Tetesi za soka Ulaya Jumatano 06.11.2019: Haaland, Xhaka, McNeil, Wenger, McGinn

kiungo wa Arsenal Granit Xhaka Haki miliki ya picha Getty Images

Red Bull Salzburg imeweka bei ya pauni milioni 86 kama dau la usajili kwa mshambuliaji Erling Braut Haaland, 16. (Tuttosport - in Italian)

Arsenal inaweza kumuuza kiungo wake Granit Xhaka ,27, mwezi Januari baada ya kuvuliwa unahodha. (Mirror)

Manchester United wanafuatilia maendeleo ya winga wa Burnley na timu ya umri wa miaka 21 ya England Dwight McNeil, 19 (Sun)

Aston Villa itakataa ofa yoyote ya Manchester United kwa kiungo wa uskochi John McGinn,25.(Birmingham Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri atafaa sana kwa Manchester United, anasema kocha wa zamani wa timu ya taifa Italia Marcello Lippi. (Mail)

Allegri atakua chaguo zuri kwa Bayern Munich, anasema mshambuiaji wa zamani Luca Toni.(Sport1, via Goal)

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amesema angependa kushika nafasi iliyoachwa wazi kwenye klabu ya Bayern Munich. (Bein Sports)

Kiungo wa pembeni wa Chelsea na timu ya taifa ya England Mason Mount, 20, amekana kauli ya mchezaji mwezake wa zamani Mitchel van Bergen kuwa huenda akajiunga na Madrid au Barcelona. (Express)

Makamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward alitaka kumsajili kiungo wa Paris St-Germain Marco Verratti,27 na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Real Madrid Raphael Varane,26,(Manchester Evening News)

Real Madrid wamefanya mazungumzo na kiungo wa Napoli Fabian Ruiz,23, kuhusu uhamisho muhimu kuelekea Bernabeu msimu ujao. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema ana furahia namna anavyojitoa Christian Eriksen, 27 ingawa mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na taarifa za kuachana na klabu hiyo.(Football London)

Arsenal inapaswa ''kutumia pesa nyingi'' kumpata Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers kwenye klabu hiyo, anasema mchazaji wa zamani Paul Mason. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina Mauro Icardi, 26, anafanya ''kila kitu'' kufanikisha uhamisho wake kwa mkopo kutoka Inter Milan kwenda Paris St-Germain kuwa wa kudumu (RMC - in French)

Barcelona itamtazama kwa karibu kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Kai Havertz,20, juma hili katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico Madrid.(ESPN)

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 05.11.2019

Unalitamkaje jina la nyota huyu wa Liverpool?

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema anafahamu mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe,20 ''ana ndoto'' ya kukichezea kikosi cha mabingwa wa La Liga. (Goal)

Rangers striker Alfredo Morelos, reportedly a target for Aston Villa, says he has had no contact with any club but the Colombian, 23, added: "Many teams that would be offering a good amount of money for me." (Antena 2, via Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Rangers Alfredo Morelos, anayeripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Aston Villa, amesema hana mawasiliano na klabu yoyote lakini mchezaji huyo 23, amesema ''labda itokee timu itakayotangaza ofa nzuri kwake.''(Antena 2, via Birmingham Mail)

Mada zinazohusiana