Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2019: Mourinho, Sancho, Ibrahimovic, Lovren, Mandzukic, Bale

Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Man United ana hamu ya kuifunza Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images

Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kurudi katika soka ya Uingereza kutokana na lengo lake la kutaka kushinda mataji katika ligi ya Premia. (Sky Sports)

Mourinho ana hamu ya kuchukua uongozi wa klabu ya Arsenal iwapo ipo. (ESPN)

Manchester City inataka kumsajili Jadon Sancho kutoka klabu ya Borrusia Dortmund , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa katika chuo cha mafunzo ya kandanda katika klabu ya City kabla ya kuelekea Ujerumani atagharimu zaidi ya £100m. (Sport Bild, via Sport Witness)

Pia unaweza kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya LA Galaxy Dennis te Kloese ana mipango ya kukutana na Zlatan Ibrahimovic, 38, kujadili hatma ya mshambuliaji huyo kwa lengo la kumzuia kutoondoka katika klabu hiyo. (ESPN)

AC Milan iko tayari kuwasilisha ombi jingine la kujaribu kumsaini beki wa Liverpool na Croatia Dejan Lovren, 30. (Tuttosport, via Mail)

Juventus iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33, kwa Manchester United au Sevilla mwezi Januari , lakini wanataka kulipwa dau la £4.6m. (Calciomercato, via Mirror)

Wolves na Watford wanajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kulia wa klabu ya Royal Antwerp na Ureno Aurelio Buta 22 ifikiapo mwezi Januari kwa dau la £5m. (Mail)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30, bado anaungwa mkono na wachezaji wenza katika klabu hiyo. (Marca)

Ajenti wa Bale , Jonathan Barnett, amefutilia mbali uvumi kwamba raia huyo wa Wales anatarajiwa kuondoka Real Madrid na kujiunga na klabu moja ya China . (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City na Arsenal wanajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco, 27. (Mundo Deportivo, via Manchester Evening News)

Klabu ya Ujerumani ya Schalke inataka kumzuia kuondoka mchezaji wa klabu ya Everton ambaye yupo kwa mkopo katika klabu hiyo Jonjoe Kenny kusalia zaidi ya msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo kwa mkopo wa kudumu. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, lazima abadili mienendo yake ya kutaka kuheshimiwa zaidi kwa kuwa 'ana tabia za kitoto' , kulingana na mchezaji mwenza wa zamani Dani Alves. (Spor TV, via Independent)

Mshambuliaji wa Brazil Joao Pedro, 18, amepewa kibali cha kufanya kazi na atajiunga na Watford mwezi Januari.

Klabu hiyo ilikuwa na makubaliano ya dau la £2m na klabu ya Fluminense mwezi Oktoba 2018, lakini wamekuwa wakisubiri ombi lake la kibali chake cha kufanya kazi.. (Standard)

Liverpool, Borussia Dortmund na Barcelona wana hamu ya kumsajili winga wa Valencia na Uhispania Ferran Torres, 19.

TETESI ZA SOKA JUMATANO

Manchester United imekaribia kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic 33 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Tuttomercatoweb, via Express)

Arsenal, Liverpool na Manchester United wamekuwa wakiwasiliana na jopo la maafisa wa kiungo wa kati wa Uswizi na Borussia Dortmund Denis Zakaria, 22. (Sky Deutschland, via Inside Futbol)

Unaweza pia kusoma:

Mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 22, amepinga uvumi unaomuhusisha na Bayern Munich , akiandika katika mtandao wa Instagram kwamba uvumi huo ulikuwa uongo. (Manchester Evening News)

Juventus iliwatuma maskauti kutazama mechi ya Liverpool dhidi ya Tottenham na walikuwa wakimuangazia mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 27, mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 27, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Tuttosport, via Mirror)

Newcastle iko tayari kumsaini kiungo wa kati mwenye urefu wa futi sita na nchi nne raia wa Ufaransa Ibrahima Sissoko, 21, kwa dau la ya £13m kutoka klabu ya ligi ya daraja la kwanza Strasbourg. (Sun)

Manchester United iko kifua mbele kumsaini Red Bull Salzburg na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Halaand, 19. (Corriere dello Sport, via Manchester Evening News)

Lyon imewasiliana na ajenti wa mshambuliaji Oliver Giroud kuhusu uhamisho wa mwezi januari kutoka Chelsea kwa raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33 (Soccer Link, via Football.London)

Everton imekuwa ikimsaka kiungo wa kati wa Czech Republic na Spartak Moscow Alex Kral, 21. (Clubcall)

Mshambulauji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, amefichua kwamba alizungumza na rais wa Real Madrid Florentino Perezmwaka mzima kabla ya kupata uhamisho wa kuelekea Chelsea. (Talksport)

Wachezaji wa Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 27, kusalia kuwa nahodha wa klabu hiyo licha ya kuwatukana mashabiki alipotoka katika mechi iliotoka sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili.. (Times, subscription required)

Leicester na Watford ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia Ronald Sobowale - mpwa wa mchezaji wa Bayern Munich na nyota wa Austria David Alaba. Sobowale, 22, anaichezea timu ya daraja la nane katika ligi ya Bostick klabu ya kusini mashariki ya Whyteleafe na pia amefanyiwa majaribio na klabu ya Middlesbrough. (Mail)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, amesema kwamba huenda akajiunga na klabu ya La Liga kufuatia huduma yake ya miezi kumi na nane akiichezea LA Galaxy. (Metro)

Kiungo wa kati wa zamani wa Tottenham Rafael van der Vaart amekiri kwamba alimwambia mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumsaini kiungo wa kati wa Ajax na Morocco Hakim Ziyech, 26. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Arsenal na England Stan Flaherty, 17, ametumia muda wake mwingi kufanyiwa majaribio katika klabu ya Newcastle mwezi huu . (Newcastle Chronicle)

TETESI ZA SOKA JUMANNE

Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare, 20, na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23. (ESPN)

Mshambuliaji wa Wales na Real Madrid Gareth Bale ameitaka Real Madrid kutochapisha rekodi zake za kimatibabu. (ESPN)

Timu ya ligi ya China Shanghai Shenhua wamehusishwa na uhamisho wa Bale. (Marca)

Bale alielekea mjini London kukutana na ajenti wake siku ya Jumatatu huku hofu ikiendelea kuhusu hatma yake katika klabu ya Real Madrid. (Mail)

Real Madrid inasema kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham alielekea mjini London kwa sababu za kibinafsi. (Marca)

Roma imekataa fursa ya kumsaini aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Jack Rodwell, 28. (Corriere dello Sport, via Mail)

Tottenham imeambia Inter haitamuuza beki Jan Vertonghen, 32, mwezi Januari lakini klabu hiyo ya Serie A inatumai kwamba mchezaji huyo wa Ubelgiji atajiunga kwa uhamisho wa bila malipo katika ndirisha la uhamisho la msimu huu . (Guardian)

Kipa wa Southampton na England Fraser Forster, 31,yuko tayari mshahara wake kupunguzwa ili kuendelea na kazi yake katika klabu ya Celtic kwa kandarasi ya kudumu. (The Scotsman)

Nahodha wa Arsenal Granit Xhaka, 27, alitembelewa nyumbani na wachezaji watatu wakuu baada ya kuzomwa na mashabiki wa klabu hiyo wakati alipotolewa katika sare ya siku ya jumpili dhidi ya klabu ya Crystal Palace. (The Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal itakutana na Xhaka katika kipindi cha siku chache zijazo ili kujadili vitendo vyake baada ya kutolewa nje wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette amependa chapisho la mtandao wa Instagram akitoa tamko kali kwa mchezaji mwenza Xhaka na kutoa wito kwa mkufunzi Unai Emery kufutwa kazi. (London Evening Standard)

Nahodha wa zamani wa England Alan Shearer anasema kwamba Xhaka huenda akapata shida kuruhusiwa kuichezea Arsenal baada ya kuonekana akiwatusi mashabiki. (Sun)

Beki wa England Chris Smalling, 29, anatarajiwa kurudi Manchester United mara moja baada ya huduma zake za muda mrefu katika klabu ya Roma kukamilika mwisho wa msimu huu licha ya uvumi wa kutaka kuhamia katika klabu nyengine ya Itali kwa mkataba wa kudumu.. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Napoli itawacha matumaini ya kumsaini mshambuliaji wa RB Salzburg mzaliwa wa Leeds na raia wa Norway Erling Haaland mwezi Januari kwa sababu wanatumai Man United itamsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Corriere dello Sport, via Talksport)

Newcastle inamtaka mshambuliaji wake raia wa Brazil Joelinton, 23, kuwaleta England watu wa familia yake huku wakihofia kwamba huenda matatizo yake uwanjani yanashinikizwa na hatua yake kuhamia taifa jipya. (Telegraph)

Beki wa Liverpool na Cameroon Joel Matip, 28, anatarajiwa kuendelea kukaa katika benchi baada ya kuumia tena katika jeraha alilokuwa akiliuguza na anaweza kuwa nje kwa hadi ya wiki sita zaidi.. (London Evening Standard)

Klabu ya Besiktas inataka kutamatisha mkopo wao wa miaka miwili na kipa wa Liverpool Loris Karius mapema na kumrudisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Ujerumani Merseyside mwezi Januari. (Takvim, via Sun)

Tottenham inatarajiwa kutegemea vijana badala ya dirisha la uhamisho mwezi Januari , huku wachezaji kama yule wa taifa la Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, 17, miongoni mwa wale ambao wanatarajiwa kupewa nafasi. (Star)

Kiungo wa kati wa Liverpool James Milner, 33, anataka kusalia na klabu hiyo zaidi ya kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Guardian)

Maafisa watatu wa Arsenal waliwachwa vinywa wazi baada ya kusafiri ili kumtazama Eddie Nketiah akiichezea Leeds dhidi ya West Brom , kabla ya mchezaji huyo kutoshirikishwa katika mechi hiyo.(Athletic, via Star)

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Rafael Van der Vaart anataka klabu yake ya zamani kumsaini kiungo wa kati wa Ajax na Morocco Hakim Ziyech, 26, na kumtumia ujumbe mwenyekiti Daniel Levy. (Talksport)