Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.10.2019: Sancho, James, Ceballos, Mbappe, Rakitic

Kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Jadon Sancho

Manchester United wanajiandaa kutimiza masharti ya Borussia Dortmund huku wakijiandaa kusaini mkataba na mshambuliaji wa England Jadon Sancho.

Timu hiyo ya Ujerumani huenda ikadai pauni milioni £100m kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 (Mirror)

Meneja wa Newcastle Steve Bruce anapanga kuweka dau la mkopo kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi wa tmu ya Chelsea mwenye umri wa miaka 19 anayechezea timu ya England ya vinaja wenye chini ya umri wa miaka 20 Reece James. (Sun)

Kurejea kwa wachezaji wa mkopo wa Real Madrid, akiwemo Dani Ceballos, mwenye umri wa miaka 23, katika Arsenal, kunaweza kuongeza fursa ya kuweka dau kwa ajili ya kiungo wa safu ya mashambulizi wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20. (AS)

Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Croatia Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari kwa "ofa" katika kipindi cha uhamisho wa wachezaji mwezi Januari, huku Manchester United na Juventus wakimfuatilia mchezaji huyo . (marca)

Southampton wanamtaka Erik Stoffelshaus, ambaye amekuwa akifanya kazi katika klabu za Schalke na Lokomotiv Moscow, awe mkurugenzi wao mpya wa mchezo ,huku Manchester United pia wakiwa na nia ya kumuajiri mkurugenzi huyo mwenye umri wa miaka 48 . (Sun)

Liverpool walivaa fulana maalum katika mechi yao dhidi ya Tottenham iliyokuwa na maandishi "Futuremakers" ili kuutangazia umma kuhusu azma ya mdhamini wao mkuu Global initiative ya kukabiliana na ukosefu wa usawa kwa kukiwezesha kizazi kijacho kujifunza, kupata rizki na ukuaji. (Liverpool Echo)

Mpiga picha mmoja anapanga kutuma ujumbe wa malipo kwa klabu ya Brescia kwa kumpasulia kamera yake baada ya mchezaji wa zamani wa safu ya mashambulizi wa Liverpool na Manchester Mario Balotelli, 29, kuipiga teke baada ya kukasirika alipoondolewa uwanjani na kuingizwa kwa mchezaji mwingine.(Sun)

TETESI ZA SOKA JUMAPILI

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Man U yabadili azma ya kumsaini Gareth Bale,30, baada ya mchezaji huyo kujeruhiwa

Manchester United imesitisha mpango wa kusamjili mshambuliaji wa Real Madrid na kiungo wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale,30, baada ya mchezaji huyo kujeruhiwa. (Mirror)

Manchester City imeweka kiwango cha juu cha £100m kama bei ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 22, katika juhudi za kuvunja mpango wa Bayern Munich, kumnunua. (Sun)

Afisa mkuu mtendaji wa Manchester United Ed Woodward, amekubali kutoa £125m kubadilishana wachezaji wawili wa Bundesliga akiwemo kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz, 20, na mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 30. (Mirror)

Hata hivyo mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Hasan Salihamidzic anasema Muller hana mpango wa kuhama klabu hiyo mwezi Januari mwakani. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller (Kushoto) huenda akajiunga na Manchester United

Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min,27, raia wa Korea Kusini, anafuatiliwa na Juventus na Napoli. (Express)

Real Madrid anajiandaa kuikosesha Arsenal matumaini ya kumpata mchezaji wa kimataifa wa Uhispania anayecheza safu ya kati Dani Ceballos, 23, kupitia mkataba wa kudumu kwa kumrudisha katika klabu hiyo msimu ujao . (AS, via Mail)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Real Madrid anajiandaa kuikosesha Arsenal matumaini ya kumpata Dani Ceballos

Barcelona imefanya mazungumzo na Inter Milan kuhusu uuzaji wa kiungo wa kimatiga wa Croatia Ivan Rakitic, 31. (Sport)

Manchester United na Manchester City zinamnyatia beki wa Rochdale wa England wa chini ya miaka -18 Luke Matheson, 17. (Star)

Beki wa Liverpool Joe Gomez imepata usumbufu wa kimawazo kwa kutopewa nafasi ya kucheza misimu huu huku Tottenham na Arsenal zikionesha ishara ya kutaka kumsajili nyota huyo wa miaka 22 raia wa Uingereza . (90min)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Tottenham na Arsenal zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Beki wa Liverpool Joe Gomez(Kushoto)

Ujumbe wa maafisa wa Manchester United ounajianda kuzuru Saudi Arabia huku tetesi kuhusu klabu hiyo kuchukuliwa na mwanamfalme wa taifa hilo la uarabini zikiendelea. (Mail)

Napoli haina mpango wa kumuuza hivi karibuni kiungo wa kati wa kimataifa wa Uhispania Fabian Ruiz, 23, anayelengwa na Manchester City. (Gazzetta dello Sport, via Inside Futbol)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Napoli haina mpango wa kumuuza Fabian Ruiz, 23, anayelengwa na Manchester City

Kocha wa Newcastle Steve Bruce amekiri kuwa hana uhakika ikiwa ataweza kukiimarisha kikosi chake dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari mwakani nakuongeza kuwa hajafanya mazungumzo yoyote na bodi ya usimamizi ya klabu hiyo. (Sky Sports)

Tetesi Bora Jumamosi

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Washauri wa kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kuhamia katika ligi ya MLS. (Mail)

Hatahivyo imeripotiwa kwamba Ozil amejiandaa kuendelea kuichezea Arsenal kwa muda mrefu. (Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kwamba wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz ,21, ambaye alijiunga na Aston Villa msimu huu. (Manchester Evening News)

Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal ilifanya uamuzi mzuri kumsaini Nicolas Pepe, 24, badala ya mshambuliaji wa Ivory Coast Zaha msimu huu. (Mirror)

Manchester United imeanza mazungumzo na klabu ya Roma kuhusu kumpatia kandarasi ya kudumu beki Chris Smalling aliye katika klabu hiyo kwa mkopo . (Express)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Beki wa Manchester United, Chris Smalling kwa sasa nachezea klabu ya Roma kwa mkopo