Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 27.10.2019: Bale, Jesus, Son, Phillips, Ceballos, Muller

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jurgen Klopp anataka kumleta Anfield, mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumleta Anfield mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, 20. (Express)

Kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, yuko huru kuhamia MLS, huku tetesi zinazomhusisha nyota huyo wa kimataifa wa zamani wa Ujerumani na DC United zikiibuka. (Bleacher Report via MLS official website)

Manchester City imeweka kiwango cha juu cha £100m kama bei ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 22, katika juhudi za kuvunja mpango wa Bayern Munich, kumnunua. (Sun)

Manchester United imesitisha mpango wa kusajili wa mshambuliaji wa Real Madrid na kiungo wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale,30, baada ya mchezaji huyo kujeruhiwa. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Man U yabadili azma ya kumsaini Gareth Bale,30, baada ya mchezaji huyo kujeruhiwa

Afisa mkuu mtendaji wa Manchester United Ed Woodward, amekubali kutoa £125m kubadilishana wachezaji wawili wa Bundesliga akiwemo kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz, 20, na mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 30. (Mirror)

Hatahivyo mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Hasan Salihamidzic anasema Muller hana mpango wa kuhama klabu hiyo mwezi Januari mwakani. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller (Kushoto) huenda akajiunga na Manchester United

Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min,27, raia wa Korea Kusini, anafuatiliwa na Juventus na Napoli. (Express)

Real Madrid anajiandaa kuikosesha Arsenal matumaini ya kumpata mchezaji wa kimataifa wa Uhispania anayecheza safu ya kati Dani Ceballos, 23, kupitia mkataba wa kudumu kwa kumrudisha katika klabu hiyo msimu ujao . (AS, via Mail)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Real Madrid anajiandaa kuikosesha Arsenal matumaini ya kumpata Dani Ceballos

Barcelona imefanya mazungumzo na Inter Milan kuhusu uuzaji wa kiungo wa kimatiga wa Croatia Ivan Rakitic, 31. (Sport)

Manchester United na Manchester City zinamnyatia beki wa Rochdale wa England wa chini ya miaka -18 Luke Matheson, 17. (Star)

Beki wa Liverpool Joe Gomez imepata usumbufu wa kimawazo kwa kutopewa nafasi ya kucheza misimu huu huku Tottenham na Arsenal zikionesha ishara ya kutaka kumsajili nyota huyo wa miaka 22 raia wa Uingereza . (90min)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Tottenham na Arsenal zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Beki wa Liverpool Joe Gomez(Kushoto)

Ujumbe wa maafisa wa Manchester United ounajianda kuzuru Saudi Arabia huku tetesi kuhusu klabu hiyo kuchukuliwa na mwanamfalme wa taifa hilo la uarabini zikiendelea. (Mail)

Napoli haina mpango wa kumuuza hivi karibuni kiungo wa kati wa kimataifa wa Uhispania Fabian Ruiz, 23, anayelengwa na Manchester City. (Gazzetta dello Sport, via Inside Futbol)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Napoli haina mpango wa kumuuza Fabian Ruiz, 23, anayelengwa na Manchester City

Kocha wa Newcastle Steve Bruce amekiri kuwa hana uhakika ikiwa ataweza kukiimarisha kikosi chake dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari mwakani nakuongeza kuwa hajafanya mazungumzo yoyote na bodi ya usimamizi ya klabu hiyo. (Sky Sports)

Tetesi Bora Jumamosi

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Washauri wa kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kuhamia katika ligi ya MLS. (Mail)

Hatahivyo imeripotiwa kwamba Ozil amejiandaa kuendelea kuichezea Arsenal kwa muda mrefu. (Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kwamba wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz ,21, ambaye alijiunga na Aston Villa msimu huu. (Manchester Evening News)

Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal ilifanya uamuzi mzuri kumsaini Nicolas Pepe, 24, badala ya mshambuliaji wa Ivory Coast Zaha msimu huu. (Mirror)

Manchester United imeanza mazungumzo na klabu ya Roma kuhusu kumpatia kandarasi ya kudumu beki Chris Smalling aliye katika klabu hiyo kwa mkopo . (Express)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Beki wa Manchester United, Chris Smalling kwa sasa nachezea klabu ya Roma kwa mkopo