Tetesi za Soka Ulaya 21.12.2019: Aubameyang, Havertz, Pogba, Xhaka, Wanyama

Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pierre-Emerick Aubameyang

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anataka kuihama Arsenal kwa udi na uvumba. (Mirror)

Manchester City na Manchester United wanakumbana na ushindani kutoka Liverpool, Real Madrid na Barcelona kumsajili kiungo Mjerumani Kai Havertz, 20 kutoka Bayern Munich. (Sun)

Manchester City walishtushwa na tangazo rasmi la Arsenal kumteua Mikel Arteta kuwa kocha wao mpya kupitia runinga na mitandao ya kijamii. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mikel Arteta amesaini mkataba wa miaka mitatu unusu kuifundisha Arsenal

Ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola amethibitisha kuwa kiungo huyo wa Ufaransa mwenye miaka 26 anataka kusalia Manchester United na "kushinda mataji", lakini anahitaji uungwaji mkono zaidi kutoka klabuni. (Telegraph)

Raiola pia amesema kuwa "anajisikia vibaya" kushindwa kuwaunganisha Pogba na kocha Mfaransa wa Real Madrid Zinedine Zidane katika dirisha lililopita la usajili. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Erling Haaland (kushoto) na Paul Pogba wote wanawakilishwa na ajenti Mino Raiola.

Wakati huo huo, United watakataa kuunganisha mustakabali wa Pogba na makubaliano yeyote ya usajili na mshambuliaji wa orway na klabu ya RB Salzburg Erling Braut Haaland, 19, ambaye pia anasimamiwa na Raiola. (Standard)

Mustakabali wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City utategemea vile kikosi chake kitakavyoandikisha matokeo kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (The Athletic, via Mirror)

Maelezo ya picha,

Man City msimu huu imekuwa na kiwango hafifu, je kuchukua Champions League ndi utakuwa 'ulinzi' wa Guardiola?

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini kuwa klabu hiyo itafanya usajili wa kueleweka mwezi Januari. (Manchester Evening News)

United wanategemea kusajili wachezaji wawili mwezi ujao. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanyama kutimkia Ujerumani mwezi ujao?

Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 27, yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Hertha Berlin juu ya uwezekano wa usajili mwezi ujao utakaompeleka ligi ya Bundesliga. (ESPN)

Kocha wa Hertha Jurgen Klinsmann anataka kusajili kiungo mkabaji na anasuka mipango ya kumnasa kiungo wa Kenya na Tottenham Victor Wanyama, 28. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amemtaka mshambuliaji wake wa kimataifa Olivier Giroud, aondoke Chelsea.

Bordeaux wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa Ufaransa anatumai kujiunga na Inter Milan. (Goal)

Msambuliaji wa zamani wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, yupo radhi kuhamia Everton pale Carlo Ancelotti atakapokabidhiwa rasmi klabu hiyo. (Talksport)

Maelezo ya picha,

Zlatan Ibrahimovic amepita vilabu vya Malmo,Ajax, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, Paris St-Germain, Man United na LA Galaxy

Kiungo wa Ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 23, ameamua kuwa anataka kujiunga na miamba ya nyumbani kwao Bayern Munich.(Bild - in German)

Tetesi Bora za Ijumaa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mesut Ozil

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo wa miezi sita katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Fotomac, via Football.London)

Klabu ya Bruges nchini Ubelgiji inataka Yuro milioni 30 ili kumuuza mshambuliiaji wake Emmanuel Dennis huku klabu za Leicester, Brighton ana Southampton zikiwa miongoni mwa klabu zinazomnyatia. (Foot Mercato, via Leicester Mercury)

Maelezo ya picha,

Lucas Moura

Mshambuliaji wa Tottenham na Brazil Lucas Moura, 27, amekiri kwamba alikaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2012 kabla ya kuamua kujunga na PSG badala yake. (ESPN Brasil, via Mirror)

Manchester United italazimika kulipa dau la £12m kwa ajenti Mino Raiola juu ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa RB Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19. (Sun)

Crystal Palace ina hamu ya kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Sunderland Fabio Borini, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Itali akiwa na klabu ya AC Milan kwa sasa. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)