Tetesi za soka Ulaya Alhamisi tarehe 26.12.2019: Werner, Pogba, Neymar, Haaland, Alonso, Cavani

Chelsea wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa RB Leipzig

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa RB Leipzig

Chelsea wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Express)

Kiungo wa kati wa kati Mfaransa Paul Pogba, 26, anataka kundoka Manchester United na kujiunga tena na klabu yake ya zamani ya Juventus. (Calciomercato - in Italian)

Barcelona itajaribu kusaini tena mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, katika msimu wa uhamisho wa majira ya joto. (Goal)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Barcelona itajaribu kusaini tena mkataba na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar

Mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33, amemaliza tetesi juu ya hali yake ya baadae kwa kukamilisha taratibu za kuhamia klabu ya Al-Duhail ya Qatari licha ya kwamba Manchester United kumtaka. (Mail)

Manchester United wako tayari kumpa Mnorway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 19 anayecheza katika safu ya mashambulizi mkataba wa pauni 200,000-kwa wiki kujiunga nao kutoka Red Bull Salzburg. (Sun)

Kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuwasiliana na Manchester United kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kwa pauni milioni 80 msimu ujao wa majira ya joto. (Daily Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

James Maddison, anatarajiwa kuwasiliana na Manchester United kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

Monaco wamejiunga na AC Milan na Manchester United katika harakati za kusaini mkataba na kiungo wa kati-nyuma wa Barcelona Mfaransa Jean-Clair Todibo, mwenye umri wa miaka 19. (Calciomercato)

Meneja anayekabiliwa na shinikizo wa West Ham Manuel Pellegrini anahitaji kusaini mikataba na wachezaji wanne mwezi Januari lakini wanaweza kumuacha mlinzi wao Issa Diop, 22, aondoke. (Express).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Monaco wamejiunga na AC Milan na Manchester United katika harakati za kusaini mkataba na Mfaransa Jean-Clair Todibo

Arsenal wanatarajiwa kumuuza mmoja wa washambuliaji wao na kumumleta kikosini mshambuliaji wa timu ya Lyon Mfaransa Moussa Dembele mwenye umri wa miaka 23. (Le10Sport - in French)

Everton na Atletico Madrid wanapambana katika kusaini mkataba na mchezaji wa klabu ya River Plate anayecheza katika safu ya mashambulizi Molombia Rafael Santos Borre, mwenye umri wa miaka 24. (AS)

Maelezo ya picha,

Arsenal wanamtaka Mfaransa Moussa Dembele

Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, mwenye umri wa miaka 30, anataka kubakia katika Roma wakati mkataba wake wa mkopo utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Roma Press)

AC Milan wanaimani ya kukamilisha mkataba wa kumrejesha tena katika klabu hiyo kiungo wa safu ya mashambulizi Msweden Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, mwezi Januari. (Mail)

West Ham wako makini kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Uhispania Unai Nunez, 22, kutoka Athletic Bilbao. (AS, in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

AC Milan wanaimani ya kukamilisha mkataba wa kumrejesha tena katika klabu hiyo kiungo wa safu ya mashambulizi Msweden Zlatan Ibrahimovic

Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo anawapatia wachezaji wake mapumziko ya siku moja ili wakae na familia zao kabla ya mechi dhidi Manchester City. (FourFourTwo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juan Sebastian Veron

Juan Sebastian Veron anasema kwamba kuna mazungumzo kati ya Estudiantes na kiungo wa kati wa Vissel Kobe Andres Iniesta kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 wa Uhispania kujiunga na klabu hiyo ya Argentine . (La Oral Deportivo, via Marca)

Liverpool watawasilisha ombi kwa Primia Ligi la kutaka haki ya kuvaa beji za Washindi wa kombe la dunia la Fifa kwenye fulana zao katika gemu za ndani. (The Athletic - subscription required)