Tetesi za soka Ulaya Jumanne 29.10.2019: Bale, Xhaka, Lacazette, Smalling, Haaland, Rodwell

Mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23. (ESPN)

Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare, 20, na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23. (ESPN)

Mshambuliaji wa Wales na Real Madrid Gareth Bale ameitaka Real Madrid kutochapisha rekodi zake za kimatibabu. (ESPN)

Timu ya ligi ya China Shanghai Shenhua wamehusishwa na uhamisho wa Bale. (Marca)

Bale alielekea mjini London kukutana na ajenti wake siku ya Jumatatu huku hofu ikiendelea kuhusu hatma yake katika klabu ya Real Madrid. (Mail)

Real Madrid inasema kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham alielekea mjini London kwa sababu za kibinafsi. (Marca)

Roma imekataa fursa ya kumsaini aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Jack Rodwell, 28. (Corriere dello Sport, via Mail)

Tottenham imeambia Inter haitamuuza beki Jan Vertonghen, 32, mwezi Januari lakini klabu hiyo ya Serie A inatumai kwamba mchezaji huyo wa Ubelgiji atajiunga kwa uhamisho wa bila malipo katika ndirisha la uhamisho la msimu huu . (Guardian)

Kipa wa Southampton na England Fraser Forster, 31,yuko tayari mshahara wake kupunguzwa ili kuendelea na kazi yake katika klabu ya Celtic kwa kandarasi ya kudumu. (The Scotsman)

Nahodha wa Arsenal Granit Xhaka, 27, alitembelewa nyumbani na wachezaji watatu wakuu baada ya kuzomwa na mashabiki wa klabu hiyo wakati alipotolewa katika sare ya siku ya jumpili dhidi ya klabu ya Crystal Palace. (The Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal itakutana na Xhaka katika kipindi cha siku chache zijazo ili kujadili vitendo vyake baada ya kutolewa nje wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amependa chapisho la mtandao wa Instagram akitoa tamko kali kwa mchezaji mwenza Xhaka na kutoa wito kwa mkufunzi Unai Emery kufutwa kazi. (London Evening Standard)

Nahodha wa zamani wa England Alan Shearer anasema kwamba Xhaka huenda akapata shida kuruhusiwa kuichezea Arsenal baada ya kuonekana akiwatusi mashabiki. (Sun)

Beki wa England Chris Smalling, 29, anatarajiwa kurudi Manchester United mara moja baada ya huduma zake za muda mrefu katika klabu ya Roma kukamilika mwisho wa msimu huu licha ya uvumi wa kutaka kuhamia katika klabu nyengine ya Itali kwa mkataba wa kudumu.. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Napoli itawacha matumaini ya kumsaini mshambuliaji wa RB Salzburg mzaliwa wa Leeds na raia wa Norway Erling Haaland mwezi Januari kwa sababu wanatumai Man United itamsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Corriere dello Sport, via Talksport)

Newcastle inamtaka mshambuliaji wake raia wa Brazil Joelinton, 23, kuwaleta England watu wa familia yake huku wakihofia kwamba huenda matatizo yake uwanjani yanashinikizwa na hatua yake kuhamia taifa jipya. (Telegraph)

Beki wa Liverpool na Cameroon Joel Matip, 28, anatarajiwa kuendelea kukaa katika benchi baada ya kuumia tena katika jeraha alilokuwa akiliuguza na anaweza kuwa nje kwa hadi ya wiki sita zaidi.. (London Evening Standard)

Klabu ya Besiktas inataka kutamatisha mkopo wao wa miaka miwili na kipa wa Liverpool Loris Karius mapema na kumrudisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ujerumani Merseyside mwezi Januari. (Takvim, via Sun)

Tottenham inatarajiwa kutegemea vijana badala ya dirisha la uhamisho mwezi Januari , huku wachezaji kama yule wa taifa la Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, 17, miongoni mwa wale ambao wanatarajiwa kupewa nafasi. (Star)

Kiungo wa kati wa Liverpool James Milner, 33, anataka kusalia na klabu hiyo zaidi ya kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Guardian)

Maafisa watatu wa Arsenal waliwachwa vinywa wazi baada ya kusafiri ili kumtazama Eddie Nketiah akiichezea Leeds dhidi ya West Brom , kabla ya mchezaji huyo kutoshirikishwa katika mechi hiyo.(Athletic, via Star)

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Rafael Van der Vaart anataka klabu yake ya zamani kumsaini kiungo wa kati wa Ajax na Morocco Hakim Ziyech, 26, na kumtumia ujumbe mwenyekiti Daniel Levy. (Talksport)