Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 26.10.2019: Pogba, Bale, Mbappe, Nunez, Ozil, Luiz

Kiungo wakati wa man United Paul Pogba

Real Madrid iko tayari kuipatia Manchester United £90m pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30, ili kumsajili Paul Pogba, lakini inataka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuimarisha kiwango chake cha mchezo uwanjani . (El Desmarque, in Spanish)

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato)

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Bayern Munich inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa beki wa Atletico Bilbao na Uhispania Unai Nunez na wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Everton. (Goal.com)

Washauri wa kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kuhamia katika ligi ya MLS. (Mail)

Hatahivyo imeripotiwa kwamba Ozil amejiandaa kuendelea kuichezea Arsenal kwa muda mrefu. (Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kwamba wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz ,21, ambaye alijiunga na Aston Villa msimu huu. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa Brazil Willian, 31, hana mpango wa kurudi nyumbani wakati kandarasi yake itakapoisha mwisho wa msimu huu , licha ya ripoti zinazomuhusisha na klabu ya Barcelona , na kwamba anatumai kusalia Chelsea. (Metro)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anatumai kwamba mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 22, na beki mwenye umri wa miaka 21 Fikayo Tomori watatia saini kadarasi mpya katika uwanja wa Stamford Bridge. (Goal.com)

Klabu ya Itali Roma itaamua wiki ijayo iwapo itamsaini kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Jack Rodwell, 28 (Sun)

Manchester United imeanza mazungumzo na klabu ya Roma kuhusu kumpatia kandarasi ya kudumu beki Chris Smalling aliye katika klabu hiyo kwa mkopo . (Express)

Mkufunzi wa Norwich Daniel Farke anasema kwamba klabu hiyo ilijaribu kumnunua winga wa Man United na Wales Daniel James, 21, kutoka Swansea msimu huu. (Mirror)

Mkurugenzi wa klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorc amesema kwamba ripoti kwamba Jose Mourinho ni miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kuchukua mahala pake Lucien Favre hazina msingi wowote". (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe anasisistiza kuwa beki wa Uholanzi Nathan Ake, 24, hataathiriwa na uvumi wa kurudi Chelsea na anaendelea kuwa katika mpango wa muda mrefu wa klabu hiyo ya kusini mwa pwani. . (Daily Echo)

Wolves inafikiria kukubaliana kandarasi mpya na beki wa Ufaransa Willy Boly, 28, ambaye amesalia na chini ya miaka miwili katika kandarasi yake iliopo.. (Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Darren Bent anaamini kwamba Arsenal inaweza kumsaini beki wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, katika uhamisho wa bila malipo 2020 iwapo beki huyo wa Ubelgiji hatosaini kandarasi mpya. (Football Insider)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson amesisistiza kuwa Wilfried Zaha hakaribii kujiunga na Arsenal msimu huu kwa kuwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast amejiandaa kukabiliana na Arsenal wikendi hii . (Football.London)

Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal ilifanya uamuzi mzuri kumsaini Nicolas Pepe, 24, badala ya mshambuliaji wa Ivory Coast Zaha msimu huu. (Mirror)

Mkufunzi Mauricio Pochettino anasema kwamba kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 22, raia wa Argentina Giovani Lo Celso, 23, beki wa England Ryan Sessegnon, 19 - watahitaji kupewa muda wa miezi 18 kabla ya kuanza kuimarisha kiwango chao cha mchezo. (Telegraph)

Napoli na Juventus zilikosa fursa ya kumsaini mshambuliaji wa Salzburg aliyezaliwa Leeds raia wa Norway Erling Haland, 19 - ambaye amehusishwa na uhamisho wa Man United na Manchester City - kwa dau la Yuro milioni 4 wakati alipokuwa akiichezea timu ya Norway Molde. (Calciomercato)

Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo anasema kwamba mshambuliaji wa Italy Patrick Cutrone, 21, atachukua muda mrefu kabla ya kuingiliana na maisha ya Molineux. (Express and Star)