Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 23.12.2019: Bellingham, Mertens, Matic, Barbosa, Ancelotti

Meneja mpya wa New Arsenal Mikel Arteta anamtaka winga wa Napoli Dries Mertens,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Meneja mpya wa New Arsenal Mikel Arteta anamtaka winga wa Napoli Dries Mertens,

Meneja mpya wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka winga wa Napoli Dries Mertens, mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji katika mkataba wake wa mwisho wa mwaka.(Calciomercato)

Arsenal pia wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Bayer Leverkusen Mjerumani Kevin Volland mwenye umri wa miaka 27. (Sky Sports)

Manchester United pamoja na klabu kadhaa za Ligi ya Ujerumani Bundesliga wanamlenga kiungo wa kati wa Birmingham City anayechezea Kikosi cha vijana wadogo cha England -Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 16, baada ya timu hiyo kuweza kufuzu. (Telegraph)

Maelezo ya picha,

Manchester United pamoja na klabu kadhaa za Ligi ya Ujerumani Bundesliga wanamlenga kiungo wa kati (mbele)

United hawatamtoa kiungo wao wa kati Mserbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkata wake mpya unamalizika mwezi Juni 2020. (Express)

Mchezaji anayelengwa na West Ham Gabriel Barbosa amekataa kufanya mazungumzo juu ya hali yake ya baadae baada ya klabu ya mchezaji huyo wa klabu ya Flamengo kushindwa na Liverpool. Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 23-ana cheza katika safu ya mashambulizi kwa deni nchini kwake Inter Milan. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa West Brom Mmisri Ahmed Hegazi, mwenye umri wa miaka 28.

Everton wamemuahidi kocha mpya Carlo Ancelotti kuwa atatumia pesa yake mwezi Januari wakati Italia itakapojiandaa kufanya kazi katika Goodison Park. (Star)

Mlinzi wa West Brom Mmisri Ahmed Hegazi, mwenye umri wa miaka 28, hakuchukuliwa na meneja Slaven Bilic kutokana na tukio lililotokea katika uwanja wa mazoezi. (Express & Star)

Mshambuliaji wa zamani wa Juventus Juventus Mroatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, amewasili Qatar kabla ya kuhamia Al-Duhail, licha ya kwamba awali alilengwa kuchukuliwa na Manchester United. (Sky Italia)

Maelezo ya picha,

Mroatia Mario Mandzukic ametua Qatar

Mshambuliaji wa Brescia and Italia Mario Balotelli anataka kubakia katika klabu hiyo ili mradi mmiliki wa klabu hiyo Massimo Cellino yuko makini kuendelea kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Football Italia)

Mshambuliaji wa Norway anayetarajiwa kufanya vizuri Bryan Fiabema mwenye umri wa miaka 16 amejipanga kujiunga na klabu ya Chelsea kutoka Tromso baada kuwavutia katika majaribio. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Brescia and Italia Mario Balotelli anataka kubakia katika klabu hiyo ili mradi mmiliki wa klabu hiyo

Tottenham Hotspur wamefanya mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa Flamengo Gerson na ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22 kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji mwezi Januari. (90min)

Spurs pia wanataka kumleta beki wa Ufaransa Issa Diop, 22, ambaye thamani yake inakadiriwa na West Ham United kuwa £50m .(Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Spurs inapania kumsajili beki wa Ufaransa Issa Diop

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anataka kuihama Arsenal kwa udi na uvumba. (Mirror)

Bordeaux wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa Ufaransa anatumai kujiunga na Inter Milan. (Goal)

Msambuliaji wa zamani wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, yupo radhi kuhamia Everton pale Carlo Ancelotti atakapokabidhiwa rasmi klabu hiyo. (Talksport)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa klabu hiyo iko tayari kufanya kazi na Mino Raiola kumnasa mshambuliaji wa miaka 19-kutoka Norway Erling Haaland kutoka Red Bull Salzburg.(Sunday Mirror)

Raiola pia anamwakilisha kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, na ameambiwa na Real Madrid kuwa hawataweka dau la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwezi Januari. (Marca)