Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 20.12.2019: Ozil, Pogba, Ancelotti, Ibrahimovic, Borini, Haaland

Mesut Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Fotomac, via Football.London)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Fotomac, via Football.London)

Manchester United haitaruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kuondoka kuelekea Real Madrid katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)

Wachezaji wa United na maafisa wameshawishika kwamba Pogba ameichezea klabu hiyo mechi yake ya mwisho na atandoka mwezi Januari. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester United haitaruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kuondoka kuelekea Real katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)

Iwapo Carlo Ancelotti atakuwa mkufunzi mpya wa Everton uhamisho wake wa kwanza utakuwa jaribio la kumsaini mshambulaji wa zamani wa Man United Zlatan Ibrahimovic, 38.

Raia huyo wa Sweden atakuwa mchezaji aliye huru wakati kandarasi yake na LA Galaxy itakapokamilika. (Calcio Mercato)

Aliekuwa beki wa Everton Alan Stubbs ametuma pongezi kwa Duncan Ferguson na jinsi alivyoisaidia Everton kama kaimu meneja , akisema kwamba uteuzi wa Ancelotti hautawezekana bila kuwepo kwa mchezaji huyo wa zamani. (Talksport)

Chelsea ni miongoni mwa klabu za ligi ya Premia zinazotarajia kumsaini winga wa Real Madrid na Brazil Vinicius Junior, 19, mnamo mwezi Januari.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Iwapo Carlo Ancelotti atakuwa mkufunzi mpya wa Everton uhamisho wake wa kwanza utakuwa jaribio la kumsaini mshambulaji wa zamani wa Man United Zlatan Ibrahimovic, 38

Klabu zote mbili za Manchester zimefanya mazungumzo ya kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani mwenye umri wa miaka 20 Kai Havertz. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anaongoza baadhi ya wachezaji wa klabu ya Arsenal ambao wanafikiria kuhusu hatma yao katika klabu hiyo. (Independent)

Klabu ya Bruges nchini Ubelgiji inataka Yuro milioni 30 ili kumuuza mshambuliiaji wake Emmanuel Dennis huku klabu za Leicester, Brighton ana Southampton zikiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia. (Foot Mercato, via Leicester Mercury)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anaongoza baadhi ya wachezaji wa klabu ya Arsenal ambao wanafikiria kuhusu hatma yao katika klabu hiyo. (Independent)

Crystal Palace ina hamu ya kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Sunderland Fabio Borini, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Itali akiwa na klabu ya AC Milan kwa sasa. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)

Manchester United italazimika kulipa dau la £12m kwa ajenti Mino Raiola juu ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa RB Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19. (Sun)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Brazil Lucas Moura, 27, amekiri kwamba alikaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2012 kabla ya kuamua kujunga na PSG badala yake. (ESPN Brasil, via Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Tottenham na Brazil Lucas Moura, 27

Real Betis inataraji kwamba klabu ya Tottenham itakamilisha usajili wa kudumu wa Giovani lo Celso mwezi Januari. Kiungo huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo atagharimu £27.3m. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 25, anaweza kutoa ombi la kutaka kuhamia Juventus akiendelea kutafuta nafasi ya kwanza katika klabu hiyo.. (Goal)

Tetesi bora za Alhamisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arteta anakaribia kurejea Arsenal kama kocha mkuu

Manchester City wanataka walipwe pauni milioni moja ili wavunje mkataba na kocha wao msaidizi Mikel Arteta - Arsenal wanataka kumtangaza Arteta kama kocha wao mkuu mpya. (Mail)

Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 23, baada ya kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japani na klabu ya Red Bull Salzburgforward Takumi Minamino, 24. (Star)

Maelezo ya picha,

Je, hatimaye Eriksen kuihama Spurs Januari?

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amedai kuwa Spurs "hawaogopi" kumuuza kiungo mchezeshaji raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, kwa timu pinzani za England mwezi ujao. (Evening Standard)

Carlo Ancelotti anatarajiwa kutangazwa kama kocha mpya wa Everton baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 11.5 kwa mwaka. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ancelotti hivi kariuni ametimuliwa Napoli licha ya kuifikisha klabu hiyo hatua ya mtoano Champions League

Winga Mjerumani Leroy Sane, 23, anataka kuhamia miamba ya nyumbani kwao Bayern Munich na anapiga hesabu za kuihama Manchester City mwezi Januari. (Bild via Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bayern Munich wamekuwa wakimtaka Leroy Sane kwa muda, na sasa yeye pia ameonesha nia ya kujiunga nao.

Liverpool, Chelsea na Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinamnyemelea mshambuliaji kinda wa Nigeria anayechezea klabu ya Lille ya Ufaransa Victor Osimhen, 20. (Sky Sports)