Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 03.11.20119: Sane, Onana, Diallo, Sane, Everton, Emery

Bayern Munich inapania kumsaini winga wa Manchester City Leroy Sane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bayern Munich inapania kumsaini winga wa Manchester City Leroy Sane

Bayern Munich inapania kumsaini winga wa Manchester City Leroy Sane, lakini iko tayari kulipa euro milioni 80 pekee (£69m) kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Calciomercato)

Leicester inatarajiwa kuwa klabu ya kwanza ya ligi kuu England, kuweka dau la kumnunua mshambuliaji wa Metz na Senegal Habibou Diallo, lakini Newcastle pia wanamtaka mchezaji huyo wa miaka 24. (Express)

Manchester United iko tayari kuikosesha Liverpool nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Mirror)

Tottenham inatafakari uwezekano wa kumnunua kipa wa kimataifa wa Cameroon na Ajax, ambaye bei yake inakadiriwa kuwa £35m - Andre Onana, mwenye umri wa miaka 24, mwezi Januari mwakani. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye sasa anaichezea LA Galaxy katika ligi ya MLS, japo amehusishwa na tetesi za kurudi Manchester United, huenda akarejea klabu yake nyingine ya zamani, AC Milan. (Marca)

AC Milan inatarajiwa kukomesha mpango wake wa kumnunua mshambuliaji wa Brazil anaeichezea Gremiord, Everton Soares, mwenye umri wa miaka 23, ambaye pia anahusishwa na tetesi za kujiunga na Tottenham. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic, huenda akarejea klabu yake ya zamani, AC Milan

West Ham inajiandaa kumuuza mchezaji wa safu ya kati Mbrazil Carlos Sanchez, 33, kwa kima cha karibu £3.5 milioni mwezi Januari mwakani. (Football Insider)

Ole Gunnar Solskjaer anasema Manchester United inastahili kuangazia zaidi suluhisho la kufunga mabao baada ya kutoka sare tasa katika mechi yake na Bournemouth. (Manchester Evening News)

Barcelona na Manchester City wako tayari kumenyana katika kinya'nganyiro cha usajili wa kiungo wa kati wa Uruguay na Juventus, Rodrigo Bentancur, 22. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Arsenal, Unai Emery, amepuzilia mbali maswali kuhusu hatma yake katika klabu hiyo

Kocha wa Arsenal, Unai Emery amepuzilia mbali maswali kuhusu hatma yake katika klabu hiyo baada ya timu yake kutoka sare na Wolves katika mechi iliyochezwa katika uwanja wao wa nyumbani. (Express)

Wachunguzi wa vipaji wa Newcastle, walikuwa Elland Road siku ya Jumamosi kufuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa QPR na raia wa Jamhuri ya Ireland Ryan Manning, 23. (Football Insider)

Barcelona itamruhusu kiungo wa kati Mhispania Carles Alena, 21, ambaye anadaiwa kulengwa na Tottenham, kuondoka klabu hiyo kwa mkopo mwezi Januari mwakani. (Mundo Deportivo, via Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barcelona itamruhusu mchezaji wake Carles Alena, kuondoka klabu hiyo kwa mkopo

Afisa mkuu mtendaji wa Inter Milan, Giuseppe Marotta, amepuuzilia mbali tetesi kuwa mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, aliye na miaka 22, ataondoka klabu hiyo ya ligi ya Serie A ili kujiunga na Barcelona. (Goal)

Wolves wanajiandaa kuweka dau la £10m mwezi Januari kumnunua beki wa Preston, Ben Davies, 24. (Express)

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino, anajaribu kuitafutia mbinu mpya safu yake ya mashambulizi na huenda akatumia nafasi ya usajili wa wachezaji wa Januari mwakani kuwasaini wachezaji Tanguy Ndombele, 22, Giovani Lo Celso, 23, na Ryan Sessegnon, 19, ili kupata suluhisho la haraka. (Sky Sports)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii