, Mandzukic, Slimani, Maddison

Fabinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fabinho

Unai Emery amedokeza kuwa alikaribia kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na raia wa Brazil Fabinho, 26, alipojiunga na Arsenal kama kocha mkuu mwaka jana. (Evening Standard)

Manchester City imeongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 23, na pia ilituma wataalamu wake kufuatilia mechi ya Jumatano ya Champions League dhidi ya Red Bull Salzburg. (Guardian)

Tottenham inamfuatilia mshambuliaji wa Gremio raia wa Brazil Everton Soares, huku mtaalamu mkuu soka Steve Hitchen akimtazama mchezaji huyo wa miaka 23 katika michuano ya Copa Libertadores. (Sky Sports)

Manchester United ina mpango wa kuwasajili wachezaji wawili wa safu ya mashambulizi baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kuomba kuimarisha kikosi chake zaidi. (Star)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer

Arsenal itawasilisha ombi la kutaka kupunguziwa bei ya kumnunua beki wa kati na nyuma wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi cha Unai Emery. (Sun)

Monaco wana nafasi ya kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 31, anayewachezea kwa mkopo huku tetesi zikisema kwa ada hiyo ni robo ya £29m iliyolipwa mwaka 2016. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Rex Features

Real Madrid imemtambua kipa wa Athletic Bilbao Mhispania Unai Simon, 22, kama mchezaji ambaye huenda akachukua nafasi ya kipa wao wa sasa Mbelgiji Thibaut Courtois, 27. (El Desmarque, via AS)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemtaja Harry Kane wa Tottenham kama mshambuliaji mahiri lakini amekiri kuwa haoni kama klabu yake itafanikiwa kumhamisha nyota hiyo wa miaka 26 kutoka London kaskazini. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema angelipendelea kumsajili Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye mkataba wake katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwezi Januari. (ESPN)

Brendan Rodgers amemwambia kiungo wa kati James Maddison kuwa Leicester ni mahali anapoweza "kujikuza" licha ya Manchester United kuonesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 22. (Leicester Mercury)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption James Maddison

Juventus inafanya mazungumzo na Mario Mandzukic kuhusu uhamisho wake kutoka klabu hiyo mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Croatia wa miaka 33 amekuwa akilengwa na Manchester United. (Mirror)

Vilabu vya Derby, Huddersfield na Swansea vinamfuatilia mchezaji wa safu ya kati wa Fleetwood Kyle Dempsey, 24. (Football Insider)

Tetesi Bora Jumatano

Mchezaji wa zamani wa Liverpool wa safu ya kati Dietmar Hamann anasema kuwa amepata fununu kwamba Reds "wanahamu sana" ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Sky Germany - via Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jadon Sancho

Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza kama sehemu ya kuondokeana nae kabisa. (Mail)

Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Sport)

Mchezaji wa safu ya kati ya Real, Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Isco, kiungo wa kati wa Real Madrid

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic,38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A.

Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. (Goal)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii