Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.12.2019: Sancho, Arteta, Gerson, Diop, Haaland

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea kuzishinda Manchester United na Liverpool katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa England Jadon Sancho

Chelsea itazishinda Manchester United na Liverpool katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa England Jadon Sancho, 19, kwa sababu wako tayari kufikia dau la £120m iliyotolewa na Borussia Dortmund. (Sun on Sunday)

Mikel Arteta amekubali kuwa kocha mkuu wa Arsenal baada ya kukosa kupata hakikisho kutoka kwa Manchester City kwamba atakuwa mrithi wa Pep Guardiola katika uwanja wa Etihad. (Sunday Mirror)

Tottenham Hotspur wamefanya mazungumzoya kumsaini kiungo wa kati wa Flamengo Gerson na ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22 kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji mwezi Januari. (90min)

Spurs pia wanataka kumleta beki wa Ufaransa Issa Diop, 22, ambaye thamani yake inakadiriwa na West Ham United kuwa £50m .(Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Spurs inapania kumsajili beki wa Ufaransa Issa Diop

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa klabu hiyo iko tayari kufanya kazi na Mino Raiola kumnasa mshambuliaji wa miaka 19-kutoka Norway Erling Haaland kutoka Red Bull Salzburg.(Sunday Mirror)

Raiola pia anamwakilisha kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, na ameambiwa na Real Madrid kuwa hawataweka dau la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwezi Januari. (Marca)

Kiungo wa kati wa Tottenham wa miaka 27-raia wa Denmark, Christian Eriksen yuko tayari kukataa uhamisho wa kwenda Manchester United mwezi Januari, licha ya kutokuwa na mkataba wowote msimu ujao. (Daily Star Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Tottenham, Christian Eriksen hana mpango wa kujiunga na Manchester United

Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili imekubali mshambuliaji wa Norway wa chini ya miaka -17 Bryan Fiabema kutoka Tromso. Kiungo huyo wa miaka 16- sasa atajiunga na chuo cha mafunzo ya soka ,Stamford Bridge. (Metro)

Arsenal, Borussia Dortmund na Bayern Munich zinapania kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji wa miaka 32-Dries Mertens kutoka Napoli kwa kima cha £8.5m. (Calciomercato)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Dries Mertens amefuifungia Napoli jumla ya mabao 116

AC Milan na Atletico Madrid zinataka kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United na Serbia, Nemanja Matic, 31. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

Manchester United, Everton na Southampton ni miongoi mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Barcelona wa miaka 19 Mfaransa Jean-Clair Todibo kwa £17m. (Sport)

Tetesi Bora Jumamosi

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anataka kuihama Arsenal kwa udi na uvumba. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pierre-Emerick Aubameyang

Manchester City na Manchester United wanakumbana na ushindani kutoka Liverpool, Real Madrid na Barcelona kumsajili kiungo Mjerumani Kai Havertz, 20 kutoka Bayern Munich. (Sun)

Manchester City walishtushwa na tangazo rasmi la Arsenal kumteua Mikel Arteta kuwa kocha wao mpya kupitia runinga na mitandao ya kijamii. (Mail)

Mustakabali wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City utategemea vile kikosi chake kitakavyoandikisha matokeo kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (The Athletic, via Mirror)

Maelezo ya picha,

Man City msimu huu imekuwa na kiwango hafifu, je kuchukua Champions League ndi utakuwa 'ulinzi' wa Guardiola?

Bordeaux wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa Ufaransa anatumai kujiunga na Inter Milan. (Goal)

Msambuliaji wa zamani wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, yupo radhi kuhamia Everton pale Carlo Ancelotti atakapokabidhiwa rasmi klabu hiyo. (Talksport)