Franck Ribery ameomba radhi kwenye ukurasa wa Twitter baada ya kumsukuma mwamuzi

Franck Ribery

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Franck Ribery (kushoto) amefunga mara mbili katika michezo 9 tangu ajiunge na Fiorentina

Kiungo mshambuliaji Franck Ribery ameomba radhi kwa kumshukuma mwamuzi, kitendo kilichosababisha kutolewa kwa kadi nyekundu, baada ya Fiorentina kufungwa 2-1 na Lazio.

Mchezaji huyo 36, aliingia dakika ya 74, alizozana na mwamuzi Matteo Passeri baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.

Mchezaji mwa zamani wa Bayern Munich alieleza kuwa alikuwa ''amechukizwa'', na maamuzi ya kukanganya baada ya goli la dakika 89.

''Ninaomba radhi kwa wachezaji wenzangu, kocha na mashabiki'', Ribery aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

''Ninaomba radhi kwa bwana Passeri kwa sababu mwishoni mwa mchezo nilikua nimekasirika sana na nina matumaini anaweza kuelewa hali niliyokuwa nayo wakati huo.''

Fiorentina wanalalamikia goli la ushindi la Lazio lililofungwa na Ciro Immobile, lilianzia katika kufanya makosa yaliyosababishwa na Jordan Lukaku kupitia kwa winga Riccardo Sotil.

Klabu ilitaka kujua kwa nini mwamuzi Marco Guida hakuchunguza kitendo hicho kwenye skrini na kuchagua kuwasikiliza maofisa wa VAR pekee.

''Kwanini hakwenda kutazama?'' aliuliza kocha wa Fiorentina Vincenzo Montella.

''Ni jambo la kushangaza ikiwa mwamuzi hajiridhishi kutazama vipengele muhimu.

''Sote tulisimama kwa dakika nne kusubiri wakisubiri VAR kuona kama mwamuzi ataenda kutazama kwenye mashine hiyo au la, lakini hakwenda kuangalia kitu ambacho kingechukua dakika moja au mbili, lakini angalau tungekuwa na uhakika.''

Ribery alijiunga na Klabu ya ligi ya Serie A kwa uhamisho wa bure akitokea Bayern Munich alikocheza kwa misimu 12.