Tetesi za soka Ulaya Jumanne 24.12.2019: Haaland, Kolasinac, Diop, Sancho, Cavani, Kessie

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa man United paul Pogba

Real Madrid wamemwambia ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola kwamba hawatomsaini kiungo huyo wa kati mwezi Januari.. (Mail)

Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la £44m na Real Madrid, hatua itakayotoa fursa kwa mabingwa hao wa Uhispania kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Christian. (Mirror)

Beki wa Arsenal na Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac, 26, analengwa na Napoli pamoja na Roma. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la £44m na Real Madrid

Mkufunzi mkuu wa RB Leipzig Oliver Mintzlaff amefichua kwamba wanapata shida kushindana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji wa Norway Erling Haaland kutoka Salzburg. (Mail)

Tottenham watahitaji kulipa dau la £50m kumsaini beki wa Ufaransa Issa Diop mwenye umi wa miaka ,22, kutoka West Ham. (Express)

Spurs inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 pia analengwa na Manchester United. (L'Equipe - via Football 365)

Borussia Dortmund haitazuia uuzaji wa winga wa England Jadon Sancho, 19, mwezi Januari. (Bild)

Maelezo ya picha,

Borussia Dortmund haitazuia uuzaji wa winga wa England Jadon Sancho, 19, mwezi Januari . (Bild)

AC Milan wameweka dau la £26m kwa kiungo wake wa kati Franck Kessie, huku Wolves ikifikiria kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari.. (Calciomercato - in Italian)

Lyon inamnyatia kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24,. (L'Equipe - in French)

Atletico wameafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 32. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Atletico wameafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 32. (Star)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameungwa mkono kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, kwa makubaliano ya muda mfupi. (Express)

Everton wameshauriwa kumsaini mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 28, pamoja na mshambuliaji wa Southampton Danny Ings, 27. (Talksport - via Star)

Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anasema beki wa Croatia Filip Benkovic, 23, huenda akaondoka kwa mkopo mwezi Januari huku klabu ya Derby County. (Leicester Mercury)