Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.10.2019:Rodwell, Muller, Mourinho, Chilwell, Maddison, Sidibe

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tesesi za kuwa Jose Mourinho anaelekea Borussia Dortmund si za kweli

Kiungo wa kati wa Manchester City Jack Roderll,28 , yuko kwenye mazungumzo na Roma kuhusu kuhamia Serie A (Mail)

Manchester United wanamtolea macho mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller, 30. (Bild, via Star)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amekana uvumi kuwa kocha wa zamani wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho kuwa ataelekea kwenye klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Germany, via Mirror)

Manchester United haitarajii kuwasajili Ben Chilwell wa Leicester au James Maddison, 22, mwezi Januari.(Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Monaco haiwezi kumuita tena mlinzi wa timu ya Ufaransa Djibril Sidibe

Monaco haiwezi kumuita tena mlinzi wa timu ya Ufaransa Djibril Sidibe, 27, kutoka Everton anakochezea kwa mkopo, kutokana na tetesi kuwa mfaransa huyo anahusishwa na kuelekea AC milan.(Liverpool Echo)

Paul Scholes anaamini klabu yake ya zamani Manchester United ijaribu kumsajili mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil,31, ili kutatua tatizo la safu ya ushambuliaji (BT Sport, via Evening Standard)

Leicester wanahusishwa na taarifa kuwa wana mpango wa kumsajili kiungo Kerem Baykus,19. (Fotospor - in Turkish)

Mkurugenzi wa Wolves sporting Kevin Thelwell anasema uhamisho wa mkopo haumfai kiungo wa kati Gibbs-White, akisisitiza kuwa mchezaji huyo, 19 ''hajashindwa'' (Express and Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester United wanamtolea macho mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller

Crystal Palace wamepata pauni milioni 22.5 baada ya kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Aaro Wan-Bissaka,21, kwenda Manchester United.(Evening Standard)

Manchester City nusura wamkose Pep Guardiola kutokana na kukosekana kwa mazingira mazuri ya klabu hiyo.(Independent)

Kiungo wa kati Ronald de Boer,49, karibu ajiunge na Manchester United mwaka 2000 lakini alishauriwa kutofanya hivyo na aliyekuwa kocha wa wakati huo Louis Van Gaal, ambaye alienda kuwa meneja wa United mwaka 2014.(FourFourTwo)