Nyota wa 2020: Wanaopigiwa upatu katika Olimpiki ya Tokyo

Briana Williams, Bianca Andreescu na Gabriel Veron

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Briana Williams, Bianca Andreescu na Gabriel Veron

2020 ni mwaka wa mashindano ya Olimpiki ya Tokyo - ambayo yatatoa fursa ya washiriki nyota kuwa mabigwa wapya. Haya ni baadhi ya majina ya washiriki wanaotarajiwa kuwa tajika katika kipindi kama hiki mwaka ujao...

Miho Nonaka (Japan) - Upandaji miamba

Chanzo cha picha, Marco Kost

Maelezo ya picha,

Nonaka anayetarajia kuwa bigwa katika mchezo mpya kwenye Olimpiki

Bila shaka kuibuka na ushindi katika Olimpiki nyumbani ni jambo linalowezekana kwa mchezaji ambaye hakuwa anahafamika na kuwa bingwa kama ilivyotokea kwa mrukaji anayetumia fito Thiago Braz da Silva katika mshindano ya Rio.

Lakini kupata ushindi wa aina kwa mchezo ambao ni mara ya kwanza kujuishwa katika Olimpiki - kama huu wa kukwea miamba ni kitu cha kusisimua zaidi kuwa na matarajio naco. Na Miho Nonaka anatarajia kutimiza ndoto yake.

Ni mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu - ambaye alikuwa mshindi wa mashindano ya Dunia ya upandaji miamba 2018 na wakati huu atakuwa na mashibiki wengi wanaomshangilia nyumbani.

Japo yeye binafsi alikuwa anapigania pakubwa kuhakikisha hilo linfanikiwa alikuwa na matarajio kidogo kwamba mchezo huo utajumuishwa kwenye Olimpiki na kumpa msisiko zaidi wa kushiriki kwenye michezo hiyo.

"Kujumuishwa kwa mchezo huu ni mafanikio makubwa wakati ambao umeshawahi kuushiriki na kuwa mshindi pamoja na ule muonekano wa mandhari unapokuwa juu. Ni jambo la kufurahisha," ameiambia BBC.

Tom Schaar (USA) - Kuteleza kwenye ubao

Chanzo cha picha, Sean M. Haffey

Maelezo ya picha,

Schaar amekuwa akishiriki mchezo wa kuteleza kwenye ubao tangu akiwa kijana

Mchezo mwengine uliojumuishwa kwa mara ya kwanza ni kuteleza kwenye ubao - na matarajio ni kwamba Schaar, ambaye ana umri wa miaka 20 atakuwa mchezaji wa kiume anayepigiwa upatu.

Schaar alifanikiwa kufanya mizungungo mitatu iliyokamilika hewani katika nusu duara maalum ya mchezo huo na ni mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kushinda medali ya dhahabu katika mashindnao ya X. kwa wakati huu ana medali tisa kwa ujumla.

Mashindano ya Olimpiki ya mwaka huu yanalenga zaidi vijana na kutumai kwamba watu kama kima Schaar wanaposhiriki Olimpiki huku mkakati wa utumiaji mtandao wa Kijamii ukiimarishwa na kuwa mbinu moja ya kuleta mashabiki wambao mara nyingi hufurahikia mchezo wa riadha pamoja na wale wanaotazama wakiwa majumbani.

Briana Williams (Jamaica) - Riadha

Chanzo cha picha, Charlie Crowhurst

Maelezo ya picha,

Williams alishauriwa kujitokeza mwaka 2019 - je huu utakuwa mwaka wake?

2019 ulitarajiwa kuwa mwaka wa mwanariadha wa Jamaica lakini hilo halikutimia kama ilivyoratajiwa.

Briana Williams mwenye umri wa miaka 17, alionekana kuwa mrithi wa Elaine Thompson (2016) na Shelly-Ann Fraser-Pryce (2012).

Williams ambaye alikuwa ameweka rekodi katika Under-20 alishindwa kutimiza ndoto yake mwake huu baada ya kugundulika kwamba ana chembechembe za dawa ya kuongeza nguvu mwilini kabla ya kushiriki kwenye mashindano ya Dunia ya Qarar.

Mwakilishi wa Williams Emir Crowne alidai kwamba chembechembe hiyo ilipatakana baada ya kununuliwa dawa dukani ya kuponya homa na mafua na jamaa wake wa karibu. Hata hivyo Williams alikuwa ameonyesha dawa anazotumia kwenye fomu aliyojaza wakati anapimwa na maafisa wa Tume ya Kukabiliana na Dawa za Kuongeza Nguvu Mwilini ya Jamaica.

Maelezo hayo yalikubaliwa na Williams akakaripia kwa kitendo hicho lakini hakupigwa marufuku ya kushiriki mchezo huo.

Jambo la kipekee kwa William ni kasi yake na nguvu aliyo nayo wakati anakambia, kunako acha mashabiki wake vinywa wazi.

Williams alikuwa ametajwa katika kikosi cha Qatar 2019, lakini akajiondoa baada ya kuona kwamba mipange yake mazoezi ilikuwa imevurugika. Hata hivyo, aliamua kujitoa rasmi katika michezo ya watu wazima kwenye Olimpiki ya Tokyo 2020.

Gabriel Veron (Brazil) - Soka ya mpira wa miguu

Chanzo cha picha, MIGUEL SCHINCARIOL

Maelezo ya picha,

Mchezaji Veron na ile matarajio ya kupata magoli inasisimua wengi wenye kipaji.

Gabriel Veron huenda akawa mshambuliaji nyota wa Argentine. Na jina lake limeweka katika mizani moja na nyota kuingo wa kati Sebastian Veron.

Hata hivyo Veron ni raia wa Brazil anayelenga zaidi kufuata nyayo za somo yake Gabriel Jesus.

Kama tu mshambuliaji wa Machester City, Veron anatoka klabu ya vijana ya SE Palmeiras na mwezi Novemba alikuwa katika timu ya Brazil kwenye mashindani ya FIFA ya Vijana ya Dunia mbele ya mashabiki zake Brazil.

Alifunga magoli matatu na kuwa mshindi wa Tuzo ya mchezaji Bora wa FIFA. Pia anahishwa na kuhamia Ulaya hususan katika vilabu vya Machester.

Iwapo ataishia kusajiliwa na moja ya klabu za Machester City, atatarajia kutoka kwa namna ya kipekee zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Juan Sebastian - ambaye anakosolewa kama mmoja kati ya waliokatisha tamaa chini ya utawala wa Sir Alex Ferguson.

Bianca Andreescu (Canada) - Tenisi

Chanzo cha picha, Rene Johnston

Maelezo ya picha,

Andreescu tayari ni nyota Canada

Andreescu alishinda katika mashindano ya Kimataifa ya Tenisi ya US Open mwaka 2012 na yeye anafahamika na wengi.

Lakini yupo kwenye orodha hii kwasababu 2020, huenda ukawa mwaka ambao utamfanya kuwa nyota wa Dunia katika Tenisi.

Tofauti ni Serena Williams ambaye umaarufu wake unaendelea kudidimia - Andreescu alipata ushindi katika seti zote zalizocheza kwenye katika uwanja wa Flushing Meadows na kwa sasa Andreescu ndiye anayepigiwa upatu wa kuchua mahala pa Serena Williams.

Akiwa bado kijana, katika mji wake wa nyumbani Toronto amepewa jina la utani la "mahiri wa tenisi", huku Shirikisho la Tenisi Marekani likihoji : Je yeye ndiye mchezaji bora zaidi wa tenisi?"

"Hata hivyo wadogo kwa wakubwa watakaoshiriki michezo hiyo ni washindani wazuri lakini kati yao kuanzia Ashleigh Barty, Naomi Osaka hadi Belinda Bencic walio katika umri wa miaka ya 20 hivi ambao wana kipaji maalum hakuna aliye na uzeofu ambao Andreescu amepata," Shirikisho la Tenisi Marekani limesema.

Je kuna uwezekano kwamba mchezo huu ambao ni vigumu kwa mshindi kutabirika hasa kwa washiriki wanawake huenda mwaka Andreescu akawapiku wote kwenye mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Alex Albon (Thailand) - F1

Chanzo cha picha, Mark Thompson

Maelezo ya picha,

Albon anakibarua kigumu mwaka 2020

Albon mwendeshaji gari la Red Bull ni mshirika wa hivi karibuni zaidi katika mashindano ya Formula 1 ''Daraja la A'' lenye madereva sita wenye uwezo wa kuibuka na ushindi(Mercedes, Ferrari naRed Bull).

Awali Albon, alikuwa amejumuishwa katika timu ya Red Bull junior Toro Rosso 2019, kujaza pengo la Pierre Gasly wakati yeye alipohitajika kujumuika katika timu ya waandamizi baada ya Daniel Ricciardo kujiunga na Renault bila kutarajiwa.

Matokeo yake ya kuridhisha yakamfaya apewe fursa ya kushika usukani mwaka 2020. Hata hivyo, katika timu hiyo anakabiliana na Max Verstappen, mmoja kati ya wenye vipaji vya juu zaidi katika mchezo wa uendeshaji magari pamoja na Lewis Hamilton.

Verstappen ana kasi ya ajabu na Albon atahitajika kudhihirishia umma kwamba ana uwezo unaohitajika.

Ikiwa atafanikiwa, 2020 itakuwa mafanikio makubwa sana kwake ama kuonyesha kwamba pia yeye si mchache katika tumu hiyo.

Hii ni moja ya mbinu ya utafutaji washiriki mahiri katika katika mashindano ya Formula 1.