Arsenal yamfuta kazi Unai Emery: Ni nini alichofanya raia huyo wa Uhispania na je ni makosa yake?

Unai Emery Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emery alishinda asilimia 55 ya mechi 78 akiisimamia Arsenal

Uamuzi wa Arsenal wa kumfuta kazi kocha Unai Emery baada ya kuhudumia timu hiyo kwa kipindi cha miezi 18 ni mfano mwengine wa klabu na mkufunzi aliyefeli katika jukumu la kupanga kumrithi mtu aliyewacha sifa nyingi.

Man United ni mfamo wa karibu - wakati Sir Alex Furgerson alipojiuzulu baada ya miaka 26 na mataji 38 aliyemrithi alikuwa David Moyes ambaye alifeli na kupigwa kalamu baada ya miezi 10.

Emery aliwasili mwezi Mei 2018 kumrithi Wenger - ambaye alikuwa katika klabu ya Arsenal kwa takriban miaka 22 akiwa na rekodi ya ufanisi wa Ulaya na Sevilla na mataji ya nyumbani akiifunza PSG, lakini ameshindwa kuiondoa klabu hiyo kutoka kwa kivuli cha raia huyo wa Ufaransa.

Hivyobasi tunauliza ni wapi ambapo mvua ilianza kumnyeshea Emery akiwa Arsenal?

Emery alishindwa kutibu matatizo ya Arsenal

Muda wa Wenger ulikuwa umekwisha Arsenal - wachache wangepinga hilo licha ya kuwa na kipindi kizuri akiwa mkufunzi wa klabu hiyo ambayo ilishinda mataji matatu ya Ligi , mataji saba ya FA mbali na mataji mawili ya nyumbani mwaka 1988 na 2002.

Uwanja wa Emirates ulikuwa umekuwa sumu huku mashabiki wakikata tamaa na Wenger kila wanaponcheza dhidi ya Liverpool, Man City na timu nyengine katika kinyang'anyiro cha kushinda taji la ligi.

Emery ambaye ana rekodi ya kushinda mataji matatu ya Ligi ya Yuropa akiifunza Sevilla na mataji mengine akiifunza PSG aliongoza miongoni mwa makocha waliotarajiwa kumrithi Arsene Wenger akipatiwa jukumu la kuisongesha mbele Arseneal na kuitoa katika kivuli cha Wenger.

Alifeli katika njia zote. Kulikuwa na mwangaza wakati walipotinga fainali ya kombe la Yuropa bila kufungwa lakini walifungwa vibaya na Chelsea katika mechi ya fainali.

Emery, kwa uwezo wake wote alishindwa kuisaidia Arsenal na shutuma kuu ni kwamba matatizo ya muda mrefu ya Arsenal yamesalia bila mtatuzi.

Arsenal chini ya ukufunzi wa Wenger, ilikuwa haiwezi kustahimili presha hususan wanapocheza ugenini. Emery hakuweza kutatua tatizo hilo. Na takwimu zilikuwa zinaumiza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uni Emery aliteuliwa kuwa mkufunzi wa Arsenal mwezi Mei 2018, akimrithi Arsene Wenger

Msururu wa mechi saba bila ushindi wowote uliomfanya Emery kupigwa kalamu ndio yalikuwa matokeo mabaya zaidi tangu Februari 1992 chini ya George Graham.

Wenger alichukua uongozi wa mechi 1,235 lakini hakuwa na msururu mbaya kama huo. Arsenal ilijipatia pointi 88 katika mechi 51 na Emery sawa na walivyojipatia pointi kama hizo wakiwa na Arsene Wenger katika mechi 51.

Anaiwacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya nane, pointi 19 nyuma ya viongozi Liverpool na pointi nane nyuma ya nafasi nne za kushiriki katika kombe la klabu bingwa Ulaya.

Emery aliijenga timu yake kwa shauku kubwa: Usajili wa beki Dvid Luiz kutoka Chelsea ili kuimarisha safu ya ulinzi .

Usajili wa Matteo Guendouzi, kiungo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa na ufanisi mkubwa lakini usajili wa winga wa Lille Nicolas Pepe, ndio ulioshindwa kuzaa matunda huku Kieran akiwasili kutoka Celtic na jeraha na hadi kufikia sasa ameshindwa kuokoa timu.

Kwa ufupi hii ni Arsenal ile ile ya zamani - na sio kwa njia nzuri.

Arsenal iimekuwa na washambuliaji wazuri kupitia Alexander Lacazette na Pierre - Emerick Aubameyang lakini hata tishio lao haliwezi kuziba makosa ya Emery.

Kukosekana kwa mawasiliano

Ni mojawapo ya sababu za kwanza kwamba mkufunzi huyo alishindwa kuwasilisha ujumbe kwa wachezaji kutokana na hatua yake kushindwa kuzungumza Kiingereza vizuri na kocha huyo alifanya kila juhudi kuwasiliana kwa njia hiyo tangu alipowasili Arsenal.

Hakuna maswali kwamba Emery alipata shida kuwasiliana na wachezaji pamoja na mashabiki , akifanya maisha kuwa magumu katika uwanja wa mazoezi lakini pia kuimarisha uhusiano na mashabiki, swala muhimu sana kwa meneja mpya,.

Hatahivyo alikuwa mtaalam katika mambo yake na alikuwa na heshima kila mara hata chini ya maswali makali.

Mpango wa Emery na mawasiliano yaliefli kwengineko wakati ilipofika muda wa kumchagua nahodha atakayemrithi Laurent Kolscielny.

Badala ya kufanya uamuzi na kumchagua nahodha wake alimchagua mchezaji ambaye alikua ameshindwa kuonyesha ni kwani nini alisainiwa kwa £35m wakati alipowasili katika klabu ya Borussia Monchenglabach mwezi Mei 2016.

Je yalikuwa makosa ya Emery?

Emery anapaswa kulaumiwa pakubwa lakini alikuwa akifanya kazi katika klabu ambayo ilikuwa inaugua ndani kwa ndani chini ya umiliki wa Stan Kroenke.

Kroenke ni mmiliki asiyekuwepo , akiwa hayuko tayari kuwekeza fedha zinazohitajika kushindana na klabu nyengine ambazo pia zinawania mataji , ijapokuwa mwanawe Josh amekuwa akiwasiliana na mashabiki na kuzungumzia kuhusu hofu iliopo.

Ilikuwaje Ozil akakabidhiwa mkataba kama huo licha ya kiwango cha chini cha mchezo?

Na huu ulikuwa uamuzi mbaya zaidi - je Aron Ramsey aliwachiliwa kuondoka katika uhamisho wa bila malipo kujiunga na Juventus licha ya kusisitiza kwamba alidhania alikuwa ameafikiana kupata mkataba mpya?

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii