Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 04.11.2019: Emery, Lallana, Mourinho, Allegri, Haaland, Saliba, Alena

Unai Emery Haki miliki ya picha Getty Images

Unai Emery amepewa mwezi mmoja kuokoa kazi yake kama mkufunzi wa Arsenal. (Mirror)

Kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, analengwa na vilabu vya China na ligi kuu ya soka, huku mkataba wake na Liverpool ukielekea kumalizika. (Telegraph)

Arsenal imejitenga na tetesi kuwa huenda ikamuajiri Jose Mourinho kama kocha wao mpya. (ESPN)

Mkuu wa soka wa Arsenal, Raul Sanllehi, ameripotiwa kuonekana akila chakula cha jioni na Mourinho lakini wawili hao hawajazungumza kwa miaka kadhaa.(London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal imejitenga na tetesi kuwa huenda ikamuajiri Jose Mourinho

Kocha wa zamani wa Juventus Max Allegri, ambaye aliwahi kuhusishwa na Arsenal, anapigiwa upatu kujiunga na Bayern Munich baada ya Niko Kovac kuondoka. (Bild, via Football Italia)

Meneja wa Leipzig Ralf Rangnick pia amehusishwa na nafasi ya ukufunzi iliyoachwa wazi Bayern Munich - naye Jose Mourinho akiwa mmoja wa wale wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo. (London Evening Standard)

Salzburg bado haijapokea ofa kutoka usajili wa mshmbuliaji wa Leeds-mzaliwa wa Norway, Erling Braut Haaland, 19, ambaye amehusishwa na vilabu vya Manchester United, Real Madrid na Juventus. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshmbuliaji wa Leeds Erling Braut Haaland ananyatiwa na Manchester United, Real Madrid na Juventus

Roma inajiandaa kufanya mkutano na Manchester United kuhusu mkataba wa kudumu wa beki wa England Chris Smalling na iko tayari kulipa euro milioni 10 kumpata kiungo huyo wa miaka 29. (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Manchester City, Mhispania David Silva, 33, anatarajiwa kukosa mechi ya Jumapili ya ligi ya premia watakapuzuru Liverpool baada ya kuumia misuli. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Silva, 33, anatarajiwa kukosa mechi ya Jumapili ya ligi ya premia Man City watakapuzuru Liverpool

Mkufunzi wa Real Madrid, Zinedine Zidane ana azma ya kumsaini beki wa Arsenal William Saliba, 20, ambaye kwa sasa yuko St Etienne kwa mkopo. (Express)

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Paris St-Germain, Kylian Mbappe, 20, siku moja ataichezea Real Madrid, kwa mujibu wa rais wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev. (Mail)

Kiungo wa kati wa Barcelona Mhispania Carles Alena,21, anayelengwa na Tottenham huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo kwa mkopo mwezi Januari mwakani. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption 'Kylian Mbappe, siku moja ataichezea Real Madrid' asema rais wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev

Mkufunzi wa Uholanzi,Ronald Koeman amethibitisha kuna kifunguu cha sheria katika mkataba wake ambacho kitamruhusu kuhamia Barcelona, ambako alicheza kuanzia mwaka 1989-95, lakini hadi baada ya kombe la Euro 2020. (Goal.com)

Washambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30 na raia wa Colombia James Rodriguez,28 hawakufanya mazoezi na timu ya kwanza siku ya Jumapili. (Marca)

Mkufunzi wa Real Madrid, Zinedine Zidane ana azma ya kumsaini beki wa Arsenal William Saliba, 20, ambaye kwa sasa yuko St Etienne kwa mkopo. (Express)

Tetesi Bora Jumapili

Manchester United iko tayari kuikosesha Liverpool nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Mirror)

Bayern Munich inapania kumsaini winga wa Manchester City Leroy Sane, lakini iko tayari kulipa euro milioni 80 pekee (£69m) kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bayern Munich, iko tayari kulipa euro milioni 80 pekee (£69m) kumpata winga wa Manchester City Leroy Sane

Ole Gunnar Solskjaer anasema Manchester United inastahili kuangazia zaidi suluhisho la kufunga mabao baada ya kutoka sare tasa katika mechi yake na Bournemouth. (Manchester Evening News)

Barcelona na Manchester City wako tayari kumenyana katika kinya'nganyiro cha usajili wa kiungo wa kati wa Uruguay na Juventus, Rodrigo Bentancur, 22. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rodrigo Bentancur alisaidia Uruguay kushinda mashindano ya vijana ya Amerika kusini mwaka 2017

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii