Slavia Prague 1-2 Barcelona: Lionel Messi avunja rekodi nyingine licha ya ushindi mwembamba

Goli la Barcelona

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jitihada za Luis Suarez akijaribu kufunga katika eneo gumu lakini Peter Olanyika akajifunga

Lionel Messi alikua mchezaji wa kwanza kufunga katika misimu 15 ya Ligi ya mabingwa mfululizo wakati Barcelona ilidai ushindi mwembamba huko Slavia Prague.

Nahodha Messi aliipa Barca ushindi wa mapema baada ya kupata pasi kutoka kwa kiungo Arthur.

Barcelona ambao wako juu kwenye ligi ya La Liga, kwa sasa wameshinda mechi sita mfululizo kwenye michuano yote.

Matokeo hayo yanafanya kikosi cha Ernesto Valverde kuwa kinara kwenye kundi F ikiwa na alama saba kutoka kwenye michezo mitatu, alama tatu juu ya Inter Milan na Borussia Dortmund.

Timu hizo mbili zilikutana kwenye uwanja wa Giuseppe Meazza , huku Inter ikishinda 2-0. Penalti ya Martinez ikiokolewa, huku kiungo Antonio Candreve akifunga goli la ushindi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Messi avunja rekodi

Matokeo yake yanawaweka vijana wa Ernesto Valverde juu ya Kundi F kwa alama saba kutoka michezo mitatu, alama tatu juu ya Inter Milan na Borussia Dortmund.

Pande hizo mbili zilikutana huko San Siro kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo, huku Inter ikishinda 2-0.

Barca walikuwa na bahati ya kupanda kileleni huku Slavia wakiwa na haki ya kutoka na ushindi.

Upande wa Prague ulikuwa na mashambulizi zaidi kuliko Barcelona, ​​haswa katika kipindi cha sekunde 60 wakati Marc-Andre ter Stegen alilala chini na kuokoa shambulio la Lukas Masopust na kisha kupangua shambulio la Olayinka juu ya mlingoti wa goli.

Barca walinusurika mwishoni huku vichwa vya Tomas Soucek na Olayinka vikiokolewa katika dakika za majeruhi

Slavia ni timu ya 33 ambayo Messi ameifunga katika kombe la mabingwa Ulaya ikiwa ni rekodi ya pamoja ilioafikiwa na Cristiano Ronaldo na Raul.

Huku akifunga magoli 15 msimu mmoja mfululizo , Messi yuko chini kwa goli moja zaidi ya mchezaji wa zamani wa Man United Ryan Giggs ambaye ana rekodi ya magoli 16 katika mechi tofauti za ligi ya mabingwa.

Nahodha huyo wa Barca angefunga magoli zaidi lakini alizuiwa na kipa Ondrej Kolar kabla ya kupiga nje akiwa karibu na goli.